TAARIFA KUHUSIANA NA SEMINA ENDELEVU YA YA 28, ITAKAYOFANYIKA
TAREHE 12-13 OCTOBER,2017 KATIKA UKUMBI WA MLIMANI CITY– DAR ES SALAAM.
Na Torinto Hot Blog.
1.0 UTANGULIZI:
Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo
na Wakadiriaji Majenzi ni taasisi ya Serikali chini ya Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano inayosimamia utekelezaji wa sheria namba 4 ya mwaka
2010.
Jukumu kuu la Bodi ni kusajili na
kuratibu mienendo ya kitaalam ya Wabunifu Majengo, Wakadiriaji Majenzi,
Wataalam wanaohusiana nao pamoja na kampuni zao.
Pamoja na majukumu mengine
yaliyoainishwa katika kifungu cha 5 cha sheria hiyo, Bodi ina wajibu wa
kuratibu na kutoa nafasi za mafunzo endelevu kwa wadau wa sekta ya ujenzi
kupitia semina na warsha mbalimbali.
Semina hizi zilianzishwa mwaka 2003
na hufanyika mara mbili kwa mwaka. Jumla ya wadau 5,789 wa sekta ya ujenzi
wamenufaika na semina hizi.
Albert Munuo
KAIMU MSAJILI BODI YA USAJILI WA WABUNIFU MAJENGONA WAKADIRIAJI MAJENZI |
Semina ya 28 itakuwa ni ya siku mbili, tarehe 12 na 13 October,2017, kuanzia saa 1.30 asubuhi,na Mgeni Rasmi atakuwa Mheshimiwa Professa Makame Mbarawa(MB), Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano;
2.0 MALENGO MAKUBWA YA SEMINA HII:
·
Kuwanoa Wabunifu Majengo(Architects), Wasanifu wa Ndani ya
Majengo( Interior Designers), Wabunifu wa Mandhari ya Nje(Landscape Architects),
Wakadiriaji Majenzi(Quantity Surveyors), Wasimamizi Ujenzi( Construction
Managers), Watathmini Majengo(Building Surveyors) na wadau wengine katika sekta
ya ujenzi kukabiliana na
mabadiliko ya sayansi na teknolojia katika sekta ya ujenzi.
·
Kubadilishana uzoefu wa kazi
za kitaalam kwa lengo la kuziboresha.
·
Kuwapa fursa wataalam katika
sekta ya ujenzi kupata nasaha kutoka kwa viongozi wa serikali.
3.0 Mada Kuu ni Mbinu za Kupunguza Madhara
ya Matetemeko ya Ardhi, Ukaguzi wa Miradi ya Ujenzi na Matengenezo ya Majengo
na Miundombinu Katika Sekta ya Ujenzi (Mitigation
of Earthquakes, Technical Audits and Maintenance in The Construction Industry)
Mada zifuatazo zitatolewa:
1.
Consideration
of Earthquakes Forces in Structure Design in Tanzania
2.
Technical
Audits in the Construction Industry.
3.
Maintenance
of Construction Projects.
4.
Project
Cost Accounting in Professional Practice in the Construction Industry.
Mada hizi zimechaguliwa kuwapa fursa wadau
katika sekta ya ujenzi, kukumbushana umuhimu wa mambo yafuatayo:
(i)
Kukuza uelewa wa kitaalam
kuhusu namna ya kuzingatia tatizo la matetemeko ya ardhi katika Ubunifu,
Ukadiriaji na Ujenzi wa majengo na miundo mbinu, ili kupunguza athari
zinazoweza kuletwa na matetemeko kwenye miradi ya ujenzi, wakati wa ujenzi na
wakati wa matumizi ya jengo. Mada hii imebuniwa kufuatia matetemeko yaliyotokea
sehemu mbali mbali duniani, ikiwepo Kagera na kusababisha maafa makubwa kwa
jamii.
(ii)
Kukuza uelewa wa namna ya
kufanya ukaguzi wa miradi ya ujenzi katika hatua mbali mbali.
(iii) Umuhimu
wa kuzingatia ukarabati katika miradi ya ujenzi, ili kuongeza thamani ya miradi
na kupunguza gharama za matengenezo, pale inapoachwa kwa muda mrefu bila
matengenezo. Tukumbuke kauli ya wahenga isemayo ‘usipoziba ufa utajenga ukuta’;
na hili limetokea kwa mradi mingi ya ujenzi.
(iv) Kuelimisha
wadau kuelewa namna ya kupanga gharama za uendeshaji wa miradi, ili kuepusha gharama
na hasara zisizo za lazima wakati wa ujenzi wa miradi.
4.0 HITIMISHO:
Bodi
inachukua fursa hii kuwasihi Wabunifu Majengo, ‘Interior Designers’ ‘Landsacpe
Architects’ , Wakadiriaji Majenzi, ‘Building Surveyors’ ‘Construction Managers’
‘Project Managers’ Wahandisi, Wakandarasi na wadau wengine katika sekta ya
ujenzi kushiriki kwa wingi katika semina hii muhimu, ili kuwaongezea ujuzi na
maarifa ya kuboresha utendaji wao wa kazi.
Bodi
inapenda kuwaomba waajiri wote nchini kufadhili kwa kuwalipia wataalam wao ada
ya shs 300,000, ili waweze kuhudhuria semina hii, ambayo itawawezesha wataalam
wao kuongeza tija katika utendaji wao wa kazi.
Aidha
napenda kuwakaribisha wanahabari katika semina; ili kuwezesha wananchi kupata
habari zaidi juu ya semina hii.
0 maoni:
Chapisha Maoni