Na Zainabu Ally
Serikali ya Kenya imeanza mpango wa kutenga mkondo mmoja wa barabara kuu ya Thika wa kutumiwa na mabasi ya kubeba abiria jijini Nairobi.
Waziri wa uchukuzi nchini humo, James Macharia amesema kuwa mpango huo ambao utaanza kutekelezwa mara moja unalenga kupunguza msongamano wa magari jijini Nairobi.
Akizungumza katika mkutano wa kamati ya Bunge la Seneti kuhusu barabara nchini humo, amesema kuwa mpango huo umeanza kutekelezwa.
Aidha, Barabara ya Thika ni miongoni mwa barabara sita kuu za kuingia na kutoka jijini Nairobi ambazo zimewekewa mpango na serikali wa kupunguza msongamano wa magari jijini humo.
“Tunahitaji zaidi ya mabasi 900 katika njia hizi sita kuu za kuingia na kutoka jijini lakini kwa sababu hatuna mabasi hayo, tumefungua njia moja, barabara kuu ya Thika,”amesema Macharia
0 maoni:
Chapisha Maoni