Jumatatu, 6 Novemba 2017
Mkutano wa wadau wa Kutengeneza Sera ya Pombe, tarehe
31/10/2017, Katika Ukumbi wa NIMR-DSM.
By
Jasson Joel Kyaruzi
Afisa Masajili wa Vyakula Mkuu, TFDA
www.tfda.or.tz
UTANGULIZI
SEHEMU YA KWANZA
• Mamlaka ya Chakula na Dawa ni nini?
-Majukumu yake ni yapi kususan kwenye sekta ya vinywaji
vitumikavyo kama chakula?
-Mipaka yake ni ipi kisheria katika suala la udhibiti wa
usalama wa chakula kwa ajili ya kulinda afya ya mlaji?
•Chakula Salama ni nini?
•Vihatarishi kwa afya ya mlaji visababishwavyo na chakula ni
vipi?
•Mpangilio/Muundo wa udhibiti wake Ukoje?
•Mbinu za Udhibiti kwa Kila Sehemu ni zipi?
•Udhibiti wa Usalama na Ubora wa chakula Unaofanywa na
Serikali Uangazia Maeneo gani?
www.tfda.or.tz
UTANGULIZI cont...
SEHEMU YA PILI
• Katika Lugha ya Udhibiti, Pombe (Alcoholic Beverage) ni nini?
•Makundi mbalimbali ya pombe ni yapi?
•Udhibiti wa Usalama na ubora wa pombe ukoje?
•Mbinu za Udhibiti kwa Kila Sehemu ni zipi?
•Udhibiti wa Usalama na Ubora Unaofanywa na Serikali
Uangazia Maeneo gani?
www.tfda.or.tz
UTANGULIZI cont...
SEHEMU YA TATU
• Changamoto za udhibiti wa Pombe kwa lengo la kulinda Afya ya
mlaji ni zipi?
•Nini kifanyike kukabiliana na changamoto hizo.
• Hitimisho
www.tfda.or.tz
SEHEMU YA KWANZA
www.tfda.or.tz
MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA NI
NINI?
Maana
Mamlaka ya chakula na Dawa ni taasisi ya umma iliyoundwa
chini ya Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi Sura ya 219.
Mamlaka hii ipo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto.
Majukumu
Kulinda na Kuendeleza Afya ya jamii kwa kuhakikisha kuwa
bidhaa za chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba
vinavozalishwa au/na kuingizwa nchini vina usalama,ubora
na ufanisi kwa mujibu wa matakwa ya kisheria yaliyopo.
Mipaka yake kisheria
Katika sekta ya chakula, TFDA inadhibiti usalama wa
vyakula mara baada ya kuvunwa kutoka mashambani hadi
kwenye hatua ya kuuzwa kwa walaji. Sheria haijaipa nguvu
TFDA kudhibiti moja kwa moja tabia ya ulaji wa vyakula
(Food Consumption Behaviour) na Vyakula vikiwa shambani.
www.tfda.or.tz
CHAKULA SALAMA NI NINI?
Chakula salama maana yake ni pale panapokuwa hakuna
hatari kwa chakula husika inayotokana na :-
i) vimelea vinavyosababisha magonjwa kwa mlaji
ii) Sumu za asili zinazoweza kuwa kwenye chakula
chenyewe
iii) Vitu/kemikali zinazodhuru afya kwa muda mfupi au
baada ya muda mrefu ambazo zinaweza kuwa
zimewekwa kwenye chakula wakati mwingine kwa nia
njema ya kukidhi lengo fulani au zimeingia kwenye
chakula kama uchafu kutoka nje ya mazingira ya
chakula husika.
www.tfda.or.tz
VIHATARISHI KWA AFYA YA MLAJI VISABABISHWAVYO NA
CHAKULA VIPI?
Vihatarishi ni:-
i) Chakula kisichosalama
ii) Tabia za ulaji zisizozingatia usalama wa afya ya mwili
(unacceptable consumption behaviour with respect to
human health).
www.tfda.or.tz
Mpangilio wa udhibiti huzingatia mtiririko wa
wa kibiashara wa chakula maarufu kama“FARM
TO TABLE FOOD SUPPLY CHAIN” ambao
huundwa na maeneo makuu yafuatayo:-
SHAMABANI (FARM)
USINDIKAJI (PRODUCT MANUFACTURE)
UHUZAJI (SALES)
UTAYARISHAJI (PREPARATION)
MEZANI KWA AJILI YA KULA (TABLE)
MPANGILIO WA UDHIBITI
www.tfda.or.tz
Chakula salama kinapatikana pale ambapo udhibiti
huanzia “shambani”, na kuendelea hadi “mezani” kwa lugha
ya kitaalam huitwa “Farm to Table Food Chain”.
Kwenye mnyororo huu kuna wadau au wahusika wengi,
ambao wanatakiwa kila mmoja atakeleze/atimize wajibu
wake ndipo uhakika wa kupata chakula salama unakuwepo.
Aidha kila mdau anatakiwa amchunge na kumuhimiza
mwenzake na ikibidi kumwelimisha kutimiza wajibu wake ili
chakula salama kiweze kupatikana.
MPANGILIO/MNYORORO WA
UDHIBITI UKOJE ?
www.tfda.or.tz
SHAMABANI (FARM): GAP, GTP & GSP
USINDIKAJI (PRODUCT MANUFACTURE):
GMP(GHP/HACCP)
SALES (UHUZAJI): GHP
UTAYARISHAJI (PREPARATION): GHP, GPP
MEZANI KWA AJILI YA KULA (TABLE):
GHP & Consumption Behaviour
MBINU ZA UDHIBITI KWA KILA
SEHEMU YA “FARM TO TABLE
FOOD CHAIN” NI ZIPI?
www.tfda.or.tz
UDHIBITI WA USALAMA ...NA
SERIKALI UANGAZIA MAENEO
GANI?
Usalama wa chakula kwa ujumla huusisha maeneo
yafutayo:-
i) Mifumo/mazingira ambapo chakula huzalishwa kuanzia
mashambani hadi kwenye utayarishaji kwa ajili ya kula
ii) Malighafi/Viambato ambavyo uchanganywa kwa lengo
la kupata bidhaa inayokusudiwa kwa ajili
ya matumizi ya walaji.
iii) Mifumo ya kufanya ufuatiliaji na uondoaji sokoni wa
chakula husika ikiwa kuna tatizo
limetokea
www.tfda.or.tz
UDHIBITI ...NA SERIKALI
UANGAZIA MAENEO GANI? Cont..
Usalama wa chakula kwa ujumla huusisha maeneo:-
iv) Vifungashio na vitu vinavyogusana na chakula
(Food Packaging Materia and Contact Surfaces)
(v) Masuala ya taarifa zinazokihusu chakula husika
(lebo na matangazo ya biashara)
(vi) Tabia za ulaji chakula (Consumption behaviour)
www.tfda.or.tz
SEHEMU YA PILI
www.tfda.or.tz
Pombe (Alcoholic Beverage) ni nini?
•Pombe (Alcoholic Beverage) ni kinywaji kilichowekwa
kwenye kundi la vyakula vyenye kiwango cha kilevi zaidi
ya 1.5%
•Makundi ya pombe :
i) Portable Spirits and Liquors (e.g. Brandy, whisky, vodka, gin,
rum, Tequilla, Cachaca and liquors),
ii) Wines and Rosella alcoholic drink (e.g. Fruit wines, table
wine, Sparkling and semi-sparkling wines, Fortified wine
and Aromatized wine. Liquor wine, Rosella alcoholic drink)
www.tfda.or.tz
Pombe (Alcoholic Beverage) Cont..
Makundi ya pombe :
iii) Cider and perry, Mead Alcoholic drinks (e.g. Apples, pears
and honey based alcoholic beverages)
iv) Cereal based alcoholic beverages (e.g. Beers, Kibuku and other
traditional brews)
(v) Non cereal based alcoholic beverages (e.g. Ready to drink
unfermented fruit flavour based alcoholic beverage)
www.tfda.or.tz
Pombe (Alcoholic Beverage) Cont..
•Udhibiti wa Usalama na ubora wa pombe
Ni sawa na vyakula vingine kama tulivyoona hapo
awali, hii ujumuisha vigezo vya usalama na ubora
vilivyotayarishwa kitaalam, pamoja na masharti ya
utoaji wa taarifa kwa mlajai kupitia lebo kwa vinywaji
vilivyofungashwa.
www.tfda.or.tz
Pombe (Alcoholic Beverage) Cont..
•Mbinu za Udhibiti kwa Kila Sehemu
Ni zile sawa na vyakula vingine. Mathalan sehemu za
Utengenezaji, utayarishaji na mezani: Upande mmoja
mtengenezaji hutakiwa kuonesha kwenye lebo maelezo
ya kumwesha mlaji kutumia kwa usahihi bidhaa husika
akizingatia usalama wa Afya yake. Upande mwingine
mlaji wakati wa utayarishaji na ulaji anatakiwa
azingatie maelezo yaliyopo kwenye lebo ya bidhaa
husika.
www.tfda.or.tz
Pombe (Alcoholic Beverage) Cont..
Udhibiti wa usalama na ubora unaofanywa na
Serikali :Huangazia maeneo yale yale ambayo
nimeyataja hapo juu. Mathalan kwenye suala la
udhibiti tabia za ulaji (consumption behaviour)
serikali imekuwa ikitengeneza kanuni (by-law)
na taratibu mbalimbali ikiwa ni pamoja na
viwango kwa lengo la kudhibiti tabia za ulaji
wenye mashaka katika suala la kulinda na
kuendeleza afya ya jamii. Mfano suala la hivi
karibuni la pombe ya viroba. Aidha Elimu
imekuwa ikitolewa kwa walaji kudhibiti tabia.
www.tfda.or.tz
SEHEMU YA TATU
www.tfda.or.tz
CHANGAMOTO
Changamoto za udhibiti wa Pombe kwa lengo la kulinda Afya ya
jamii ni pamoja na:
a) Ukosefu wa elimu ya kutosha miongoni mwa wadau hasa
baadhi ya wazalishaji juu ya umuhimu wa kutengeneza pombe
salama na bora.
b) Tabia ya unywaji pombe hisiyozingatia matakwa ya usalama
na ubora wa afya ya mlaji iliyojikita katika jamii kutokana
sababu mbalimbali kama vile tamaduni na mila zilizopo katika
jamii, ukosefu wa elimu sahihi juu ya madhara ya kiafya
kutokana na unywaji pombe kupita kiasi n.k.
c) Mabadiliko ya kiteknolojia, kiuchumi na kijamii kwenda kwa
kasi katika kiwango cha kuzifanya sheria na kanuni zilizotungwa
hapo awali kuonekana kupitwa na wakati kiufanisi kwa
matarajio yaliyokusudiwa hapo awali.
www.tfda.or.tz
CHANGAMOTO cont..
Changamoto za udhibiti wa Pombe kwa lengo la kulinda Afya ya
jamii ni pamoja na:
d) Kutokuwepo na ushirikiano rasmi wa kutosha miongoni
mwa wadau wakuu yaani Walaji, Serikali/Dola na Industry.
www.tfda.or.tz
CHANGAMOTO cont..
• Nini kifanyike kukabiliana na changamoto hizo?
Mambo yafuatayo yanapendekezwa:
i) Elimu kwa wadau husika
ii) Sheria, kanuni, viwango na miongozo iliyopo kupitiwa upya
ili kubaini kama bado ina nguvu ya kudhibiti katika namna
ya kupata matokeo yaliyokusudiwa katika suala zima la
udhibiti wa usalama wa bidhaa husika na utumiaji husioleta
madhara katika jamii.
iii) Kuwa na mechanism rasmi ya kuwaumganisha wadau
wakuu ili waweze kushirikiana katika udhibiti wa usalama
wa bidhaa husika na utumiaji wake. Sera ya taifa ya pombe
inaweza kuwa ni mojawapo ya mechanisms nzuri za
kufanikisha lengo hilo.
www.tfda.or.tz
Mwisho
• Ahsanteni sana kwa kunisikiliza
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 maoni:
Chapisha Maoni