Jumatatu, 6 Novemba 2017
Utangulizi
• Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ni
shirika la umma chini ya Wizara ya
Viwanda, Biashara na uwekezaji,
lililoundwa chini ya Sheria ya
Viwango, Nambari 3 ya mwaka
1975, na kuanzishwa upya chini ya
sheria ya Viwango Na. 2 ya mwaka
2009.
MAJUKUMU MAKUU YA TBS
- Kutayarisha viwango vya
kitaifa katika sekta zote za
uchumi, biashara, na
huduma.
- Kutekeleza viwango katika
viwanda, biashara na
huduma.
Majukumu makuu ya TBS...
- Kuboresha bidhaa zinazozalishwa
nchini kwa ajili ya masoko ya ndani
na nje.
- Kuelimisha umma juu ya masuala
yote yanayohusu uwekaji na
usimamiaji wa viwango pamoja na
udhibiti wa ubora wa bidhaa
viwandani.
Majukumu makuu ya TBS...
- Kutoa mafunzo na ushauri
kuhusu masuala ya ubora na
usalama.
- Kudhibitisha usahihi wa vipimo
vinavyotumika viwandani na
katika sekta za huduma na
biashara.
TAFSIRI YA KIWANGO
Kiwango ni nini?
Andiko maalumu lililoandikwa au kuandaliwa
na wataalamu waliobobea katika nyanja ya
taaluma husika; hususani kuhusu ubora na
usalama wa bidhaa; ikiwemo mazingira ili
kuhakikisha kwamba bidhaa hiyo inakidhi
matakwa au matarajio ya mtumiaji au mlaji;
kwa kuhusisha wadau wote, wakiwemo
wasomi, wazalishaji, wadhibiti, walaji, vyombo
vya utafiti na ushauri.
Aina za viwango
1) Viwango wa bidhaa
viwango vya lazima vinavyoainisha matakwa ya bidhaa
husika.
2) Viwango vya kimwongozo
Viwango vya hiari vinavyomsaidia mzalishaji kukidhi
matakwa ya kiwango cha cha bidhaa.
3)Viwango vya kimaabara
viwango vya hiari vinavyotumiwa na wadhibiti ubora/
wazalishaji kuhakikisha bidhaa husika inakidhi
matakwa ya ubora na usalama kama ilivyoainishwa
katika kiwango cha bidhaa husika.
FAIDA ZA VIWANGO
- Huweka usawa katika uwanja wa
biashara;
- Huondoa mkanganyiko kuhusiana na
bidhaa;
- Husaidia kufungua masoko Zaidi;
- Hurahisisha biashara baina ya nchi na
nchi;
- Hutoa uhakikisho wa ubora, usalama,
kuaminika na ufanisi.
FAIDA ZA VIWANGO...
- Huipa serikali ufanisi wa kuunda
sheria zinazohusiana na masuala
ya afya, usalama na uhifadhi wa
mazingira.
- Hulinda afya na usalama wa
walaji/watumiaji wa bidhaa
mbalimbali.
Viwango Vya Pombe
• Tanzania tuna aina ya viwango mbalimbali
vya Pombe tofauti tofauti kwa uchacne ni
kama hivi;
• Viwango vya mivinyo (Wine Standards)-
fortified wine, still table wine, sparkling wine
• Pombe Kali(Spirits)-Gin, Vodka, Whisky, Rum,
potable spirit,Brandy
• Viwango vya bia –beer, opaque beer
standards na vingine vingi
Kukidhi matakwa ya Viwango vya
Pombe
MATAKWA YA KIWANGO
Kiwango kimetengenezwa ili kumuongoza
mzalishaji wa bidhaa aweze kuzalisha bidhaa
bora na salama kwa matumizi ya binadamu
na inayokidhi mahitaji ya mauzo katika soko
la ndani na nje ya nchi.
MATAKWA YA KIWANGO...
Kiwango kina namba maalumu
inayokitofautisha na kiwango kingine.
Namba ya kiwango ni lazima ianze na TZS.
Mfano kiwango cha bia ni TZS 56
kilichochapishwa mwaka 2015 kama kiwango
cha kitaifa (TZS 56:2015)
Kiwango kinaelezea mahitaji na njia za majaribio
ya kimaabara kwa bidhaa inayozalishwa kwa ajili
ya matumizi mbalimbali.
MATAKWA YA KUZINGATIWA KATIKA VIWANGO
VYA POMBE
Malighafi na viungio
vinavyohitajika
Uhalisia wa bidhaa husika
Kikomo salama cha bacteria
Kikomo salama cha vichafuzi mfano
metal na sumu kuvu
vifungashio
MATAKWA YA KIWANGO CHA BIA
• Kiasi cha kilevi
• -Bia isiyo na kilevi, 0.5 max
-Kilevi cha chini 0.5 - 2.4
-Kilevi cha kati 2.5 - 4.0
-Kali 4.1 - 5.5
-Kali Zaidi 5.5
MATAKWA YA KIWANGO CHA BIA
• Mabaki metali ngumu (heavy metals)
-aseniki, risasi, Tini
• Sumu Kuvu
• Bacteria –Coliforms na Total Plate Count
MATAKWA YA KIWANGO CHA
MVINYO
• Kiwango cha kilevi, 6.5 -16.5%
• Sugar
-Dry wine : <4 g/l.
-Medium dry wine :4-12
-Semi‐sweet : 12-45
-Sweet wine > 45g/L
• Sulphur and sulphur dioxide
• Metal Ngumu
• Ikiwa imeongeozwa gesi ya carbondioxide, basi
gesi hupimwa
MATAKWA YA KIWANGO CHA WISKI
• Ethyl alcohol, %, Min, 37.5
• Volatile Acids, 400 mg/L
• Higher alcohols, 2 400mg/L
• Aldehydes, 400 mg/L
• Methanol, 300mg/L
VIFUNGASHIO VYA POMBE
Pombe ifungashwe kwenye vifungashio
vinavyofaa kwa chakula, vifungashio
ambavyo ni salama, vyenye ubora,
vinavyoweza kutunza ubora na usalama wa
chakula muda wote.
Pombe isifungashwe katika vifuko vya plastic
(plastic sachets), na pia ifungashwe katika
ujazo usiopungua 200mls.
VITU VYA KUZINGATIA KATIKA
MAANDISHI YA KIFUNGASHIO
Jina la aina ya pombe
Kiasi cha kilevi
Jina na anwani ya mzalishaji
Nchi inapotoka
Namba ya uzalishaji
Tarehe iliyozalishwa
Tarehe ya mwisho kutumia
Ujazo/uzito
Daraja la bia kwa kiwango cha bia
Maonyo mbalimbali yaliyopo kisheria
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 maoni:
Chapisha Maoni