WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumatano, 1 Februari 2017

 03:43      No comments

This content isn't available over encrypted connections yet.



Picha ya pamoja ya wakuu wa nchi za umoja wa Afrika katika mkutano wao wa 28 jijini Addis Ababa, Ethiopia. Rais Dkt John Pombe Magufuli ni wa pili mstari wa pili kulia.

MGODI WA BUZWAGI WAZINDUA KAMPENI YA WAKIA MOJA MTI MMOJA,MITI MILIONI 1.6 KUPANDWA KAHAMA

 Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi leo umezindua kampeni ya upandaji miti katika Wilaya ya Kahama ikiwa na lengo la kupanda mti kwa kila wakia ya dhahabu ambayo imechimbwa kwenye mgodi wa Buzwagi, ambapo miti zaidi ya milioni moja na laki sita inatarajiwa kupandwa katika kipindi cha miaka miwili.

Akizindua kampeni hiyo Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa hatua hiyo na kusema ni ya kizalendo kwa kuwa itasaidia katika kuboresha hali ya mazingira ya wilaya ya Kahama.

“Jukumu la upandaji miti na kuhakikisha mazingira yetu yanatunzwa ni letu sote, Wenzetu wa Buzwagi wameanza kuonyesha jitihada kwa kupanda miti milioni moja na laki sita, hivyo sote kama Jamii hatuna budi kuwaunga mkono kwa kuhakikisha kila mmoja wetu katika eneo lake anapanda miti na kuifanya wilaya yetu ya Kahama izidi kupendeza”Alisema Nkurlu.

Akizungumzia Malengo ya Kampeni hiyo Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo amesema kama wadau muhimu wa mazingira wanalojukumu la moja kwa moja kuhakikisha shughuli za utunzaji wa mazingira zinakuwa ni sehemu ya maisha ya kila siku.



Mkuu wa wilaya Kahama Fadhili Nkurlu akipanda mti kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya upandaji miti milioni moja na laki sita itakayopandwa katika maeneneo mbalimbali wilayani kahama kwa lengo la kutunza mazingira pamoja na kuufanya mji wa Kahama upendeze.
Mkuu wa wilaya kahama Fadhili Nkurlu akimwagia maji mti alioupanda wakati alipozindua kampeni ya upandaji miti
Mkuu wa polisi wilaya ya Kahama Mussa Mchenya akishiriki pia upandaji miti.
Afisa Usalama wa Wilaya ya Kahama Aretus Lyimo akishiriki upandaji miti wakati wa zoezi la uzindunzi wa upandaji miti milioni moja na laki sita.


PBPA KUSHUSHA TANI ZA MAFUTA 45,000 MAFUTA MWEZI MACHI

Na Joe Clanx Lieme, (TorintoHotMedia.Blog)

Wakala wa Serikali wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) leo 31 Januari 2017, wamekutana na wadau wa mafuta katika kuangalia fursa za uagizaji na usambazaji wa mafuta nchini ambapo kwa sasa pia wanaangalia fursa za kutumia bandari ya Tanga ili kusaidia wananchi wa Mikoa ya Kaskazini.

Hayo yameelezwa leo na Kaimu Wakala Mkuu wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja wa (PBPA) Modestus Lumato wakati akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Lumato amesema kuwa, kwa sasa PBPA inaangalia kushusha mafuta katika bandari ya Tanga ili kupunguza msongamano kwa bandari ya Dar es Salaam pamoja na kuondoa foleni..

Amesema mwezi uliopita wameanza kushusha mafuta bandari ya Tanga kwa kiwango kidogo kutokana na ukubwa wa eneo la awali, ambapo kwa sasa tenda inayofuata wanatarajia kushushia tena Mkoani Tanga kwani itasaidia wateja wao wa ukanda wa Kaskazini ikiwemo mikoa ya Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Manyara na mikoa mingine ya jirani.

“Tani za mafuta ya Dizeli na Petroli zinatarajiwa kwa awamu ijayo tukashuka bandari ya Tanga kwa kuanzia na tani 45,000. Mikoa ya Mwanza na jirani na mikoa hiyo itanufaika kwa kuja kuchukua bidhaa hiyo Tanga na kuliko kuja Dar es Salaam.” Alieleza Modestus Lumato.

Amesema kuwa wameshatangaza zabuni ambapo wamejitokeza wazabuni watatu katika zabuni hiyo iliyotangazwa .
 Kaimu Mkurugenzi wa wakala waagizaji wa mafuta kwa pamoja (PBPA) Modestus Lumato  wakati akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, 
 
Sehemu ya wadau wakifuatilia mjadala huo wakati wa mkutano na waandishi wa habari,

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

Thanks

MAADHIMISHO YA SIKU YA ARDHIOEVU DUNIANI TAREHE 2 FEBRUARI 2017


 TAARIFA KWA UMMA

MAADHIMISHO YA SIKU YA ARDHIOEVU DUNIANI TAREHE 2 FEBRUARI 2017

Kesho tarehe 2 Februari, 2017 ni maadhimisho ya siku ya Ardhioevu Duniani. Siku hii inaadhimishwa duniani kote kwa kutoa elimu na kuwakumbusha watu wote kuhusu uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za ardhioevu.
Ardhioevu ni maeneo ya ardhi yaliyopo kandokando na ndani ya Chemchem, Mito, Maziwa na mwambao wa bahari wenye kina cha maji yasiyozidi mita sita wakati wa kupwa. Ardhioevu pia hujumuisha Madimbwi, Mabwawa, Tingatinga na sehemu zote yanapokusanyika maji kipindi kirefu cha mwaka.
Tanzania hujumuika na nchi nyingine wanachama wa Mkataba wa “Ramsar” kuadhimisha siku ya ardhioevu duniani Februari 2 kila mwaka. Ujumbe wa mwaka huu wa Siku ya Ardioevu ni: "Ardhioevu Hupunguza Athari za Majanga” (Wetlands for Disaster Risk Reduction)". 
Tafsiri ya kauli mbiu hii ni kwamba, Ardhioevu huzuia majanga ya mafuriko yanayoweza kutokea katika pwani za bahari, hupunguza athari za kiafya zinazoweza kujitokeza kutokana na madini hatarishi kama Zebaki, hupunguza uwezekano wa kutokea kwa baa la njaa kwa kuwa maeneo okozi wakati wa kiangazi kama vyanzo vya maji na chakula kwa binadamu na wanyama. 
Ardhioevu pia ni maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa chakula kama vile mpunga na mbogamboga na chanzo cha maji yanayotumika kwenye kilimo cha umwagiliaji nchini. Arhioevu pia ni sekta endeshi ya uchumi wa nchi kwa kuwa ni chanzo cha maji yanayotumika kwenye kilimo, viwandani pamoja na uzalishaji wa umeme wa maji kwa gharama ndogo.
 Inakadiriwa kuwa asilimia 10 ya ardhi ya Tanzania ni ardhioevu ambayo ni muhimu kwa bioanwai, uchumi, shughuli za kijamii na kiikolojia. Maeneo haya ni makazi muhimu ya aina mbalimbali za viumbe hai wakiwemo samaki, viboko, mamba, ndege na viumbe wengine wasio na uti wa mgongo. Katika ikolojia ya ardhioevu tunapata bioanwai kubwa kuliko eneo lingine lolote duniani. 

BUNGE LAPITISHA MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA YA MSAADA WA KISHERIA WA MWAKA 2016.


Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo, Mjini Dodoma limepisha Muswada wa Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria wa Mwaka 2016 (The Legal Aid Bill, 2016).

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe alipokuwa akitoa taarifa wakati wa kuwasilisha muswada huo amesema kuwa muswada huo wa sheria umepitia hatua nyingi na umechukua muda mrefu hadi kufikia hatua ya kujadiliwa na Bunge tukufu.

Aliendelea kwa kusema kuwa muswada huo unapendekeza kutungwa kwa sheria ya msaada wa kisheria kwa lengo la kuanzisha (kwa mara ya kwanza katika histori ya nchi) mfumo wa kisheria wa kusimamia, kuratibu, kurasimisha na kutambua utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria katika mashauri yote ya Jinai na Madai kwa mahitaji.

Aidha utaratibu uliokuwepo kwa miaka mingi kwa upande wa Serikali unahusu baadhi tu ya makosa ya Jina, makosa yenye adhabu kubwa kama vile ya kunyongwa hadi kufa na vifungo virefu. Ambapo huduma hiyo imekuwa ikitolewa katika ngazi ya Mahakama Kuu pekee na kwa wigo mdogo tu pale inapohitajika kwa maslahi ya haki na kwa maelekezo ya Jaji Mkuu au yeyote aliyekasimiwa mamlaka ya kutoa maelekezo hayo.

“Kumekuwepo na ongezeko kubwa la mahitaji ya huduma ya msaada wa kisheria na wasaidizi wa kisheria. Kutokana na hali hiyo, Serikali imeona ulazima wa kuanzisha mfumo wa kusimamia na kuratibu utoaji wa huduma hiyo ili kuhakikisha inatolewa na watu wenye sifa, kwa wahitaji halisi na kwa taratibu zinazofahamika ili iendane na matakwa ya kikatiba,” alifafanua Dkt. Mwakyembe.

Vile vile ameeleza kuwa muswada huo unalenga kuwatambua wasaidizi wa kisheria, kufuta sheria ya msaada wa kisheria (katika mashauri ya Jinai).

Kwa upande wake Mbunge Selemani Zedi amesema kuwa, muswada huo utawasaidia wananchi ambao hawana uwezo wa kuwalipa Mawakili wanapohitaji msaada wa Kisheria.

Aidha, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson ameipongeza Serikali kwa muswada huo muhimu ambao Bunge umeipitisha unasuobiria kutiwa saini na Mhe. Rais ili kuwa Sheria.

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAWAPIGA MSASA WABUNGE WA KAMATI YA KUDUMU YA ARDHI

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) David Kanyatta akiwasilisha mada kwa Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu madhara ya kulishia mifugo ndani ya hifadhi kunavyoathiri sekta ya utalii katika semina iliyofanyika jana mjini Dodoma .
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Yussuf Hussein, akichangia hoja mara baada ya mada kuweza kuwasilishwa na wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu utalii wa baharini ambao umekuwa haupewi kipaumbele katika kutangazwa pamoja na kuendelezwa katika semina hiyo.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Marwa Chacha, (katikati) akichangia hoja mara baada ya mada kuweza kuwasilishwa na wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu wanyamapori waharibifu wa mazao kama vile tembo wanavyoathiri maisha ya wapiga kura wake kwenye vijiji vinavyozunguka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti katika semina iliyofanyika jana mjini Dodoma. Wengine ni wajumbe wa kamati hiyo .
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Atashasta Nditiye, (katikati) Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ( kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani ( wa kwanza kulia) wakifuatilia kwa makini michango ya wajumbe wa kamati hiyo wakati walipokuwa wkichangia hoja kuhusu mada mbalimbali zilizotolewa na wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu madhara ya kulishia mifugo ndani ya hifadhi, tatizo la ujangili wa tembo na faru pamoja madhara yanayosababishwa na wanyama waharibifu wa mazao kama vile tembo katika vijiji vinavyozunguka hifadhi nchini, iliyofanyika jana mjini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Devota Minja, MB ( wa kwanza kulia) pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalamu wa Wizara hiyo kuhusu madhara ya kulishia mifugo ndani ya hifadhi, tatizo la ujangili wa tembo na faru pamoja madhara yanayosababishwa na wanyama waharibifu wa mazao kama vile tembo katika vijiji vinavyozunguka hifadhi nchini katika semina iliyofanyika jana mjini Dodoma. Kwa upande wa kushoto ni viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj.Gen. Gaudence Milanzi ( wa kwanza kulia) pamoja na na viongozi wa taasisi katika semina ya kamati ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii iliyofanyika jana mjini Dodoma .

MGODI WA BUZWAGI WALIPA KODI ZAIDI YA MIL 700 KWA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA

HALMASHAURI ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga imepokea kiasi cha Sh Mil 700,040,000 kutoka kwa kampuni ya Acacia inayomiliki mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi ikiwa ni sehemu ya kodi ya huduma (service levy) ya kipindi cha mwezi Julai na Desemba 2016.

Kiasi hiki ni zaidi ya kilichotolewa kipindi cha Julai na Desemba mwaka 2015 ambapo mgodi huo uliikabidhi halmashauri ya mji wa Kahama hundi yenye thamani ya kiasi cha sh Mil 500,088,000 kama kodi ya huduma ikiwa ni utekelezaji wa sheria kwa kulipa kodi zilizopo kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Hundi ,Meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo alisema Buzwagi inamatumaini makubwa kuwa katika siku za karibuni halmashauri itaanza kutekeleza mradi huo na hivyo kutoa matumaini kwa wananchi wa Kahama kupata huduma nzuri za afya ndani ya wilaya.

“Mpaka sasa kama Kampuni tumekwisha kabidhi kwenu takribani kiasi cha bilioni 1.4 hii ikiwa na maana ya kodi yote ya ushuru wa huduma katika kipindi cha mwaka 2016, wananchi wangetamani kuona mradi huu unaanza maana kiasi hicho kilichopo kama kitatumika kinaweza kutekeleza sehemu kubwa ya mradi huu kwa kuanzia wakati tukisubiri awamu zingine” alisema Mwaipopo.

Katika hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika katika viwanja vya makazi ya viongozi katika wilaya hiyo,Mwaipopo alisema licha ya Kampuni yake kulipa kodi mbalimbali bado imekuwa ikijishughulisha katika kuhakikisha inakuwa mdau muhimu wa maendeleo kwa kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yanayozunguka Mgodi.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Fadhili Nkurlu aliyepokea hundi hiyo kutoka kwa uongozi wa Buzwagi na baadae kuikabidhi kwa mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama ameupongeza uongozi
wa Mgodi wa Buzwagi kwa jitihada ambazo wamekuwa wakizifanya katika kuhakikisha wanalipa kodi mbalimbali pamoja na jushirikiana na Jamii katika kutekeleza miradi mbalimbali.

Alisema Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi umeekua mstari wa mbele katika kulipa kodi mbalimbali ambako mpaka kufikia sasa zimefikia zaidi ya shilingi bilioni 197 ambazo zimetolewa katika vipindi tofauti.

Akizungumzia matumizi ya pesa hizo katika kutekeleza mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Kahama Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kahama Anderson Msumba alisema halmashauri iko katika hatua za mwisho za utekelezwaji wa ujenzi huo.

Miloni 700,040,000 zilizotolewa zinafanya juma ya pesa zote zilizotolewa katika vipindi vya miaka miwili kufikia Bil 1.2 fedha ambazo zitasaidia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ukiwemo wa Afya.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo(wa pili kutoka kulia) na Meneja Uendelevu wa Mgodi wa Buzwagi ,George Mkanza wakikabidhi hundi ya kodi ya huduma ya zaidi ya Sh Mil 740 kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Fadhili Nkurlu(wa pili toka kushoto) tukio lililofanyika juzi mjini Kahama ,Wa kwanza kushoto ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Kahama Bi Marry Manyambo.
Mkuu wa Wilaya Kahama,Fadhili Nkurlu na akimkabidhi hundi iliyotolewa na Mgodi wa Buzwagi kama Kodi ya Huduma yenye thamani ya zaidi ya Sh Mil 740 , Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Anderson Msumba kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa hospitali kubwa ya wilaya ya Kahama, mradi ambao ujenzi wake utategemea fedha zinazotokana na kodi za ushuru wa huduma unaolipwa na Mgodi huo.
Baadhi ya waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Kahama wakifuatilia hafla ya kukabidhi hundi kwa halmashauri ya mji wa Kahama.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo akiwahutubia waheshimiwa madiwani wa halmashauri ya Kahama pamoja na wadau mbalimbali waliohudhuria hafla ya kukabidhi hundi kwa halmashauri ya Mji wa Kahama
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu (aliyesimama) akihutubia wageni waalikwa wakati wa hafla ya kupokea hundi ya ushuru wa huduma kutoka Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi. Kutokea kushoto waliokaa ni Katibu
tawala wa wilaya Kahama Timothy Ndanya na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo.
Mkuu wa wilaya Kahama na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi wakiteta jambo.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.



NBC YAWAPONGEZA WAFANYAKAZI WAKE BORA

 Mkuu wa Idara ya Mauzo wa NBC, Mongateko Makongoro (mwenye suti nyeusi) akipiga picha ya pamoja na washindi wa tuzo ya utoaji wa mikopo binafsi walioingia kwenye Kundi la Watu Mashuhuri wa NBC lijulikanalo kama ‘ ‘Kundi la Shilingi Billioni Moja’. Tuzo hizo zilitolewa kwenye sherehe maalum ya kuwatunuku watumishi bora kwa mwaka 2016. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Huduma Reja Reja za Kibenki wa NBC, Filbert Mponzi (wa tatu kushoto), akipiga picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi bora waliofanya vizuri katika mwaka 2016 walio chini ya kurugenzi yake, katika sherehe maalum ya kuwatunuku watumishi bora kwa mwaka 2016. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
 Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Corporate, Mariam Kombo (kushoto), akionyesha cheti alichotunukiwa mara baada ya kutangazwa meneja bora wa mwaka 2016 kutokana na utendaji wake mahiri katika sherehe maalum ya kuwatunuku watumishi bora. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma Rejareja za Kibenki wa NBC, Filbert Mponzi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.  
 Meneja wa amana za wateja NBC, Dorothea Mabonye (kushoto), akikabidhi kombe la ushindi kwa Meneja wa Tawi la NBC Sea Cliff baada ya tawi hilo kuibuka kidedea katika kutoa huduma za kibenki kwa wateja wa akaunti ya malengo kwa mwaka 2016 . Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
  

BREAKING NYUZZZ: MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YATANGAZWA

Matokeo ya Kidato cha nne kwa wananfunzi waliohitimu mwaka 2016, yametangazwa wakeza kuyaona kwa KUBOFYA HAPA


HAKUNA MUDA WA KUONGEZA UHAKIKI WA TIN NAMBA KWA MKOA WA DAR ES SALAAM

Na Joe Clanx Lieme, Globu ya Jamii 

MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA) imesema uhakiki wa namba ya utambulisho ya mlipa kodi ‘TIN Number’ kwa Mkoa wa Dar es Salaam  umekwisha na uhakiki mwingine utahamia Mikoa mingine. 

Akizungumza na Blogu ya Jamii ya Michuzi ,jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo amesema uhakiki TIN Number muda wake ulikuwa ukiongezeka kutokana na mahitaji. 

Kayombo amesema kuwa kwa sasa muda hautaongezwa ,na wenye Tin number hawatakiwi kutumia mpaka pele watakapopata maelezo katika ofisi za TRA ili waweze kuendelea kutumia namba hizo. 

Amesema uhakiki huo ulianza Agasti hadi Oktoba na kuongeza tena muda wa miezi mitatu ambao umeishia leo. 

Kayombo amesema kuwa wale ambao wana Tin number na zinadaiwa TRA wanazo na wanatakiwa kulipa kodi zao ambazo wanadaiwa. 

Amesema uhakiki wa Number unasaidia kupata taarifa za mfanyabiashara kwa namba ya simu, makazi, sehemu anayofanyia kazi pamoja na anuani za mlipa kodi. 

‘’Watu wote wenye Tin Number wasizitumie mpaka pele watapokuwa wamepata maelezo juu ya kuzitumia namba hizo za utambulisho wa wafanyabiashara’’ amesema Kayombo. 


Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo akizungumza na Blogu ya Jamii ya Michuzi juu ya uhakiki wa Tin Namba leo jijini Dar es Salaam.  


 
Sehemu baadhi ya wananchi wakiwa katika uhakiki wa TIN namba leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Joe Clanx Lieme).


RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MARAIS MBALIMBALI WA AFRIKA KATIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA AFRIKA (AU) MJINI ADDIS ABABA ETHIOPIA

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kwenye mazungumzo yake pamoja na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Akinwumi Adesina mara baada ya kumaliza mazungumzo yao mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kabla ya kuanza mazungumzo yao rasmi katika moja ya Ofisi za AU mjini Addis Ababa Ethiopia.


0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *