Torintohot media Blog.
Akizungumza na waandishi Habari jijini Dar es salaam Mfamasia Mkuu wa Serikali Daudi Msasi amesema kuwa Mkataba huo kutawezesha kukuza ubora wa uzalishaji dawa ikiwemo Vidonge na Vifaa tiba ili kuongeza ushindani.
SERIKALI imeridhia Mkataba wa Usajili wa Dawa Dawana kusaini kwa niaba ya Bara la Afrika (AMA) ambao utawezesha Bidhaa za dawa nchini kuweza kuvuka Mipaka Barani Afrika.
"Mkataba huu utawezesha Bidhaa zetu ikiwemo vidonge na Vifaa tibaa kuweza kuvuka mipaka ya Bara la Afrika,TMDA ipo ngazi ya tatu katika bara Afrika katika udhibiti wa Dawa".Alisema Mfamasia Mkuu Daudi Msasi.
Msasi alisema Tangu Mwaka 2018 hadi sasa viwanda vilivyoweza kuanzishwa niviwanda 18 vya Dawa.
Alisema Hadi Sasa Serikali kupitia taasisi ya Bohari ya Dawa (MSD)imeidhinisha Gloves zinazozalishwa na Viwanda vya ndani.
"Tunahitaji Viwanda vya ndani vya Dawa kwaajili ya uzalishaji wa Vidonge na vifaa tiba"Aliongeza Daudi Msasi.
Naye Meneja Mkaguzi wa Dawa nchini Emanuel Alphonce amesemakuwa hadi kufikia Mwaka huu Tanzania inazalisha Dawa tiba kwa Asilimia 20 kwakutumia Viwanda vya ndani.
"Kitakwimu Bidhaa Dawa zinazo agizwa kutoka nje ya nchi ni Asilimia 99.5 zinafaa kwa matumizi nchini,kupitia Maelekezo ya serikali tumeendelea kuviwesha Viwanda vya ndani."Alisema Mkaguzi wa dawa Emanuel Alphonce.
Alisema Serikali imeweza kuweka Mazingira Mazuri kwa Viwanda Vinavyozalisha Bidhaa za dawa nchini nakufanyiwa ukaguzi
0 maoni:
Chapisha Maoni