RC wa simiyu akizungumza pamoja na watendaji wa TBA Dar es salaam leo kabla kuanza kwa ziara hiyo |
SOMA HABARI HII KISHA PICHA ZOTE ZA ZIARA TUMEKUWEKEA HAPO CHINI BAADA YA KUISOMA TAARIFA HII KARIBU
Jopo la viongozi wa mkoa wa Simiyu wakiongozwa na mkuu wa mkoa huo Bw. Antoni Mtaka hii leo wametembelea mradi wa majengo mapya ya hosteli za wanafunzi chuo kikuu cha Dar es Salaamu ili kujionea utendaji wa TBA juu ya garama za utekelezaji wa mradi pamoja na ufanisi mbalimbali unaotekelezwa na TBA ili kujionea unafuu wa garama za fedha katika utekelezaji wa miradi kiukandarasi hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa mkoa wa Simiyu amesema kuwa wamelazimika kufanya ziara ya kutembelea mradi wa ujenzi huo wa hosteli, unaotekelezwa na TBA ili kujifunza mambo mbalimbali yakiwemo unafuu wa kuwatumia wakandarasi wa hapa nchini ili kupunguza garama ambazo wakati mwingine zinakuwa juu ikilinganishwa na ualisia wa majengo husika.
Pia ameeleza kilichopelekea wao kufanya ziara ni katika kutii agizo la Mh. Rais Dk. Jonh Magufuli ambapo aliwaagiza watembelee mradi huo wa hosteli uliojengwa na TBA ambao umetumia garama ya Bilioni kumi tu (10) hadi ujenzi kukamilika, huku ikiwa ni tofauti na garama walizoomba wao mkoa wa Simiyu kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Mkoa ambapo wao waliomba garama ya shilingi bilioni arobaini na sita (46)
Naye mkurugenzi mkuu wa TBA Elius Mwakalinga amesema kuwa baada ya kupokea taarifa iliyo mhusu meneja mkoa wa Simiyu kwa TBA kuweka makadirio ya ujenzi huo wa hospitali ya mkoa wa simiyu makubwa tofauti na ilivyodhaniawa hivyo ameamuw kumwamisha meneja huyu kutoka mkoa wa Simiyu na kurudi Makao makuu ya TBA ili kupisha timu ya uchunguzi itakayoenda kupitia upya michoro ya ramani pamoja na garama katika uandaaji wa ujenzi wa hospitali hiyo na kulinganisha na garama za wali alizokuwa ameziomba meneja huyo.
Mkurugenzi wa TBA Elius Mwakalinga akizungumza mbele ya mkuu wa mkoa wa simiyu kabla ya kuanza kwa ziara hiyo katiak ofisi ya makao makuu TBA. |
Baadhi ya watendaji wa TBA na Viongozi wa Mkoa wa simiyu wakiendelea na kikao hivi leo kabla ya ziara. |
Watendaji wa TBA pamoja na viongozi kutoka mkoa simiyu wakielekea katika kukagua ujenzi wa hosteli za chuo kikuu cha Dar es salaam(UDSM)mara baada ya kuwasili eneo hilo |
Baadhi ya mafundi wakiendelea na shughuli zao katika kuelekea kukamilika kwa ujenzi huo wa hosteli |
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Antoni Mtaka wakijadiliana jambo pamoja na mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha wakala wa majengo TBA Edna Joseph mara baada ya kuwasili katika ujenzi huo |
Kutoka kushoto ni mkuu wa mkoa wa Simiyu akikabidhiwa kofia na mkurugenzi wa TBA tayari kwa kuingia ndani ya ujenzi huo wa vyumba katikati ni mkuu wa kitengo cha mawasiliano TBA |
Hapa uongozi ulikuwa tayari kwa kwenda kukagua ujenzi huo pamoja na kujifunza mambo mbalimbali katika kutekelezwa kwa mradi huo |
Mafundi wakiendelea na kazi katika kukamilisha chemba za maji machafu |
Monekano wa majengo ya hosteli ya chuo kikuu cha DAR kama yanavyoonekana ambayo yamejengwa kwa garama nafuu na kutumia muda mfupi wa miezi tu hadi kufikia hapa |
ukaguzi ukiendelea |
Rc na uongozi wakikagua vyumba vya ndani katika hosteli |
Mafundi umeme wakiendelea na kazi katika hosteli za UDSM |
RC pamoja na uongozi wakikagua ujenzi wa bwalo la chakula UDSM |
Hapa Rc wa Simiyu akifafanuliwa jambo na mkurugenzi wa TBA |
Baadhi ya Mafundi na watendaji wakiendelea na majukumu yao |
Viongozi wakikagua chumba cha hosteli ya wanafunzi UDSM |
Picha zote na Joe Clanx |
Asante kwa kuwa pamoja nasi mpendwa wetu
0 maoni:
Chapisha Maoni