Tarehe 26/10/2016 nyenzo ya mawasiliano inayotumiwa na Mradi wa Lishe wa Mwanzao Bora ili
kuboresha lishe ya akina mama na watoto itaasiliwa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
ili kuwa kama nyenzo ya kitaifa. Nyenzo hii inayoitwa "Mkoba wa siku 1000" itazinduliwa katika
ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kama sehemu ya mkutano shirikishi wa tathmini ya
lishe wa mwaka 2016. Mwanzo Bora ni mradi wa lishe wa miaka saba unaofadhiliwa na Watu wa
Marekani kupitia Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID). Mradi wa lishe wa Mwanzo Bora una
lengo la kupunguza kwa asilimia 20 udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka miwili na pia
upungufu wa damu kwa akinamama wajawazito na wanaonyonyesha katika mikoa sita ya Tanzania Bara
na katika wilaya tatu ya Zanzibar.
Inakadiriwa kuwa watoto milioni 2.7 hapa nchini Tanzania walio chini ya umri wa miaka mitano
wamedumaa. Juhudi zinazofanywa na serikali pamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya lishe
zinasaidia sana katika kupunguza tatizo la udumavu; kwani tatizo hili limepungua kwa kiasi kikubwa
kutoka asilimia 42 (mwaka 2010) mpaka kufikia asilimia 35 (mwaka 2015).
Kupungua kwa tatizo la udumavu hapa nchini kumechangiwa pia na matumizi ya Mkoba wa Siku 1000
uliotengenezwa na mradi wa lishe wa Mwanzo Bora kwa kushirikiana na Taasisi ya Chakula na Lishe
Tanzania. Mradi wa lishe wa Mwanzo Bora umechangia pia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la
udumavu katika mikoa ya Dodoma (kutoka asilimia 56 mpaka asilimia 36.5), Morogoro (kutoka asilimia
44 mpaka asilimia 33.4) na Manyara (kutoka asilimia 56 mpaka asilimia 36.5).Mafanikio haya
yametokana na matumizi ya Mkoba wa Siku 1000 ambao unahamasisha mabadiliko ya tabia za lishe.
Mkoba wa Siku 1000 utaasiliwa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kama mkoba
maalumu wa kitaifa utakaotumika kutekeleza afua mbalimbali za lishe hapa nchini. Mradi wa lishe wa
Mwanzo Bora utakabidhi mikoba 200 kwa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania.ambapo mwakilishi
kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe atakabidhi mikoba hiyo kwa Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi
kama mwakilishi wa serikali. Tendo hili litamaanisha kwamba Mkoba wa Siku 1000 umezinduliwa rasmi
kuwa mkoba wa Kitaifa.
Baada ya uzinduzi huu, Mkoba wa Siku 1000 na wadau mbalimbali wa lishe hapa nchini kama vile
maafisa lishe wa mikoa na wilaya pamoja na taasisi na mashirika mbalimbali ili kuhamasisha tabia
chanya za lishe na hivyo kupunguza tatizo la udumavu kwa watoto na upungufu wa damu kwa
akinamama wajawazito na wanaonyonyesha katika jamii zetu.Mkazo unawekwa katika kuhamasisha tabia
na mitazamo ya kijinsia itakayosaidia kuboresha hali za lishe na afya za akinamama na watoto.
Uzinduzi wa Mkoba wa Siku 1000 umeandaliwa na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania.Washiriki
katika uzinduzi huu wanajumuisha wadau kutoka katika mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na wadau
wengine wa masuala ya lishe
0 maoni:
Chapisha Maoni