
Torintohot
Na. Jerome Mlaki. 0789106710
Kampuni ya ZERA imezindua magari yake mapya aina ya ZERA ZMEV ambayo yanatumia nishati ya umeme.
Akizungumza katika uzinduzi wa magari hayo, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia nishati, Mhandisi Felichism Mramba, amempongeza ujio wa magari hayo ya umeme kwa sasa kwa kiwango kikubwa na kusema kuwa utaleta mapinduzi katika eneo la huduma za usafirishaji hapa nchini.
Mhandisi Mramba amesema kwa makadirio kwa sasa nchini kuna magari zaidi ya elfu 5 yanayotumia nishati ya umeme, hivyo ujio wa magari ya ZERA si tu utasaidia sekta ya usafirishaji bali pia itakuza vipato vya Watanzania.
Amesema gharama za kuendesha chombo hicho cha umeme kunapunguza gharama kwa zaidi ya asilimia 85.
"Gari hizi ambazo zinaweza kutembea kilomota 300 baada ya kuchaji ni hatua kubwa ya mafanikio na itaboresha mazingira kwani magari hayo hayatoi moshi," alisema.
Amesema vyombo vinavyotumia nishati ya umeme ni mwaroabaini ambao utaifanya Wizara ya Nishati kuongeza uzalishaji wa umeme ili kuendana na kasi ya teknolojia hii ikiwa ni pamoja na kuweka maeneo maalum ya kuchaji magari hayo ambapo magari mengine yatachajiwa kwa wakati mmoja.
"nataka niwahakikishie kwamba itapunguza sana ukali wa maisha lakini kwa kuagiza gari hizi ambazo gharama ni wakati tu wa kuagiza ila baada ya hapo hazibadikishwi oil wala kuhitaji matengenezo ya mara kwa mara," aliongeza Mramba.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ZERA, Emmanuel Kazimoto, amesema kampuni hiyo inalenga kujenga mfumo kamili wa usafiri wa umeme unaojumuisha uuzaji wa magari, ufungaji wa miundombinu ya kuchaji, ushauri wa kubadilisha magari ya kampuni kuwa ya vanema, pamoja na huduma za matengenezo.
Ameeleza mpango wao utaanza kwa kuingiza nchini magari ya kampuni hiyo ya ZERA yaliyokamilika (CBU), kisha hatua ya pili italenga kuingiza yaliyoandaliwa nusu (SDU) ili kuongeza ushiriki wa wataalamu wa ndani, huku hatua ya tatu ikilenga kuanzisha mkusanyiko wa magari hayo hapa nchini.
Aidha amesema magari hayo yametoka China lakini baadaye wataanza kutengeneza hapa nchini kwani tayari wameshapata kibali kutoka TISEZA cha kuyatengeneza nchini na kiwanda chake kitakuwa eneo la Kibaha, Pwani.
Amesema katika hatua za mwanzo, kampuni hiyo imeingiza magari kadhaa ya umeme kwa ajili ya maonesho na matumizi ya majaribio, ikiwa ni pamoja na yale ya abiria na mabasi madogo yanayoweza kutumika katika usafiri wa mjini. Mpango huo pia unatekelezwa kwa ushirikiano na wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika masuala ya nishati na miundombinu







0 maoni:
Chapisha Maoni