WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Ijumaa, 6 Aprili 2018

 02:27      No comments




Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) Roberto Jarrin akizungumzia nafasi ya TBLkatika kuwaendeleza wakulima nchini kiteknolojiaZaidi.


Na. Jerome Mnaki
KAMPUNI ya Bia nchini(TBL) ambayo ni moja kati
ya wanafamilia AB InBev imeandaa shindano
linalowahusisha matumizi ya ubunifu na teknolojia
kwa wakulima.

Shindano hilo lililozinduliwa jana, litafikia tamati
Mei 10 mwaka huu, tukio litakalofanyikia ukumbi
wa Mlimani City ambapo washindi watatu
watapatikana.


Akizungumza kwenye uzinduzi wa shindano hilo,

linalofanyika kwa ushirikiano na Mradi wa masuala
ya Teknolojia na Ubunifu Bits & Bytes,
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Roberto Jarrin,
alisema lengo ni kuwatambua na kuwaendeleza
wakulima wanaolima kibunifu.

Amesema, kilimo cha kibunifu kinawanufaisha
wakulima kwa kuwa wanapata faida ile ile
iliyokusudiwa kwa kuwa kinaokoa mazao na mbegu
kupotea wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna.


“Tanzania Breweries tumeona nafasi ambayo
kilimo inayo katika kuendeleza uchumi wa nchi na
hilo linaweza kufanikiwa kwa kutumia teknolojia na
ubunifu katika kilimo, hivyo shindano hili linalenga
kuwafikia wakulima wengi zaidi”alisema Roberto
Jarrin.

Kwa upande wake Mwanzilishi mwenza wa Bits and
Bytes Zuweina Farah, alisema katika kuhakikisha
kilimo chenye kuhusisha ubunifu na teknolojia
unafanikiwa mnamo April 9 watakua SUGECO, na
tarehe 10 na 12 watashiriki kwenye kongamano la
kilimo biashara mkoani Morogoro.

Ameongeza kuwa Arusha mnamo April 12 na 13 katika
Chuo cha ufundi Arusha kutakuwa na mjadala

kuhusiana na kilimo ikiwa pamoja na kutembelea
miradi tofauti ya Twende. Huku April 14 hadi 15
itashirikiana na AIESEC kwa Dar na mipango
mingine kufanyiwa kazi kufikisha ujumbe kwa
wabia tofauti kwenye eneo hili.
Mwanzilishi mwenza wa mradi wa Bits and Bytes
unaojihusisha na matumizi ya teknolojia na
ubunifu, Lilian Madeje, akizungumzia nafasi ya
Teknolojia katika kuendeleza kilimo nchini, mradi
huo ndio unaoratibu shindano la kuwapata
wakulima wanaotumia teknolojia na ubunifu katika
kuendeleza kilimo.



Waandishi wa Habari Wakifuatilia Matukio Hayo kwa umakini

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *