Jerome Mlaki November 06, 2023
Na Mwandishi Wetu
IMEELEZWA kuwa sera nzuri za Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan,za kufungua uchumi inatajwa ni sababu inayowavutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam,Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jijini Dar es Salaam,Omary Kumbilamoto,wakati ufunguzi wa duka kubwa la kisasa la uzaji wa bidhaa za Hisense ikiwemo Tv,friji,majiko lilipo Posta mpya jijini hapa,
Kumbilamoto, amesema ujio wa wekezaji hao kuja kufungua maduka makubwa ni ishara nzuri ya sera awamu ya Sita.
Hata hivyo,Kumbilamoto,ametumia mkutano huo kuwapongeza kampunini ya Hisense kwa hatua ya kuja kuwekeza nchini na kubainisha uwekezaji wao utaongeza ajira.
"Tunawashukuru mlivyopanua wigo wa ajira kwa watanzania kupitia uwekezaji,na mmemsaidia Rais Samia kwenye kupunguza tatizo la Ajira"Amesa Kumbilamoto.
Huku Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Edward Jonas Mpogolo, amewapongeza Hisense kwa kuwezesha kufunguliwa duka hilo kwa kuwataka watanzania kulinda tunu ya Amani iliyopo.
"Mmeona uwekezaji huu ,unatokana na wawekezaji hawa kukubali kuja kuwekeza nchini ni kutokana na Amani iliyopo nchini."Amesema Mpogolo.
0 maoni:
Chapisha Maoni