Torintohot media Blog
Na. Jerome Mlaki wa Dar.
Mjumbe wa halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mh. Juma Simba ameendelea na ziara ya kutathimini utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo Ili kubaini mapungufu yaliojitokeza Katika utekelezaji yaweze kufanyiwa Kazi na kuleta maendeleo kwa wananchi.
Ziara hii imelenga kutembelea kata Tisa zilizopo Wilaya ya kigamboni lakini pia kuweka mikakati ya ushindi Katika uchaguzi mdogo kwenye kata ya kimbiji unao unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Kata ya somangile iliyopowilaya ya kigamboni jijini Dar es Salaa m Mh.Juma Simba Gadaffi ameitembelea na kusikiliza changamoto mbali zinazoikabili kata hiyo ikiwemo upinzani mkuu kutoka vyama vya upinzani kwani Ikumbukwe kwamba kata ya somangile iliyopowilaya ya kigamboni ndio makao makuu chadema Katika Wilaya hiyo hivyo chama Cha Mapinduzi Ili kiweze kupata nafasi na Katika kata hiyo hakina budi kijikite Katika utekelezaji wa miradi mbalimbali itakayo leta Imani kwa wananchi.
Mh. Juma Simba amesemaKuwa lazima kila mwanachama ajue wajibu wake na kutekeleza wajibu wake na kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo ndio itakuwa sababu kubwa kwa wananchi kukiamini chama na kukichagua Katika nafasi mbalimbali za uongozi.
Ziara hii iliambatana na kupokea wanachama wapya wa CCM ikiwemo kupokea Katibu wa Chadema Ndugu Salumu Juma Pazzy ambaye amerudisha kadi ya Chadema na kujiunga na CCM.
Pia wanachama wapya kadhaa wameongozwa Katika kiapo Cha kujiunga nachama Cha Mapinduzi pamoja na zoezi la ugawaji wa kadi kwa wanachama hao.
Ikumbukwe kwamba ziara hii inaongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mh Abas Mtemvu ziara ambayo imeleta hamasa na kuchochea umoja kichama na kasi ya utekelezaji wa miradi.
Kata ya Somangile kigamboni Katika ziara hii yalikusanyika matawi kadhaa Ili kuweza kupokea maelekezo kutoka kwa mgeni rasmi matawi hayo ni Kizani, mwenge, Gezs ulole, Malipika, Muongozo, Ndege, Shirikisho, Mboto Kichangani, Mboto mkwajuni, Mwigogo, Sala, Mwanzo Mgumu n.k wenyeviti wa mitaa na viongozi mbalimbali wamehuzuria Katika ziara hii.
0 maoni:
Chapisha Maoni