Mwenyekiti wa Kitengo cha Nafaka
na Mamalishe wa Soko la Kisutu jijini Dar es Salaam,Bw. Mohamed Salum
akielezea jambo kwa mwandishi wa habari kuhusu hali ya upatikanaji wa
chakula katika Soko hilo leo jijini Dar es Salaam. Mohamed amesema kuwa
chakula kinapatikana kwa wingi kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa.
Picha ikionyesha baadhi ya nafaka zikiwa zinauzwa katika Soko la Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mkazi wa jijini Dar es Salaam akinunua nafaka katika Soko la Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Picha na: Frank Shija – MAELEZO.
……………………………………………………………
Na: Frank Shija – MAELEZO.
HALI ya upatikanaji wa chakula
nchini inaridhisha licha ya changamoto ya kuongezeka kwa bei ya bidhaa
za chakula zitokanazo na nafaka.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti
wa Kitengo cha Nafaka na Mamalishe wa Soko la Kisutu jijini Dar es
Salaam, Bwana Mohamed Salum katika mahojiano maalum na mwandishi wa
habari hii leo jijini Dar es Salaam.
Mohamed amesema kuwa pamoja na
kuwa Dar es Salaam inategemea chakula kutoka mikoani bado hali ya
upatikanaji wake ni mkubwa na wa kuridhisha kama ambavyo imekuwa miaka
ya nyuma.
“Chakula bado kinapatika kwa
wingi japo changamoto iliyopo ni ongezeko la bei pekee kitu ambacho si
kigeni duniani kote,” alisema Salum.
Alisema nia ajabu sana kusikia watu wanasema kuna baa la njaa wakati vyakula vinapatikana kwa wingi katika masoko yetu.
Aliongeza kuwa kungekuwa na
tatizo la uhaba wa chakula basi hata uingizwaji wa chakula katika jiji
la Dar es Salaam ungepungua kwani asilimia kubwa inategemea chakula
kutoka mikoani, badala yake upatikanaji wa chakula umeendelea kuwa wa
kuridhisha.
“Ndugu mwandishi ukitaka kujua
kuwa hakuna uhaba wa chakula jaribu kutembelea maeneo ya Manzese Uzuri
utajionea namna maroli matani kwa matani yanayoingiza nafaka kwenye
mashine za kusaga na kukoboa.” Alisisitiza.
0 maoni:
Chapisha Maoni