WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumanne, 4 Julai 2017

 02:52      No comments


 TAGS



wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi  akiwa pamoja watendaji kutoka ATCB wa pili kutoka kulia ni Bi Sheila Minafi ambae ni Afisa Mauzo na Masoko wa ATCB,wa tatu kutoka kushoto ni Bwn.Zachy ambae ni mkuu wa idara ya Masoko na Biashara ya Nje na wa kwanza kulia ni Bwn. Salehe Khalifa ambae ni Meneja mkuu wa uzalishaji wa Kahawa ATCB wote kwa pamoja wakiifurahia tuzo walioipata katika Maonyesho ya Kibiashara ya 41 Saba Saba





Na Mwandishi wetu

 Kampuni ya Afri Tea & Coffee Blenders (1963) Limited  iliyopata tuzo ya Mshindi wa Kwanza  kwa wazalishaji bora wa bidhaa za ndani katika maonyesho ya 41 ya biashara ya kimataifa   imewashukuru  Watanzania wote kwa  kuendelea kuzipenda, kuzinunua na kutumia bidhaa zao bora,nchini kote na kuwataka kutembelea  banda lao  katika viwanja vya maonyesho Sabasaba.

Ambapo katika moja ya swali ambalo mwenyekiti alipata kuulizwa na Raisi Magufuli lilikuwa hivi na ni swali ambalo linatija pamoja na kuchangia sana katika kutoa fursa na tuzo kwa kampuni hii mbapo aliulizwa kuwa ni wapi haswa wanakoitoa chai

"Tunapata Majani ya chai kutoka kwa wakulima wadogowadogo wa hapa nchini Tanzania waliopo sehemu mbalimbali kama vile Lupembe-Njombe,Mponde,Tanga,Iringa nk."Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ATCB  Abdullhakim Mulla alimjibu Raisi Magufuli


Akizungumza  na waandishi wa habari, Mkuu wa Idara ya Masoko na Biashara ya Nje  wa kampuni  hiyo   Ndg. Zachy Mbenna   amesema  mwaka huu wamejipanga  vema kuwahudumia wateja na wameleta  bidhaa  mbalimbali  bora zikiwemo African Pride Tea iliyoboreshwa, Uji Bora Cereal Drink, kahawa ya Africafe 3 in 1, chai ya Green Label iliboreshwa, Maziwa ya Clover yanayodumu kwa muda mrefu na bidhaa za  viungo Vegeta. 

“Wateja wetu watakaotembelea katika  banda letu kununua  bidhaa zetu hapa Sabasaba watapata zawadi kemkem na punguzo kubwa la bei. Pia kuna sehemu maalum ambapo mteja wetu  ukifika katika banda letu la maonesho unaweza kuonja bidhaa zetu na kufurahia bidhaa zetu bora. Na ukinunua  bidhaa ya chai na kahawa  utapata zawadi za kikombe na kalamu nzuri za kisasa.” Ndg. Mbenna alisema. 

Aidha Mbenna  amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Dkt John  Pombe Magufuli  na Wizara ya viwanda na biashara  , na uongozi wa Tantrade   kwa  kuongeza siku za maonyesho kutoka tarehe 8 hadi 13 imetoa fursa  nyingine kwa watanzania kutembelea maonesho haya ya kimataifa ili kujifunza na kufurahia bidhaa bora kutoka Afri Tea and Coffee Blenders (1963) Limited.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *