WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Ijumaa, 6 Aprili 2018

 01:41      No comments

Na Torinto Maiko Dar.


 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalaam, akizungumza na wanafunzi walimu, pamoja na wazazi wa Kigogo katika Uzinduzi wa Kuezeka Paa Ofisi za Walimu shule ya msingi Mpinduzi jijini Dar es Salaam.






 wanafunzi  Shule ya hazina wakitoa burudani ya sarakasi

MwambawahabariMkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amewaasa watu wanaopenda kuvamia maeneo ya Serikali yakiwemo maeneo ya shule kuacha na kuondoka mara moja kwani hatua Kali za kisheria  dhidi yao.

Rc Makonda amesema hayo Leo alipokuwa akizindua uezekaji Paa wa Ofisi za Walimu katika shule ya Msingi Mapinduzi iliyopo katika manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, na kusema  kuwa kutokana na shule kutokuwa na uzio watu  wamekuwa wakijiamulia kujenga au kufanya makazi katika maeneo ya shule kitendo ambacho si sahihi.

"Wale wanaojipangia kuhamia au kuvamia maeneo yaaliyo wazi ya Serikali yakiwemo maeneo ya shule, hospitali na mengineyo  na kufanya makazi  kuacha mara moja tabia hiyo kwani kwa kufanya hivyo hatua Kali za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kufikishwa mahakamani".Amesema Makonda

 Amesema watu wakiamia na kujenga maeneo ya shule watoto wao watasomea wapi hivyo tujiulize  kuvamia maeneo ya shule na kujenga ni kosa na wanaofanya hivi wachukuliwe hatua na kufikishwa mahakamani kwa yeyote atakaye uza au kununua maeneo hayo.

Aidha amesema wanaboresha mazingira ya kazi kwa walimu ikiwa ni kuendelea kusupoti kauli ya Mhe. Rais  MAGUFULI ya Mpango wa Elimu bure bila malipo, wameamua kuboresha mazingira ya kazi kwa Walimu katika Mkoa huo kwa kujenga ofisi zipatazo 402,ambapo Leo Amezindu uzekwaji Paa katika ofisi hizo katika shule hiyo manispaa ya Kinondoni na kuwahamasisha wadau kuendelea kujitokeza kuchangia na kushiriki kukamilisha zoezi hilo.

"Lazima mpishi aweanapika vizuri ili walaji waweze kula ivyo tunaboresha mazingira ya walimu wetu ili waweze kufanya kazi kwa ueledi na ufanisi mkubwa ili watoto wetu waweze kufaulu vyema na kusonga mbele na kutengeneza kizazi chenye wasomi wengi na taifa liweze kusonga mbele"Amesema Rc Makonda.

Kwa  upande Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe.Benjamani  Sitta amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuangalia suala la Ofisi pamoja na nyumba za  Walimu kwa Mkoa huo kwani ilikuwa ni changamoto kubwa sana kwa walimu walikuwa hawana ofisi kitendo kinachopelekea walimu kukaa chini ya miti na kufanya kazi zao.

Naye Mwalimu mkuu wa shule hiyo amemshukuru Mkuu wa mkoa kwa jitihada zake anazozifanya katka mkoa huo, kwa kuwaangalia walimu na kuweza kuwatengenezea mazingira mazuri ya kuwawezesha kufanya kazi zao katika sehemu nzuri, kwani katika shule hiyo kulikuwa na ofisi moja tuu ya walimu, kitendo kilichopelekea walimu wengine kukaa chini ya miti.

Pia katika uzinduzi huo Mhe. Paul Makonda amepoka fedha kiasi cha shilingi  Milioni 50, kwa ajili ya kusapoti ujenzi wa ofisi pamoja na nyumba za walimu katika mkoa huo.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *