Kamanda wa polisi mkoani Pwani,Onesmo Lyanga akizungumza jambo na wananchi wa kitongoji cha Mpalange,kijiji cha Ikwiriri Kaskazini,kuhusiana na masuala ya ulinzi na usalama kwa raia.
Mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo,akizungumza na wananchi nje ya kituo cha afya cha Mchukwi baada ya kwenda kumtembelea mwenyekiti wa kitongoji cha Mpalange,Bakari Mpawane aliyejeruhiwa kwa kupigwa risas.
Mkuu wa mkoa wa Pwani,Mhandisi Evarist Ndikilo,ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani hapo,akimfariji mwenyekiti wa kitongoji cha Mpalange huko,Bakari Mpawane ambae amepigwa risasi na watu wasiojulikana
Mkuu wa mkoa wa Pwani,Mhandisi Evarist Ndikilo,ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani hapo,akiingia katika kituo cha afya cha Mchukwi,wilaya ya Rufiji kwenda kumtembelea na kumpa pole, mwenyekiti wa kitongoji cha Mpalange ,Bakari Mpawane ambae amepigwa risasi na watu wasiojulikana.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi,Rufiji
Mwenyeki kitongoji cha Mpalange ,kijiji Ikwiriri Kaskazini,wilayani Rufiji mkoani Pwani ,Bakari Mohammed Mpawane ,amenusurika kifo baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Tukio hilo ni tatu kutokea ndani ya mwezi mmoja uliopita likihusisha kupigwa risasi na kuuawa wenyeviti wa vitongoji na vijiji katika hali ya sintofahamu.
Kufuatia matukio hayo kukua kwa kasi,mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo,ametangaza mapambano na mtandao wa wahalifu wanaofanya matukio mbalimbali ya mauaji wa kutumia silaha na kuweka hofu kwa jamii.
Mbali na hilo ,aliweka bayana kuwa,inspector jeneral wa polisi (IGP)Enerst Mangu ametangaza dau la mil.tano ,kwa mtu yeyote atakayemtaja ama kutoa taarifa ya kundi la wahalifu wanaohusika kufanya matukio hayo .
Akizungumza mara baada ya kwenda kumtembelea mwenyekiti huyo katika kituo cha afya Mchukwi anapopatiwa matibabu,mhandisi Ndikilo,alieleza kuwa tukio hilo limetokea march 19 majira ya saa mbili usiku wakati akiwa kwenye duka lake .
Alisema walifika watu wawili dukani hapo wakiwa kwenye pikipiki ambapo mmoja alimwita jina mwenyekiti na kabla ya kutaharuki alijikuta akipigwa risasi mbili ya mkononi na tumboni na mtu mwingine aliyepakiwa nyuma ya pikipiki hiyo.
Mhandisi Ndikilo,alibainisha kwamba,bahati nzuri risasi hizo zilipalaza hivyo hazikumuathiri na kuokoka maisha yake.
“Ni tukio la tatu kwa mwezi mmoja likiwemo lililotokea machi 13 mwaka huu mwenyekiti wa kitongoji cha Kazamoyo wilayani hapa, Hemed Njiwa (45) ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa nyumbani na lile tukio lililohusisha kifo cha OC CID”alisema .
Hata hivyo mhandisi Ndikilo,alieleza wanaendelea kuwasaka watu hao usiku na mchana hadi kuhakikisha wanawakamata watu hao.
“Tutawasaka na hatafanikiwa kwa mipango yao waliojiwekea tumejidhatiti na tutahakikisha tunategua mipango yao na kurejesha amani kwa wananchi”alisema mhandisi Ndikilo.
Mhandisi Ndikilo ,alishukuru wahudumu wa afya katika kituo cha afya cha Mchukwi kwa kuokoa maisha ya mwenyekiti bkari pamoja na kutoa huduma nzuri kwa majeruhi na wagonjwa wengine wanaofikishwa hapo kupata matibabu.
Kwa upande wake,kamanda wa polisi mkoani Pwani,Onesmo Lyanga,alitaja mtandao wa watu zaidi ya 100 wanaoshukiwa kuhusiaka na matukio ya kiuhalifu kuanzia eneo la Mkuranga-Utete-Kibiti-Rufiji hadi Bungu .
Alisema majina wanayo na wanayafanyia kazi hivyo wanaomba ushirikiano wa wananchi kutoa taarifa polisi mara wanapopata wasiwasi wa watu wanaoingia kwenye maeneo yao.
Kamanda Lyanga,alisema ameletwa mkoa wa Pwani kutoka Simiyu,kikubwa anahitaji ushirikiano na jamii ili hali kupunguza matukio yanayotikisa ikiwemo la kuuwa wa wenyeviti wa vitongoji,watendaji na wenyeviti wa vijiji.
Nae majeruhi mwenyekiti wa kitongoji cha Mpalange,Bakari alisema anashukuru mungu ni mkubwa anaendelea vizuri.
Alisema wanaishi katika hali ya hofu na anajifikiria endapo akirudi kwake baada ya matibabu ataishije wakati akiwa katoka kwenye tukio kubwa na la uuaji kama hilo.
“Naomba serikali na jeshi la polisi liweke mikakati kabambe ili kuvunja ngome za kiuhalifu na mtandao unaomaliza hasa viongozi bila kujua chanzo ni masuala ya kisiasa ama nini”alisema
0 maoni:
Chapisha Maoni