WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Ijumaa, 6 Aprili 2018

 01:44      No comments


Na Jerome Mnaki 


Halmashauri ya Wilaya ya Butiama Mkoani Mara imesema imepata ufumbuzi wa changamoto ya wanafunzi  wa  darasa  la kwanza na awali Shule ya Msingi Mwibagi wilayani waliokosa mahali pa kusomea kwa kuwagawa wanafunzi hao  kwa awamu mbili.

Hayo yamebainishwa leo (Alhamisi 04, Februari 2016), Afisa Elimu wa Wilaya hiyo, Hans Mgaya, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii, ambapo alikiri kuwepo kwa changamoto ya uhaba wa madarasa shuleni kutokana na ongezeko la wanafanuzi walioandikishwa kuanza darasa la kwanza mwaka huu, ambapo hata hivyo tayari wameshachukua hatua mbalimbali za kukabiliana na tatizo hilo.


Aidha, Mgaya amesema kuwa  jitihada za muda mfupi walizozifanya ni kuwagawa wanafunzi hao katika mikondo  miwili ili waweze kubadilishana madarasa , mkondo mmoja utaingia asubuhi na mkondo mwingine mchana. 

Kwa mujibu wa Mgaya alisema jitihada za muda mrefu ni kujenga shule nyingine mpya ili kusaidia kuchukua wanafunzi wengi kwa wakati mmoja, ujenzi wa shule hiyo ulishaanza kabla ya  tamko la elimu bure na tupo katika hatua  ya awali ya ujenzi wa msingi wa madarasa hayo alisema Mgaya.

“wanafunzi walioandikishwa kujiunga na shule ya msingi kwa mwaka huu 2016 imeongezeka kwa kiasi kikubwa hivyo kusababisha idadi ya wanafunzi kuwa kubwa” alisema Mgaya.

Idadi ya wanafunzi wa darasa la awali na la kwanza walioandikishwa kwa mwaka 2016 katika shule ya msingi Butiama kuanza masomo, ambapo hata hivyo zaidi ya wanafunzi 240 wa shule hiyo wanasomea katika chumba kimoja.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *