WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Ijumaa, 16 Oktoba 2026


Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. CPA Venance Mwasse


Na Jerome Mlaki wa Dar. 0789106710

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeongeza mapato yake kutoka Sh bilioni 1.3 hadi takribani Sh bilioni 147.8 katika mwaka wa fedha 2025/26, mafanikio yanayohusishwa na mageuzi ya kiutendaji, uwekezaji katika miradi ya madini na kuimarisha usimamizi.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 16,2026 na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. CPA Venance Mwasse wakati akizungumza na Wahariri na Waandishi wa habari nakusema kuwa mageuzi ya kuimarisha shirika hilo yaliyoanza mwaka 2020 yameimarisha uwezo wa shirika kujiendesha na kupunguza utegemezi wa fedha za Serikali.

Dkt.Mwasse ametaja mafanikio mengine kuwa ni kuongezeka kwa watumishi kutoka 111 hadi karibu 800, kuingia mikataba minne ya ubia katika miradi ya madini ya kimkakati na kuendelea kuboresha mradi wa makaa ya mawe wa Kiwira, mkoani Songwe.

Akizungumzia kuhusu wachimbaji wadogo, amesema shirika limeongeza mitambo ya uchorongaji kutoka mitatu hadi 18 na kuweka mitambo 17 kwa ajili ya kuwasaidia wachimbaji, sambamba na kutoa mafunzo na ushauri wa kitaalamu."STAMICO ina masoko 44 na vituo vidogo vya ununuzi wa madini takribani 120, vinavyorahisisha uuzaji rasmi wa madini na kusaidia kupunguza utoroshaji."amesema

Halikadhalika ameongeza kuwa mchakato wa kuanzisha Benki ya Wachimbaji Tanzania umeanza kwa kushirikiana na wadau, kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa mitaji kwa wachimbaji wadogo.

Dkt. Mwasse amesisitiza kuwa STAMICO ni mwekezaji katika sekta ya madini, si mdhibiti, jukumu linalotekelezwa na taasisi husika za Serikali.

Kwa upande Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, amesema mafanikio ya STAMICO yanaonyesha umuhimu wa mageuzi katika taasisi za umma, huku akisisitiza haja ya kuimarisha utafiti na ukusanyaji wa takwimu za kisasa ili kupima matokeo ya shughuli zake kwa usahihi.

Kumbuka kuwa STAMICO, ilianzishwa  mwaka 1972 na inamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100,inashiriki katika mnyororo wa thamani wa madini kuanzia utafiti na uchimbaji hadi uchenjuaji, uongezaji thamani na biashara ya 

 


Na Jerome Mlaki wa Dar.

Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) limehimiza Halmashauri nchini kutumia fursa zinazopatikana katika masoko ya mitaji kutafuta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Wito huo umetolewa katika warsha ya mafunzo kuhusu ufadhili mbadala kwa Halmashauri kupitia fursa za masoko ya mitaji, inayofanyika Oktoba 15 na 16, 2026.

Katika warsha hiyo, Mkurugenzi wa Usimamizi na Uchunguzi wa Soko wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Bw. Exaut Julius, amesema masoko ya mitaji yanaweza kuwa chanzo cha ziada cha fedha kwa Halmashauri zinazolenga kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo, hususan katika sekta za maji, afya, usafi wa mazingira, masoko, vituo vya mabasi, majengo ya biashara na miundombinu mingine ya kiuchumi.

Amesema kuongezeka kwa mahitaji ya huduma za kijamii na miundombinu kunahitaji Halmashauri kubuni njia mbadala na endelevu za kugharamia miradi ya maendeleo badala ya kutegemea chanzo kimoja cha fedha.

Kwa mujibu wa Bw. Julius, ingawa ruzuku za Serikali na mapato ya ndani vinaendelea kuwa vyanzo muhimu vya fedha kwa Halmashauri, masoko ya mitaji yanaweza kutoa fursa ya kuongeza rasilimali fedha kwa ajili ya miradi inayokidhi vigezo vinavyohitajika.

Ameeleza kuwa baadhi ya nyenzo zinazoweza kuchunguzwa ni pamoja na hati fungani za miundombinu, hati fungani za kijani na mifumo mingine ya ufadhili inayoruhusiwa kisheria, kulingana na aina ya mradi na uwezo wake wa kifedha.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa si kila mradi unafaa kufadhiliwa kupitia masoko ya mitaji, akibainisha umuhimu wa kufanya tathmini ya kina ya gharama, mapato yanayotarajiwa, vihatarishi na uwezo wa kutimiza wajibu wa kifedha kwa wawekezaji.

Akizungumzia usimamizi wa ufadhili kupitia masoko ya mitaji, Bw. Julius amesema upatikanaji wa fedha unapaswa kuambatana na uwazi, utawala bora, uwajibikaji na ulinzi wa wawekezaji.

Amesema taasisi zinazotaka kutumia fursa hizo zinapaswa kuwa na mifumo madhubuti ya utoaji wa taarifa za kifedha, usimamizi wa vihatarishi na uzingatiaji wa sheria na kanuni zinazosimamia masoko ya mitaji.

Ameongeza kuwa maandalizi bora ya miradi ni muhimu katika kujenga imani ya wawekezaji na kuhakikisha fedha zitakazopatikana zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Bw. Julius amesema ushirikiano kati ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI, CMSA, DSE na Halmashauri ni muhimu katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inaandaliwa kwa viwango vinavyokidhi mahitaji ya ufadhili kupitia masoko ya mitaji.

Ameeleza kuwa TAMISEMI ina nafasi muhimu katika kuratibu mipango ya maendeleo ya Serikali za Mitaa, huku CMSA na DSE zikichangia katika maeneo yao ya kitaalamu ili kuwezesha Halmashauri kuelewa na kutumia fursa za masoko ya mitaji.

Aidha, amesema mifumo kama Special Purpose Vehicles (SPVs) inaweza kuchunguzwa kama mojawapo ya njia za kimuundo za kutekeleza miradi, kwa kuzingatia mahitaji ya mradi na masharti ya kisheria.

Katika warsha hiyo, washiriki wanatarajiwa kujengewa uwezo wa kutambua miradi inayoweza kufadhiliwa kupitia masoko ya mitaji, kuchagua nyenzo zinazofaa za ufadhili na kuelewa maandalizi yanayohitajika kabla ya kuwasilisha miradi kwa wawekezaji.

Masuala mengine yatakayojadiliwa ni pamoja na vyanzo vya mapato kwa ajili ya kutimiza wajibu wa kifedha, majukumu ya Halmashauri katika usimamizi wa miradi na taratibu zinazopaswa kufuatwa ili kukamilisha mchakato wa kupata ufadhili.

Washiriki wamehimizwa kutumia fursa hiyo kuuliza maswali, kubadilishana uzoefu na kujadili changamoto zinazoweza kujitokeza katika utekelezaji wa mifumo ya ufadhili mbadala.

Matarajio ni kwamba mafunzo hayo yatasaidia Halmashauri kubaini miradi ya kipaumbele inayoweza kuandaliwa kwa ajili ya kutafuta ufadhili kupitia masoko ya mitaji.

Warsha hiyo ya siku mbili inalenga kuimarisha uelewa wa Halmashauri kuhusu fursa za masoko ya mitaji na namna zinavyoweza kuchangia katika kupanua wigo wa upatikanaji wa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo nchini

 

Na Jerome Mlaki wa Dar 

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeweka mikakati ya kuimarisha ustawi wa maveterani wake kwa kuanza utaratibu wa kuwawezesha kupata bima za afya, kuanzisha akaunti maalumu ya shughuli zao na kuratibu utambuzi wa maveterani katika mikoa yote nchini.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti CHAMUATA Taifa, Jeremiah John Wambura, katika hafla ya kuwaenzi maveterani na kumkumbuka Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, iliyofanyika Oktoba 14, 2026, katika makao makuu ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), jijini Dar es Salaam.

Wambura amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuhifadhi historia ya Taifa, kuendeleza misingi ya umoja na kuhakikisha mchango wa waliotangulia kupigania uhuru wa Taifa na kusaidia nchi nyingi za Afrika kupata uhuru hautasahaulika.

Amesema kuwa maveterani wamekuwa na mchango mkubwa katika harakati za kupigania uhuru na wanapaswa kuendelea kuliombea Taifa na kulinda amani yake.“Siku ya kumbukizi ya kifo cha Hayati Mwalimu Julius Nyerere inapaswa kuwa fursa ya kuwaombea Watanzania na Taifa kwa ujumla ili tuendelee kuwa na amani, utulivu na mshikamano,” amesema Wambura.

Pia, amemtakia heri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akieleza matumaini yake kuwa juhudi za kuendeleza nchi zitaendelea kufanyika katika mazingira ya amani na utulivu.

Halikadhalika, amesisitiza umuhimu wa kuendeleza misingi ya uongozi na uwajibikaji, akihimiza maveterani kuendelea kuwa sehemu ya juhudi za kuelimisha jamii kuhusu historia ya Taifa na umuhimu wa kulinda amani kwa vizazi vya sasa na vijavyoAwali, akizungumza katika hafla hiyo, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawire (MNEC), amesisitiza umuhimu wa kutambua mchango wa maveterani na kuendeleza misingi ya chama, akieleza kuwa viongozi wanapaswa kujifunza kuthamini watu walioshiriki katika historia ya Taifa.

Mkandawire amesema Mwalimu Nyerere alikuwa mtetezi wa haki na wanyonge, akichangia pia harakati za ukombozi wa mataifa mbalimbali ya Afrika. Amehimiza Watanzania kutokubali kugawanywa kwa misingi ya dini au siasa, akisisitiza kuwa wananchi wote ni Watanzania bila kujali imani zao.

Ameongeza kuwa maveterani wana wajibu wa kuendeleza elimu kuhusu historia ya Taifa, huku akiwataka vijana kujifunza misingi ya amani, umoja na mshikamano ili kuilinda Tanzania na kuendeleza maendeleo.Naye Mwenyekiti wa Maveterani Mkoa wa Dar es Salaam, Yahaya Ngoma, ameeleza umuhimu wa kutambua mchango wa maveterani katika historia ya Taifa na kuhakikisha kazi zao zinaendelea kufahamika kwa vizazi vijavyo.

Aidha, Mzee Ngoma, ambaye ni muasisi wa Wimbo wa Taifa, amesema maneno yake yana uhusiano na mchango wa maveterani na harakati za kihistoria zilizohusishwa na mwaka 1953, kabla ya kuboreshwa mwaka 1964 na kiongozi wa bendi ya polisi aliyetajwa kwa jina la Mayagila.

Aidha, ameomba kuanzishwa kwa akaunti maalumu ya maveterani itakayosaidia kuratibu shughuli zao, kuwawezesha kukutana na kujadiliana kuhusu namna ya kuendeleza misingi ya umoja, upendo na mshikamano.

Pia, wamesema kuwa kuna mpango wa kuweka ofisi maalumu Dodoma kwa ajili ya kuratibu shughuli za maveterani na kuhifadhi kumbukumbu za mchango wao.

Miongoni mwa mipango iliyotajwa ni kuwatambua maveterani katika kila mkoa, kwa kuanza na angalau watatu kutoka kila mkoa ndani ya mwezi mmoja, pamoja na kuandaa mkutano wa kwanza wa maveterani kutoka nchi nzima utakaofanyika Dodoma.

Jumatano, 14 Oktoba 2026

 

Torintohotmedia


Na mwandishi wetu Dar.

Kampuni ya Tripbey imekuja na mfumo wa huduma za usafiri unaowawezesha wananchi kusafiri kwa ndege, mabasi na treni bila kulipa nauli kabla ya kuanza safari, hatua inayolenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za usafiri nchini Tanzania na katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Akizungumza leo Oktoba 14 ,2026 jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mfumo huo Balozi wa Tripbey Maulid Kitenge amesema kuwa kupitia huduma hiyo, watumiaji wanaweza kuomba tiketi za usafiri kwa kutumia programu ya simu ya Tripbey na kulipa gharama za safari baadaye, kulingana na masharti na vigezo vilivyowekwa na mtoa huduma.

"Mfumo huu unalenga kuwapa wananchi unafuu katika kupanga safari zao, hususani wale wanaohitaji kusafiri kwa dhalura au ambao hawana fedha za kutosha kulipia nauli mara moja."amesema Kitenge

Nakuomgeza kuwa "Katika utekelezaji wa huduma hiyo, Tripbey inatumia mfumo wa tathmini ya uwezo wa kifedha wa mtumiaji (Ability to Pay) ili kubaini kama ana uwezo wa kulipa gharama za safari baada ya kupata huduma.".

Aidha amesema kuwa tathmini hiyo inalenga kuhakikisha kuwa watumiaji wanaopata fursa ya kusafiri kwa utaratibu huo wanakidhi vigezo vya kifedha vilivyowekwa,huku wakizingatia masharti ya ulipaji wa nauli baada ya safari.

Amesema huduma hiyo pia inajumuisha aina mbalimbali za usafiri, zikiwemo ndege za ndani, mabasi ya Mikoani na Treni, jambo linaloweza kuwapa wananchi chaguo pana zaidi la kupanga safari zao kulingana na mahitaji yao.

Kwa upande wake  Afisa Masoko Mwendeshaji  Tripbey Idrisa Njeru amesema kuwa kupitia matumizi ya teknolojia ya kidijitali,TripBey inalenga kurahisisha mchakato wa kupata tiketi na kutoa mfumo mbadala wa malipo ya usafiri unaowawezesha watumiaji kupata huduma kwanza na kulipa baadae.

"Wananchi wanaotaka kutumia huduma hii wanashauriwa kufahamu masharti ya malipo, vigezo vya kustahiki na gharama zinazoweza kuhusishwa na huduma hiyo kabla ya kufanya maombi ya tiketi."amesema Njeru


 Na Jerome Mlaki wa Dar 0789106710

Tanzania imeeleza utayari wa kushirikiana na nchi wanachama wa Baraza la Mawaziri la Kanda ya Mashariki, Kusini na Kaskazini mwa Afrika (MOESNA) katika kuanzisha chuo kikuu cha kikanda kitakachojikita katika elimu, mafunzo, utafiti na ubunifu wa sekta ya usafiri wa majini.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Oktoba 13, 2026, Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, aliyemwakilisha Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema uamuzi huo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uwezo wa Afrika katika sekta ya usafiri wa majini.


Kihenzile amesema Tanzania pia itakuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Kumi wa MOESNA utakaofanyika Oktoba 15, 2026 jijini Dar es Salaam, ukiwakutanisha mawaziri 26 wanaosimamia uchukuzi na lojistiki kutoka nchi wanachama.


Amesema mkutano huo utajadili namna ya kuimarisha uunganishaji wa nchi, kurahisisha biashara na kuongeza usafirishaji wa mizigo na abiria kwa njia ya maji kati ya bandari za Afrika, huku ukilenga kuongeza ushiriki wa bara katika usafirishaji wa majini.


Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa MOESNA, Kassim Mpaata, amesema tayari wamepata ushirikiano kutoka Tanzania, Botswana na nchi nyingine katika kufanikisha ujenzi wa chuo hicho, ambacho kinatarajiwa kuwa kituo cha umahiri wa kikanda katika sekta ya usafiri wa majini.

Jumanne, 13 Oktoba 2026


Written by Alex Sonna


Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (kulia), Waziri wa Fedha wa Burundi, Mhe. Dkt. Alain Ndikumana (kushoto) na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Dkt. Ndiame Diop, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukutana na kujadili namna ya kuharakisha utekelezaji wa mradi wa kimkakati wa miundombinu wa Ushoroba wa Kati (Central Corridor), unaolenga kubadilisha mtandao wa usafirishaji wa kikanda kuwa kichocheo muhimu cha ustawi wa kiuchumi, uliofanyina kando ya Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia (World Bank Group), jijini Bangkok, nchini Thailand.

Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Kulia) (Mb), akizungumza wakati wa kikao cha pamoja kati ya Tanzania, Burundi na wawakilishi wa Benki ya Dunia wakiongozwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Dkt. Ndiame Diop (hayupo pichani), kando ya Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia (World Bank Group), inayofanyika jijini Bangkok, nchini Thailand, ambapo walijadili namna ya kuharakisha utekelezaji wa mradi mkakati wa miundombinu wa Ushoroba wa Kati (Central Corridor), unaolenga kubadilisha mtandao wa usafirishaji wa kikanda kuwa kichocheo muhimu cha ustawi wa kiuchumi. Kushoto ni Waziri wa Fedha wa Burundi, Mhe. Dkt. Alain Ndikumana.

Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (Kulia), Waziri wa Fedha wa Burundi, Mhe. Dkt. Alain Ndikumana (kushoto) na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Dkt. Ndiame Diop, wakiteta jambo mara baada ya kufanya mkutano uliojadili namna ya kuharakisha utekelezaji wa mradi mkakati wa miundombinu wa Ushoroba wa Kati (Central Corridor), unaolenga kubadilisha mtandao wa usafirishaji wa kikanda kuwa kichocheo muhimu cha ustawi wa kiuchumi kayika ukanda huo, wakati wa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia (World Bank Group), inayofanyika jijini Bangkok, nchini Thailand.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Bangkok, nchini Thailand)

Na Benny Mwaipaja, Bangkok, Thailand

Mawaziri wa Fedha wa Tanzania na Burundi, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar na Mhe. Dkt. Alain Ndikumana, kwa pamoja, wamekutana na wawakilishi wa Benki ya Dunia wakiongozwa na Makamu wa Rais anayehusika na Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Dkt. Ndiame Diop, kujadili namna ya kuharakisha utekelezaji wa mradi wa kimkakati wa miundombinu wa Ushoroba wa Kati (Central Corridor), unaolenga kubadilisha mtandao wa usafirishaji wa kikanda kuwa kichocheo muhimu cha ustawi wa kiuchumi katika ukanda huo.

Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Omar amesema kuwa majadiliano hayo yalilenga kuubadilisha Ushoroba wa Kati kutoka kuwa njia ya kawaida ya usafirishaji na kuwa eneo jumuishi la kiuchumi huku msisitizo mkubwa ukiwekwa katika maendeleo ya Reli ya Kisasa (SGR) ikiunganishwa na miundombinu ya bandari ya Dar es Salaam, sambamba na uwekezaji katika sekta za kilimo, madini na viwanda.

Alisema Serikali imepiga hatua kubwa katika ujenzi wa reli ya SGR iliyogawanywa vipande saba ambapo sehemu ya kwanza na ya pili, zinazounganisha Dar es Salaam na Dodoma imeanza kufanya kazi, huku kazi zikiendelea katika sehemu ya tatu hadi ya sita zitakazopanua mtandao wa reli kuelekea Tabora, Mwanza na hatimaye Kigoma, karibu na mpaka wa Burundi.

Aliongeza kuwa pamoja na umuhimu wa reli katika usafirishaji, ni lazima iunganishwe na mtandao wa barabara pamoja na vituo bora vya huduma za usafirishaji na ugavi na kwamba ushirikiano wa Benki ya Dunia na nchi za Tanzania, Burundi na DRC na washirika wengine wa maendeleo ni muhimu katika kufanikisha mradi huo.

Alisema lengo si kuondoa usafirishaji wa mizigo kwa malori na kutumia reli pekee, bali ni kujenga mfumo jumuishi wa usafirishaji ambapo malori yatapeleka mizigo kwenye reli, hatua itakayoongeza ufanisi, faida na uwezo wa miundombinu hiyo kuvutia uwekezaji na ufadhili.

Naye Waziri wa Fedha wa Burundi, Mhe. Dkt. Alain Ndikumana alisema mradi huo unalenga kuboresha sekta ya kilimo nchini mwake na kurahisisha biashara ya usafirishaji wa bidhaa zinazopita nchini humo kwenda maeneo mengine, hatua itakayosaidia Burundi kuwa kitovu cha shughuli za kiuchumi katika ukanda huo.

Alielezea umuhimu wa kimkakati wa kiungo cha reli, hasa kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya nikeli na kobalti eneo la Musongati, ambayo inakadiriwa kuwa kati ya tani milioni 150 na 230 zitazalishwa na kutumia ushoroba huo kuyafikia masoko ya kimataifa.

Akizungumza katika mkutano huo, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Dkt. Ndiame Diop, alisema kuwa mradi huo ni muhimu katika kukuza biashara na ustawi wa watu katika Ushooba huo na kuahidi kuwa Benki ya Dunia inaunga mkono mradi huo na iko tayari kuufanikisha.

Alisema kuwa Benki ya Dunia na washirika wa kikanda wanatarajia kufanya tathmini ya sekta binafsi ili kubaini fursa za uwekezaji na kuhakikisha kuwa miundombinu ya reli inaendana na mahitaji halisi ya shughuli za kiuchumi katika ukanda huo.

Kadiri mradi huo unavyoendelea, makubalino ya wadau yapo wazi; kuwa Ushoroba wa Kati si mradi wa reli na miundombinu pekee, bali ni mpango wa muda mrefu wenye hatua mbalimbali unaolenga kuunganisha Bahari ya Hindi na maeneo ya ndani ya Bara la Afrika, kukuza biashara, kuzalisha ajira na kuimarisha maendeleo endelevu katika ukanda huo.

Jumatatu, 12 Oktoba 2026

 Torintohot media.


Na Jerome Mlaki wa Dar. 0789106710

Maonesho ya 33 ya kimataifa ya vitabu Tanzania yamezinduliwa rasmi hii Leo na yamehudhuriwa na wananchi wengi sekta za kiserikali na zisizo za kiserikali.


Maonesho hayo yamelenga kuonyesha kazi za waandishi wa vitambu kudhamini na kutambua mchango wao ktk Taifa. 


Akizungumza katika  Maonesho  hayo mgeni rasmi Mh. Hamis Mwinjuma Naibu Waziri wa sanaa utamaduni na Michezo amesema ili Taifa liweze kuwa na maendeleo hatuna budi kuwekeza katika kuwajengea wananchi kupenda kusoma vitabu vinavyo ongeza maarifa .

Lakini pia ameeleza vitabu vinakuza uelewa,mbali na hilo ameeleza tunakilasabu ya kuheshimu nakuitambua michango ya wazee wetu katika kuielimisha jamii kupitia usomaji wa vitabu.

Mgeni rasmi Mh Naibu Waziri Hamis Mwinjuma amesema usomaji wa vitabu unaongeza maarifa  mbinu, hekima, kukuza akili na ujuzi Kwa wasomaji na hivyo tutajikuta tuna jamii yenye uelewa wa mambo mengi.


Na Kwa upande wake Hermes Damian  mwenyekiti wa wachapishaji wa vitabu Tanzania, amesema kuwa Taifa ili liendelee linahiji liwekeze katika elimu  na jamii inapaswa kukumbuka mchango wa wananchi waliojito katika Hali na mali katika kuandika hekima na ujuzi kwenye vitabu na Leo hii vitabu vyao vimetoa na vinaendelea kutoa mchango mkubwa wa kielimu hapa inchini. 

Lakini pia Hermes Damian ameshauri kujengwe maktaba itakayo hifadhi kumbukumbu za vitambu mbalimbali  vikiwemo vya wazalendo waliotoa mchanngo mkubwa Kwa Taifa katika sekta ya habari kupitia machapisho ya nalaka zao mbalimbali za vitabu hapa inchini.

Hoja ya maktaba Hermes amesema pia itatumika kama sehemu ya kuwashukuru waandishi wote wazalendo wa Taifa lao Kwa kuifadhi kazi zao vizazi na vizazi.. amesema.. usipomkumbuka mtu aliekutangulia Kwa kazi zake Bora katika Taifa.. Basi umejiandalia kaburi la kusaaulika. (Mwisho wa kunukuu)

Jumapili, 11 Oktoba 2026

 Jerome Mlaki from Dar es Salaam

The Dar es Salaam Special Zone Police Force has arrested 11 people accused of engaging in online fraud, where they have been using the names of various companies to persuade citizens to give money with various promises.

According to a statement released by the Police Force today, October 5, 2026, the suspects are alleged to have engaged in fraud through WhatsApp and Instagram networks, using the names C2203 VDC Dawn, VBCL Business Company Ltd, Fine Modern Homes and Fine Group of Companies.

Police said the suspects were claiming that the companies were run by Prof. Vincent Mwakibote, Rebecca Ndawani and Andrew Komba, while issuing advertisements with special links directing citizens to various pages.

After the victims clicked on the links, they were allegedly asked to make payments through the accounts provided to them, including paying money to buy shares in markets such as the Dar es Salaam Stock Exchange (DSE), the London Stock Exchange and the US markets, as well as promises of house construction, which the Police have described as fake contracts.

The Police Force has said that investigations are ongoing against the suspects, while urging citizens to be careful of advertisements that encourage them to make financial transactions through networks without verifying the legitimacy of the relevant business.

The police have also warned citizens not to click on links or make payments to untrustworthy people and companies, as incidents of online fraud continue to increase.

The statement was issued by the Acting Commander of the Dar es Salaam Special Police Zone. If you wish, I can also create a strong online headline for this story without distorting the information

Jumamosi, 10 Oktoba 2026




Na Jerome Mlaki wa Dar. 0789106710

Soko la kariakoo jijini Dar es salaam.. limezindua kituo Cha huduma Kwa wateja chenye lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wateja lakini ikiwemo pia kurahisisha upatikanaji wa taarifa za kibiashara ndani na nje ya soko.

Akizungumza katika hafla ya Uzinduzi huo mgeni rasmi  Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Bi. Charangwa Selemani amesema Makampuni mbalimbali pamoja na wateja na wafanyabiashara watanufaika na huduma hiyo kwani inarahisisha mawasiliano ya kiutendaji na utatuaji wa kero mbalimbali katika soko hilo.

Makampuni mbalimbali pamoja na wateja wameuongelea Uzinduzi huo na kusema ni urahisishaji wa mawasiliano ya kibiashara lakini pia ni sehemu maalumu ya kuuliza chochote ili kupata taarifa zaidi badala ya wageni wengi kuzubaa wa kuteseka namna ya kufahamu maeneo zilipo bidhaa.


Ikumbukwe kuwa soko la kariakoo liliungua kabla ya kujengwa jipya hivyo wafanyabiasha wa soko hilo walipitia changamoto mbalimbali ikiwemo sehemu ya kufanyia biashara lakini pia uduni wa upatikanaji wa bidhaa, hata wateja wao kukosa bidhaa mara nyingi walipofika katika mazingira hayo. 

Lakini Kwa sasa baada ya kukamilika soko hili la kariakoo wafanyabiashara wamemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Kwa kutatua changamoto yao ya muda mrefu. 

Na Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo, CPA Ashiraph Abdulkarim amesema Kituo Cha huduma Kwa wateja chenye lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wateja na wafanyabiashara pamoja na kupata taarifa zaidi kuhusiana na soko kimezinduliwa ili sasa kuwaweka watu wote karibu kibiashara.

Mara baada ya kuzindua kituo hicho mgeni rasmi Bi. Charangwa Selemani  amesema sasa wakati wa wafanyabiashara kurahisishiwa utatuaji wa kero zao umefika na kurahisishiwa upatikanaji wa taarifa za kibiashara ndani na nje ya nchi umefika. 


Mgeni rasmi Bi. Charangwa Selemani  amesema kituo hicho kimeyengeneza fursa zaidi na hivyo hata wateja hawatababaika Tena wapi waulize ili wapate taarifa muhimu za soko moja kwa Moja wateja hao watapiga namba 0800114040 na kueleza shida na kujibiwa.

Jumanne, 29 Septemba 2026



Na Jerome Mlaki wa Dar.

Serikali imesema kuwa,itaendelea kuwajali watu wenye ulemavu ikiwemo kutekeleza mpango wa Taifa wa watu wenye ualbino.

Akizungumza , Septemba 28, 2026, wakati akifungua Jukwaa la Kitaifa la Uratibu na Utekelezaji wa MTHUWWU jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Watu Wenye Ulemavu), Profesa Palamagamba Kabudi, amesema hatua hizo zinapaswa kuambatana na utekelezaji wa mpango huo katika maeneo yote yanayohusu haki na ustawi wa watu wenye ualbino.

Kabudi amesema Serikali na wadau wana wajibu kuhakikisha mpango huo hautabaki kwenye nyaraka, bali utekelezwe kwa vitendo, ukipewa rasilimali na kutekelezwa kwa wakati.

“Ni muhimu kuweka mipango madhubuti ya utekelezaji wa mpango na kuhakikisha kuwa mikakati na afua zilizoainishwa katika mpango zinapatiwa rasilimali na kutekelezwa kwa wakati,” amesema.

Amesema shughuli zilizopangwa zinapaswa kutekelezwa na taarifa zake kutolewa kwa wakati ili kuwezesha Serikali na wadau kufuatilia maendeleo, kubaini changamoto, kupima matokeo na kuchukua hatua za kuboresha utekelezaji.

Kabudi amesema mpango huo una nguzo nne ambazo ni ulinzi, kinga, usawa na kutobagua pamoja na uwajibikaji, huku mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ukitakiwa kufanya kazi kuanzia ngazi ya Taifa hadi Mkoa, Halmashauri, kata, kijiji na mtaa.

Akizungumza katika mkutano huo afisa ustawi wa jamii mkuu kutoka ofisi ya Waziri Mkuu Joy Maongezi amesema imetenga Sh milioni 90 kwa ajili ya ununuzi wa mafuta kinga dhidi ya saratani ya ngozi kwa watu wenye ualbino, huku ikiagiza wadau wote kuhakikisha Mpango Kazi wa Taifa wa Haki na Ustawi wa Watu wenye Ualbino (MTHUWWU) unatekelezwa kwa vitendo na kwa wakati.

 Amesema fedha hizo zimetengwa katika mwaka wa fedha 2025/26 kwa ajili ya ununuzi wa mafuta hayo kupitia Bohari ya Dawa (MSD).

Amesema tayari chupa 339 za mafuta hayo zimesambazwa katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kwa kushirikiana na wadau.

Maongezi amesema Serikali pia ina wataalamu takribani 403 wa ngozi katika halmashauri pamoja na madaktari bingwa wa ngozi 98 katika hospitali za kanda na rufaa za mikoa.

Amesema jukwaa hilo la siku tatu linapaswa kwenda zaidi ya kutathmini yaliyofanyika, bali kubaini mambo yanayotakiwa kutekelezwa, maeneo yenye upungufu na hatua mahsusi za kuziba mapengo hayo.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Watu Wenye Ulemavu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wambura Kizito, amesema sasa ni wakati wa kutoka katika hatua ya kuwa na mpango kazi na kuingia kwenye utekelezaji unaopimika, unaoratibiwa na wenye uwajibikaji.

Amesema masuala ya watu wenye ualbino ni mtambuka na hayawezi kutekelezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu au taasisi moja pekee, bali yanahitaji ushirikiano wa sekta za afya, elimu, ajira, haki na ulinzi, ustawi wa jamii, uwezeshaji wa kiuchumi, ulinzi wa mtoto na usalama.

Amesema jukwaa hilo litabaini shughuli zilizotekelezwa, zinazoendelea na ambazo hazijatekelezwa pamoja na sababu zake, taasisi zinazohusika, rasilimali zinazohitajika na changamoto zinazokwamisha utekelezaji.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Kitaifa la Uratibu na Utekelezaji wa MTHUWWU, Yohana Sali, amesema jukwaa hilo litatoa nafasi kwa Serikali na wadau kujadili mafanikio, changamoto, fursa na vipaumbele vya utekelezaji wa mpango huo.

Amesema siku ya kwanza itajikita katika kujenga uelewa wa pamoja kuhusu mpango huo, historia yake, maudhui na hali ya utekelezaji, huku siku ya tatu ikijikita katika uratibu, masuala mtambuka na maandalizi ya mpango wa utekelezaji.

Kabudi amesema Serikali pia inaendelea kuboresha mifumo ya taarifa za watu wenye ulemavu hadi ngazi ya kijiji na mtaa.

Amesema kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Tanzania Bara ina watu wenye ualbino 71,631, wakiwemo wanaume 41,203 na wanawake 30,428.

Amesema taarifa hizo zinaisaidia Serikali kufahamu idadi na maeneo wanakoishi watu wenye ualbino ili kupanga huduma kwa kuzingatia mazingira na mahitaji yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania (TAS), Godson Mollel ameipongeza Serikali kwa jitihada zake za kutokomeza mauaji na ukatili dhidi yao, huku akibainisha kuwa utekelezaji wa mpango huo mpya unatoa matumaini makubwa katika kuboresha maisha yao na fursa sawa za elimu, ajira na huduma za afya.

Hata hivyo Serikali imesisitiza kuwa itaendelea kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Huduma na Maendeleo ya Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2004 ili kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia na mahitaji ya sasa ya kijamii na kiuchumi.

Jumatatu, 28 Septemba 2026

Na Mwandishi Wetu. 

Na. Jerome Mlaki wa Dar. 

DAR ES SALAAM.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Septemba 28, 2026, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, amesema mkutano huo utakuwa jukwaa muhimu la kujadili na kuweka mikakati ya pamoja kuhusu uhamaji salama na wenye tija, unaozingatia haki za wafanyakazi, pamoja na kukuza fursa za ajira, hususan kwa vijana.

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Pili wa Afrika na nchi za Ghuba (GCC Plus),unaojulikana kama "DOHA DIALOGUE II" unaolenga kuimarisha ushirikiano katika uhamaji wa wafanyakazi, ajira na mahitaji ya soko la ajira kati ya nchi za Afrika na Mataifa ya Kiarabu.

Mkutano huo utafanyika Oktoba 5 na 6 mwaka huu na utawakutanisha wanachama wa Umoja wa Afrika (AU), nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (GCC), ambazo ni Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Qatar, Kuwait, Oman na Bahrain, pamoja na Jordan na Lebanon.


Sangu amesema mkutano huo ni mwendelezo wa Mkutano wa Kwanza uliofanyika jijini Doha, Qatar, Mei 21 na 22, 2024, ulioshirikisha nchi 43, zikiwemo 25 za Afrika, nchi za GCC pamoja na Jordan na Lebanon, zinazojulikana kwa pamoja kama GCC Plus.“Tanzania ilishiriki katika mkutano huo wa kwanza ambao ulihusisha majadiliano yaliyolenga kuimarisha ushirikiano kati ya nchi za Afrika na nchi za Kiarabu katika masuala ya uhamaji wa wafanyakazi,” amesema.

Amesema mkutano huo ulihitimishwa kwa kupitishwa kwa Azimio la Doha (Doha Declaration), lililoweka msingi wa kuendeleza majadiliano na ushirikiano kati ya pande hizo.

Sangu amesema Tanzania imepata nafasi ya kuwa nchi ya pili kuwa mwenyeji wa mkutano huo, ambao hufanyika kila baada ya miaka miwili, na kwa mara ya kwanza kufanyika katika bara la Afrika.

“Moja ya maeneo muhimu yatakayojadiliwa katika mkutano huo ni kuimarisha uhamaji wa wafanyakazi kati ya nchi, ikiwemo makubaliano ya uhamaji, ujuzi wa wafanyakazi, mahitaji ya soko la ajira na uanzishwaji wa mifumo ya kusaidia uhamaji salama na wenye tija,” amesema.

Kwa mujibu wa Sangu, mkutano huo pia utajadili namna ya kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia na mahitaji ya soko la ajira, pamoja na kuandaa nguvu kazi yenye ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira la sasa na la baadaye.

Amesema kwa Tanzania, mkutano huo utatoa fursa ya kimkakati ya kuimarisha nafasi ya nchi katika mijadala ya kimataifa kuhusu uhamaji wa wafanyakazi, kubainisha fursa za ajira ndani na nje ya nchi, kulinda haki za wafanyakazi na kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika na GCC Plus.

“Mkutano huo unatarajiwa kuongeza ushindani wa wafanyakazi wa Tanzania katika soko la ajira la kimataifa na kuchangia katika utekelezaji wa ajenda za maendeleo ya taifa,” amesema.

“Kupitia ushirikiano huo, Tanzania inatarajia kuona fursa zaidi za ajira kwa Watanzania, hususan vijana, huku ikiweka mkazo katika uhamaji wa wafanyakazi ulio salama, wenye haki, tija na unaozingatia mahitaji ya nchi na soko la ajira,” amesema Waziri Sangu.

Amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, inaamini kuwa mkutano huo utaimarisha ushirikiano na washirika wa kimataifa na kufungua fursa zaidi za ajira kwa Watanzania.

.Aidha, amesema mkutano huo unalenga kuimarisha ushirikiano kati ya nchi za Afrika na GCC Plus katika masuala mbalimbali ya uhamaji wa wafanyakazi, huku ukilenga kubadilisha makubaliano na majadiliano yaliyopo kuwa hatua za vitendo na matokeo yanayopimika.

Alhamisi, 24 Septemba 2026

 Na Jerome Mlaki wa Dar.


DAR ES SALAAM.

Imeelezwa kuwa uamuzi wa kuruhusu mabasi ya masafa marefu kufanya safari kwa saa 24 umeelezwa kuwa miongoni mwa mageuzi makubwa yaliyofanyika katika kuboresha huduma za usafiri wa barabara nchini.

Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), iliruhusu mabasi yaliyokidhi masharti kusafiri usiku na mchana.

Hatua hiyo imeongeza muda wa huduma kwa waendeshaji wa mabasi na kuwapa abiria fursa zaidi za kuchagua muda wa kusafiri.Hayo yameelezwa leo Septemba 24,2027 jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Dk. Habibu Suluo,wakati akizungumza na Wahariri na Waandishi wa habari katika Mkutano uliyoandaliwa na ofisi ya Msajiri wa Hazina,

nakubainisha kuwa uamuzi huo uliwezekana kutokana na kuimarika kwa usalama, miundombinu ya barabara, mifumo ya mawasiliano pamoja na uwezo wa LATRA kufuatilia mabasi kupitia Mfumo wa Ufuatiliaji wa Magari (VTS).

Amesema tathmini zinaonesha kuwa huduma ya safari za usiku imechangia kupunguza ajali na msongamano katika vituo vya mabasi, huku pia ikipunguza ushindani miongoni mwa baadhi ya madereva wa kuendesha kwa mwendokasi hatarishi ili kuwahi kufika wanakoelekea.Aidha,amesema abiria wengi wamekuwa wakipendelea kusafiri usiku kwa sababu huduma hiyo imepunguza au kuondoa hitaji la kugharamia malazi, hususan wafanyabiashara wanaosafiri kati ya mikoa mbalimbali.

Halikadhalika Dk. Suluo,ameongeza kuwa kuanza kwa safari za usiku kumeongeza fursa za biashara na uwekezaji katika sekta ya usafirishaji,pamoja na kuongeza ufanisi wa matumizi ya miundombinu ya barabara na kudhibiti uchovu wa madereva



Na. Jerome Mlaki wa Dar.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ameibua maswali mengi kuhusu mkataba wa jezi ya Taifa Stars, akisema kuna haja ya kupitia nyaraka za makubaliano hayo ili kupata majibu kuhusu thamani, ubora, matumizi ya nembo na haki za kibiashara zilizotolewa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Septemba 24,2026, Makonda amesema suala la jezi ya Taifa si jambo la mtu binafsi, bali ni alama ya utambulisho wa nchi, hivyo Serikali inapaswa kuhakikisha bidhaa hiyo ina ubora, inapatikana kwa wananchi na inatumika kuitangaza Tanzania.

Waziri huyo amesema katika kuupitia mkataba huo ameona una vipengele vinavyohusisha udhamini na usambazaji wa vifaa, huku akitaka majukumu ya kila upande yawekwe wazi.

Amesema mkataba unaweka ada ya udhamini ya Sh1.5 bilioni kwa miaka mitano pamoja na vifaa vya timu za Taifa vyenye thamani ya Sh300 milioni kwa mwaka, lakini amehoji namna thamani hiyo ilivyofikiwa.

“Swali nililojiuliza ni kwamba tulifikaje kwenye Sh1.5 bilioni? Haki zote za biashara zinazotolewa kwa miaka mitano zilifanyiwa valuation gani?” amehoji.

Amesema mkataba pia una kipengele cha kufanya mapitio ya utekelezaji kila mwaka, hivyo anataka mapitio hayo yafanyike ili kuangalia kama thamani na masharti yaliyowekwa bado yanaendana na mwenendo wa timu za Taifa.

Waziri amesema pia ameibua suala la VAT, akitaka kuwekwa wazi nani anabeba gharama hiyo na utaratibu gani unatakiwa kutumika iwapo thamani ya malipo inabadilika.

Amehoji pia kuhusu ‘requirement specification’ ya jezi hiyo, akitaka kujua vigezo vilivyowekwa kuhusu ubora wa jezi, nani aliyepima na nani aliyethibitisha kuwa bidhaa iliyotolewa imekidhi viwango vilivyokubaliwa.

“Specification hiyo iko wapi? Jezi inatakiwa kuwa na kigezo au kiwango gani? Nani alipima? Nani alithibitisha kwamba imekidhi specification?” amehoji Makonda

Amesema majibu ya maswali hayo yanapaswa kupatikana kwenye nyaraka za mkataba na utekelezaji wake, badala ya mjadala kuishia kwenye maoni ya watu kuhusu jezi hiyo.

Waziri amesema pia kuna haja ya kuangalia bei ya jezi ili iweze kufikiwa na mashabiki wengi, akisema kila shabiki anapaswa kupata nafasi ya kununua na kuvaa jezi ya Taifa.

Amesema jezi hiyo inapaswa kuonekana kama bidhaa ya Taifa na si bidhaa ya kawaida ya klabu.

Amesema Serikali inataka kuona jezi hiyo ikipata soko nje ya Tanzania na kuwa sehemu ya kuitangaza nchi duniani, akitoa mfano wa uwezekano wa kukutana na jezi ya Tanzania katika maduka ya Nike yaliyopo katika nchi mbalimbali.

Amesema endapo mfumo huo utawekwa vizuri, Tanzania inaweza kupata manufaa ya kibiashara huku jezi hiyo ikiendelea kuitangaza nchi katika masoko ya kimataifa.

Aidha, amesema kuna umuhimu wa kuwapa nafasi vijana wenye vipaji vya ubunifu kubuni jezi za Taifa, ili bidhaa hiyo iweze kuakisi utambulisho na ubunifu wa Watanzania na Afrika.

Amesema mjadala kuhusu jezi haupaswi kulenga kumtafuta au kumlaumu mtu, bali kuhakikisha Tanzania inapata bidhaa bora na makubaliano yenye manufaa kwa Taifa.

Waziri amesisitiza kuwa Serikali na wadau wa michezo wanapaswa kushirikiana katika kutengeneza mpango wa kuitumia jezi ya Taifa kuongeza thamani ya Taifa, huku akisema ukosoaji na ushauri vinapaswa kutumiwa kuboresha bidhaa hiyo.

Amesema mwisho wa mchakato huo ni kupata jezi yenye ubora, inayopendwa na mashabiki, inayoweza kununuliwa kwa urahisi na inayoweza kuitangaza Tanzania ndani na nje ya nchi.

Jumatatu, 14 Septemba 2026

Na Jerome Mlaki wa Dar 



Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Priscus Kiwango, amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika ujenzi wa miundombinu ya kidijitali na utoaji wa huduma za umma kwa njia ya kielektroniki kupitia Mradi wa Digital Tanzania (DTP), unaotarajiwa kukamilika rasmi Oktoba 31, 2026.

Kiwango amesema hayo leo, Septemba 14, 2026, wakati akizungumza na waandishi wa habari kando ya Mkutano wa Wadau wa Mradi wa Digital Tanzania, na kubainisha kuwa mradi huo umeleta mafanikio makubwa katika sekta ya mawasiliano ya kidijitali.

“Mradi huu umewezesha kujengwa na kuboreshwa kwa miundombinu ya mawasiliano, ikiwemo minara katika maeneo ya vijijini yaliyokuwa hayana huduma ya uhakika ya mawasiliano,” amesema Kiwango.

Aidha, amesema mradi huo ulioanza mwaka 2021 umefadhiliwa kwa mkopo wa Dola za Marekani milioni 150 kutoka Benki ya Dunia, ukiwa na lengo la kuimarisha miundombinu ya mawasiliano, kuongeza upatikanaji wa intaneti na kuboresha utoaji wa huduma za Serikali kwa kutumia teknolojia.

Amesema wananchi katika maeneo hayo sasa wanaweza kupata huduma za mawasiliano kupitia mitandao ya 3G na 4G, huku taasisi za Serikali hadi ngazi za Serikali za Mitaa zikiunganishwa katika mifumo mbalimbali ya kidijitali.

Miongoni mwa mifumo iliyowezeshwa kupitia mradi huo ni PEPMIS, unaotumika kupima utendaji wa watumishi wa umma, pamoja na Mfumo wa Daktari wa Huduma za Serikali unaomwezesha mwananchi kupata taarifa kuhusu huduma zinazotolewa, muda wa kuzipata na gharama zake.Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa Digital Tanzania, Bakari Mwamgugu, amesema mradi huo unatekelezwa katika maeneo makuu matatu ambayo ni Ekolojia ya Kidijitali inayohusisha sheria, miongozo na sera za TEHAMA; Uunganishaji wa Kidijitali; pamoja na kuwajengea uwezo watumishi.

Mratibu huyo amesema kupitia mradi huo, minara mipya 758 imejengwa, huku minara 304 ikiboreshwa kutoka teknolojia ya 2G kwenda 3G na 4G, hatua inayolenga kuongeza upatikanaji wa mawasiliano katika maeneo mbalimbali nchini.

Amesema Serikali imeongeza uwezo wa intaneti kwa Gbps 60, ambapo Gbps 40 ni kwa Tanzania Bara na Gbps 20 kwa Zanzibar, hatua inayosaidia kupunguza gharama za matumizi ya intaneti kwa taasisi za umma.

Mradi huo pia umewezesha kuanzishwa kwa vituo 32 vya huduma pamoja (One-Stop Service Centers) katika majengo ya Posta, vinavyomwezesha mwananchi kupata huduma za NIDA, RITA, Jeshi la Polisi na Land Registry katika eneo moja.

Halikadhalika, amesema watumishi wa umma wapatao 500 wamepatiwa mafunzo kuhusu teknolojia za kisasa, ikiwemo matumizi ya akili mnemba (AI), huku watumishi 50 wakipelekwa kusoma nje ya nchi katika ngazi ya uzamili, ikiwemo India, Singapore, China, Estonia, Finland na Malaysia.Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano na Miundombinu, Wizara ya Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu Zanzibar, Issa Bakari, amesema mradi huo umewezesha kuanzishwa kwa Zanzibar Digital Services Directory (ZGSD), ZanPortal na vituo viwili vya One-Stop Center vilivyojengwa Posta Kijangwani, Unguja, na Chakechake, Pemba.

Bakari amesema zaidi ya asilimia 90 ya wananchi wa Zanzibar sasa wanafikiwa na huduma za mawasiliano kuanzia 2G hadi 5G kupitia minara 63 iliyojengwa katika utekelezaji wa mradi huo.

“Kutokana na mafanikio yaliyopatikana, Serikali imeanza mazungumzo na Wizara ya Fedha pamoja na Benki ya Dunia kuhusu uwezekano wa kuingia katika awamu ya pili ya Mradi wa Digital Tanzania, itakayolenga kukamilisha na kuendeleza maeneo ambayo hayajakamilishwa katika awamu ya kwanza,” amesema Bakari.

Ijumaa, 11 Septemba 2026

 Na Mwandishi wetu.

Shahidi wa utetezi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, Brenda Rupia, amekubaliana na upande wa Serikali kwamba kuchoma vituo au karatasi za kupigia kura, kuharibu mali na hata kukata vidole vya waliopiga kura kunaweza kuzuia uchaguzi au kuwafanya wananchi wengine wasiingie katika mchakato wa kupiga kura.

Kauli hiyo ilitolewa jana Septemba 9, 2026, wakati Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga, akimhoji Brenda katika madodoso yaliyolenga kufafanua maana na athari za msimamo wa kuzuia uchaguzi uliokuwa ukihusishwa na Lissu na CHADEMA kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Katuga alimuuliza Brenda kuwa kama kuchoma vituo vya kupigia kura au kuchoma karatasi za kupigia kura kunaweza kuwa kitendo cha kuzuia uchaguzi, shahidi akajibu, “Ni sahihi.” Alipoulizwa kama kuharibu mali kunaweza kuvuruga amani na hivyo kusababisha kuzuia uchaguzi, Brenda pia alikubali. Aidha, alikubali kuwa kukata vidole vya watu waliopiga kura kunaweza kuwatisha wengine wasiende kupiga kura na hivyo kuzuia uchaguzi usifanyike.

Katika madodoso hayo, Katuga pia alimuuliza Brenda kuhusu haki ya vyama vingine kushiriki uchaguzi endapo CHADEMA inaamini katika demokrasia. Brenda alikubali kuwa vyama vingine vina haki kushiriki uchaguzi na kwamba hiyo ni haki ya kikatiba. Pia alikubali kuwa kumzuia mtu kushiriki uchaguzi si haki na kwamba kufanya hivyo ni kosa.

Hata hivyo, alipoulizwa kama anajua kwamba kumhamasisha mtu kuzuia uchaguzi ni kosa la jinai kisheria, Brenda alijibu, “Sijui kama ni kosa la jinai.” Katuga alipoendelea kumuuliza kama mtu aliyemsikiliza Lissu ana haki ya kuitafsiri hotuba yake kwa namna alivyoielewa, Brenda alikubali kuwa ni haki, akisema pia ni haki kwa mtu aliyeisikiliza na kuielewa hotuba kuifanyia kazi kwa namna anavyoona inafaa.

Katuga pia alimuuliza Brenda kuhusu kundi la wanachama 55 wa CHADEMA, maarufu G-55, ambao walikuwa wamepinga msimamo wa chama kuhusu kuzuia uchaguzi na kuuelezea kama uasi ambapo Brenda alikubali kuwa walikuwa wanachama wa CHADEMA na kwamba walipingana na msimamo huo. Alipoulizwa kama walipoona msimamo wa kuzuia uchaguzi unaashiria uasi walijitoa kwenye chama, Brenda alieleza kuwa waliendelea kubaki, lakini baadaye walijiondoa kwenye chama.

Katika hatua nyingine, Katuga alimuuliza kama baada ya G-55 kusema msimamo huo unaashiria uasi, Mwenyekiti alisema ni kweli msimamo huo unaashiria uasi. Brenda alijibu, “Ni sahihi.” Maswali hayo yaliibua moja kwa moja suala la namna msimamo wa kuzuia uchaguzi ulivyoeleweka na baadhi ya wanachama wa chama hicho wakati huo.

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *