WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumamosi, 14 Machi 2026

 08:04      No comments

 Na Jerome mlaki 0789106710



Na Torintohot 

Dar es Salaam leo imekuwa mwenyeji wa mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja (Joint Permanent Commission - JPC) kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Uganda, mkutano unaolenga kuimarisha zaidi uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili jirani.

Mkutano huo umefunguliwa rasmi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo, ambaye amesisitiza umuhimu wa jukwaa hilo kama sehemu muhimu ya kuimarisha mahusiano ya pande mbili pamoja na kupanua ushirikiano katika sekta mbalimbali.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Balozi Shelukindo amesema kuwa Tume ya Kudumu ya Pamoja inatoa fursa muhimu kwa nchi hizo mbili kufanya mazungumzo yenye kujenga, kupitia maendeleo ya ushirikiano uliopo, pamoja na kubaini maeneo mapya ya ushirikiano yatakayowanufaisha wananchi wa Tanzania na Uganda.

Aidha, mkutano huo unawakutanisha maafisa waandamizi wa serikali kutoka Tanzania na Uganda kwa lengo la kupitia utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa katika mikutano iliyopita ya JPC pamoja na kujadili namna bora ya kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara, miundombinu, nishati na usafirishaji.

Vilevile, majadiliano yanatarajiwa kujikita katika kutafuta suluhu za changamoto zinazoweza kuathiri biashara ya mipakani kati ya nchi hizo mbili, ikiwemo kuondoa vikwazo vya ushuru na visivyo vya ushuru ili kurahisisha biashara na kuongeza fursa za kiuchumi kwa wananchi wa Tanzania na Uganda

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *