WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumatatu, 6 Novemba 2017

 04:26      No comments


MWANASHERIA
TAMWA

SHERIA ZA POMBE

• Intoxicating liquor Act 1968/ Sheria ya vileo
• Business licensing Act 1972/ Sheria ya leseni
• The traditional liquor ( Control of Distillation
(licensing) Regulation/ Sheria ya pombe za
kienyeji
• Law of the child Act 2009/ Sheria ya Mtoto
ya mwaka 2009
• By laws / Sheria ndogondogo

SHERIA ZINAZOHUSU POMBE ZINASEMAJE?

• Sheria ya leseni za vileo vimenyambulisha
aina mbalimbali za leseni ya vileo zinazoweza
kutolewa chini ya sheria hii.

• Leseni za rejareja:

• Leseni za jumlajumla:

SHERIA ZA VILEO CONT.............

• Hoteli:

• Restaurant/Mgahawa:

• Wanachama wa Club:

• MASHARTI YA KUPATA LESENI: Mtu yeyote raia wa
Tanzania anayo haki ya kupatiwa leseni ya vileo ili mradi
awe ametimiza umri wa miaka 18 mwenye akili timamu
na ambaye hajawahi kupatikana na kosa la jinai na awe
na eneo la kufanyia biashara linalokubalika kisheria

MASHARTI YA UNUNUAJI, UUZWAJI NA UNYWAJI WA

POMBE TANZANIA

• Sheria ya vileo ya mwaka 1968, Sheria ya Mtoto ya
mwaka 2009 na Sheria ndogondogo inakataza
unywaji, uuzwaji au ununuaji pombe kwa mtoto chini
ya miaka 18;
– Imekataza matangazo ya pombe kwa mtoto chini ya
miaka 18.

• Sheria ya vileo kifungu cha 68 na 69(1) imekataza
kuajiri mtu chini ya miaka 16 kuuza pombe na
kumuuzia pombe Sheria ya mtoto 2009 kifungu cha
17 imemkataza mtoto chini ya miaka 18
Sheria ya vileo kifungu cha 69(2)imekataza kuruhusu
mtu mwenye umri chini ya miaka 16 kukaa katika
eneo la kuuzia pombe na kurusu eneo la biashara
kutumika kama danguro.

MASHARTI YA UUZWAJI,UNUNUAJI NA UNYWAJI

POMBE TANZANIA CONT.................

• Sheria ya vileo, Sheria ndogondogo, inakataza kuuza pombe
kwa muda ambao ni kinyume cha sheria

BAR
• Jumatatu mpaka Ijumaa – saa 12.00 jioni hadi saa 5.00 usiku.
Jumamosi , Jumapili na sikukuu – saa 5.00 asubuhi hadi saa
8.00 mchana na saa 12.00 jioni hadi saa 6:00 usiku.

GROCERY
• Jumatatu mpaka Ijumaa – saa 2.00 asubuhi mpaka saa 1.00
jioni
• Jumamosi, Jumapili na sikukuu – saa 5.00 asubuhi hadi saa
8.00 mchana na saa 12.00 jioni hadi saa 6.00 usiku.

CHANGAMOTO

• Hakuna ufuatiliaji wa sheria ya kuuza pombe;
• Vyombo vilivyopewa dhamana vya kuhakikisha
sheria inatekelezwa havifuatilii ;
• Wengi hawana uelewa wa Sheria zilizopo ;
• Hakuna sera ya kitaifa ya kudhibiti matumizi ya
pombe kupita kiasi kuzuia madhara ya kiafya na
ukatili wa kijinsia;
• Sheria zilizopo zinazumgumzia zaidi uzalishaji na leseni
kuliko madhara yake na jinsi ya kutatua madhara mfano sheria
ya vileo, pombe za kienyeji na sheria za leseni ya mwaka
1972

Changamoto –CONT ....

• Sheria ndogondogo kutofautiana kwa kila eneo
husika hazisimami kwa pamoja.
• Sheria ya vileo ya mwaka 1968 inahamasisha
uuzwaji wa pombe nje ya muda uliowekwa kisheria
kifungu cha 61 kimewaongezea muda wa nyongeza
wa kuuza pombe kwa wamiliki wenye leseni
waliolipa ada kwa mazingira maalum
– Kanuni ya adhabu CAP 16 kifungu cha 14 (1)
kimetoa utetezi kwa mtu aliyefanya uhalifu akiwa
amelewa na kumchukulia kama alikuwa hajui
anachokifanya.

CHANGAMOTO – CONT..........

• Sheria ya umri wa mtoto wa kuuza, kununua
pombe zinakinzana mfano sheria ya vileo
kifungu cha 68, 69(1) na 69(2)inasema chini ya
miaka 16 na Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009
kifungu cha 17 chini ya miaka 18.
• Sheria ya pombe za kienyeji hazijawekewa
muda maalumu wa kuuza au kununua pombe
kama sheria ya vileo ya mwaka 1968.

HATUA ZA AWALI ZILIZOCHUKULIWA NA TAMWA

PAMOJA NA WADAU WENGINE

• TAMWA walifanya warsha ya siku mbili
Morogoro tarehe 10 na 11/11/2015 na wadau
mbalimbali; kutoka kwa watoa maamuzi
kutoka wizara mbalimbali serikalini na wadau
mbalimbali
• Tuliweza kuafikiana maazimio kuhakikisha
kuwa kuna na sera na sheria zinazodhibiti
matumizi ya pombe kupita kiasi

MAAZIMIO YALIYOFIKIWA

• Kupitia sheria zilizopo ambazo zinaleta
mkanganyiko ili kuweza kupata Sheria moja.
• Kuwa na sera ya kitaifa inayozungumzia
pombe;
• Kudhibiti matangazo ya pombe itakayopelekea
athari kwa jamii mfano kwa watoto, afya N.K

MAAZIMIO YALIYOFIKIWA CONT......

• Kufanya tafiti za madhara ya pombe.
• Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, viongozi
wa dini kuendelea kotoa elimu ili watu wapate
uelewa zaidi ya madhara ya pombe ya kijamii;
• Kuwa na siku ya campaign ya ‘no alchohol’.
• Kufuatilia sera ya pombe
..................................................................................................

HALMASHAURI YA MANISPAA YA

KINONDONI

MADHARA YATOKANAYO NA POMBE

Imeandaliwa na Judith Kimaro
Social Welfare Officer

Oct 2017

UTANGULIZI

• Pombe ni moja ya vinywaji vinavyotumika
kwenye jamii zote za nchi zilizoendelea na
zinazoendelea kama Tanzania
• Kinywaji hiki kinaweza kutengenezwa kiasili au
kisayansi (kiteknolojia) kulingana na hali halisi ya
jamii hasa kwenye nyanja za kiasili, kiuchumi na
kitenolojia
•Kinywaji cha pombe kina faida na hasara
kulingana na utumiaji wake
•Kwenye jamii nyingi zinazoendelea kama vile
Tanzania pombe imekuwa na madhara mengi
hususani kijamii, kiuchumi na kiafya

UTANGULIZI.........

• Madhara mbalimbali ya kijamii, kiuchumi na kiafya
yanayotokana na unywaji pombe yametoeka nchini
tanzania
• Manispaa ya Kinondoni ni miongoni mwa maeneo ya
Jiji ambapo pombe zinanywewa kwa kiasi kubwa
kama sehemu ya starehe.
• Kuna idadi kubwa ya kumbi rasmi za starehe na bar
2069 zilizosaajiliwa mwaka 2016 (chanzo Afisa
biashara Mansipaa)
• Mbali ya maeneo yasiyo rasmi ambayo huuza pombe
za kienyeji na za kigeni

SABABU ZINAZOPELEKEA WATU

KUNYWA POMBE

• Kuongezeka kipato
• Matatizo ya kifamilia yanayopelekea
msongo wa mawazo
• Makundi mabaya
• Ukosefu wa ajira/ shughuli za kufanya
• Utandawazi/ Sayansi na teknolojia
• Asili/mila na desturi

FAIDA ZA POMBE

Unywaji wa pombe una faida ndogo kwenye
maeneo makuu mawili:
1. Kiuchumi
• Hutumika kama bidhaa ya biashara na chanzo
cha mapato binafsi na Taifa
2. Kijamii
• Kiburudisho kwa wanywaji (mpe masikini kileo
asahau shida zake)
• Huongeza mahusiano kwenye jamii,
huwakutanisha watu kwenye vilabu na baa

MADHARA YATOKANAYO NA UNYWAJI
POMBE KIJAMII, KIUCHUMI NA KIAFYA
KIJAMII
• Migogoro katika ndoa na mahusiano kwa mwaka 2016/17 iko 1134

Migogoro iliyosababishwa na pombe ni 266
Migogoro 76 imeweza kusuluhishwa

• Kuongezeka kwa watoto yatima
• Kuongezeka kwa vitendo vya ubakaji na ukatili wa kijinsia-Mwaka 2016/17
tumepata kesi 40 ambazo pia ziko mahakamani
• Familia kusambaratika (kuachana/kutengana)-Mwaka 2016/17 ni familia
27
• Familia zenye migogoro inayoendelea na usuluhishi ni 765
• Kuongezeka kwa watu wanaojiuza miili yao kwa jinsia zote
• Kuongezeka kwa watoto wa mitaani

MADHARA YANAYOTOKANA UNYWAJI

POMBE.......

KIUCHUMI
• Kukosa wafanyakazi wenye nguvu na akili
timamu (uzalishaji mali kupungua)
• Kurudisha nyuma pato binafsi na taifa kwa
ujumla
• Kupelekea jamii/ nchi kuwa tegemezi

MADHARA YANAYOTOKAN NA

UNYWAJI ......

KIAFYA
• Mwili kudhoofika kutokana na kukosa hamu ya
kula chakula
• Kupata magonjwa kama vile figo, mapafu,
moyo, UKIMWI, sukari, presha na magonjwa
ya kuambukiza
• Kupoteza maisha kutokana na ajali
zinazosabishwa na unywaji pombe kupindukia

Matukio ya ukatili wa kijinsia

yaliyojitokeza Jan-Oct 2017 Kinondoni

KIPIGO
(PHYSICAL
ABUSE)

UKATILI WA
NGONO (SEXUAL
ABUSE)

UKATILI WA
KISAIKOLOJIA

MALE 440 43 807

FEMALE 565 147 1379

JUMLA 1005 190 2186

MATUKIO
YALIYOCHANGIWA NA
UNYWAJI POMBE

64% 21% 23%

USHAURI/ MAONI

• Serikali iingize kwenye mitaala ya shule za msingi hadi
vyuo, elimu juu ya madhara ya unywaji pombe
• Halmashauri zisimamie sheria ndogo ndogo za udhibiti
uuzaji na unywaji pombe holela
• Vyombo vya habari vishirikishwe kikamilifu katika elimu
juu ya madhara ya pombe kwa jamii
• Serikali iweke kipaumbele mapambano ya madhara ya
unywaji pombe kama ilivyo matatizo mengine ya jamii,
mfano UKIMWI, malaria, madawa ya kulevya n.k
• Taratibu za ukuwaji wa utandawazi ziwekewe mipaka hasa
kwa watoto wanaendelea kukua
• Jamii ishiriki katika mapambano dhidi ya ulevi wa
kupindukia ili kuepusha madhara

HITIMISHO

• Madhara ya unywaji pombe ya kijamii,
kiuchumi na kiafya yataepukwa endapo
tutashirikiana kikamilifu na wananchi,
wanasheria na wataalamu wa elimu kwa ujumla
• Hii itapelekea kutengeneza jamii bora
itokanayo na kizazi kilichopo na kunusuru kizazi
kijacho na madhara ya pombe

ASANTENI KWA KUNISIKILIZA

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *