WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Alhamisi, 2 Aprili 2026

 04:37      No comments

Torintohot 

Na Jerome mlaki 0789106710


Maadhimisho ya Siku ya Ukombozi wa Afrika yanatarajiwa kufanyika leo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kufungua mdahalo uliofanyika katika Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika, Mkurugenzi Msaidizi wa Utamaduni na Maadili ya Taifa, Dkt. Julieth Kabyemela, amesema kuwa Tanzania ni moja ya nchi yenye kumbukumbu nyingi kuhusu harakati za ukombozi barani Afrika.

“Sisi kama Watanzania, siku hii ni muhimu sana kwetu, kwa sababu nchi yetu ilikuwa kitovu cha harakati za kupigania uhuru wa mataifa mbalimbali ya Afrika,” amesema Dkt. Kabyemela.

Naye Mratibu wa Kituo hicho, Christopher Mhongole, amesema kuwa nchi nyingi za Afrika zinaweza kujifunza historia ya ukombozi kwa ushahidi wa kutosha kwa kuitembelea Tanzania, ambako harakati nyingi ziliratibiwa.

“Hivyo basi, maadhimisho kama haya ni muhimu kwa Tanzania, kwani hutoa fursa ya kuielimisha jamii, hasa vijana, ili watambue na kuthamini historia ya nchi yao,” amesema Mhongole.

Aidha, mmoja wa wanafunzi wa kidato cha sita kutoka Shule ya Sekondari Zanaki, jijini Dar es Salaam, Jesca Denis Monahera, aliyeshiriki katika mdahalo huo, amesema kuwa jambo la kwanza alilojifunza ni umuhimu wa kuwa mzalendo kwa nchi yake

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *