Torintohot media Blog
Na Jerome Mlaki wa Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi mkoa wa Dar es Salaam Mh. Abas Mtemvu ameendelea Tena na ziara Kata ya kisarawe 2 ambapo amejionea changamoto mbalimbali Katika kata hiyo ikiwemo uharibifu wa miundombinu ya Barabara kutokana na mfululizo wa Mvua zinazoendelea kunyesha kwa wingi jijini Dar es Salaam.
Mh. Abas Mtemvu amesema Serikali ya Mh. Rais Dk.Samia Suluhu Hasani kupitia chama Cha Mapinduzi ni sikivu na Ipo tayari kutatuachangamoto zinazoikabili kata hiyo na kuhakikisha Mazingira yanaboreshwa Ili wananchi waweze kuishi mazingiryatakayo ridhisha.
Akizungaumza Katika kata ya kisarawe 2 Mjumbe wa halmashauri Kuu ya taifa Mh. Mneki ameeleza kuwa kero zote alizozisikia katika kata ya kisarawe 2 kata hizo ni kigogo, tumaini, ligato, mwaninga, mwas'onga, Ngome Mapinduzi, Mkamba, Madege, Vumilia Ukooni n k changamoto zote Sana zinahusu ujenzi barabara au madarasa.
Mh. Juma Simba Mneki ameeleza kuwa Tayari Ujenzi wa barabara kutoka kibada mpaka kimbinji umeshaanza na inatarajiwa ujenzi wa barabara hiyo utakamilika kabla ya uchaguzi.
Mh.Juma Simba Mneki ameeleza kuwa kero nyingine Katika kata hiyo ambayo imesumbua wananchi kwa mda mrefu ni ujenzi wa daraja la Sangatini ambapo Mh. Mneki ameeleza kuwa Ujenzi wa daraja Hilo upo karibuni kuanza hivyo adha wanayokumbana wananchi itamalizika.
Ziara hii imelenga kufanya tathmini ya miradi mbalimbali ya maendeleo Ili kubaini mapungufi yaliojitokeza Katika utekelezaji yaweze kufanyiwa Kazi.
Hata hivyo pia Mh. Juma SimbaMneki ameongelea wanachama kujenga ushirikiano utakao leta Faida kwa chama na wananchi waliokiamini na kukiweka madarakani.
Ziara hii imeamsha ari na hamasa kwa makatibu wenyeviti Serikali za mita na watendaji wote kuongeza spidi Katika utekelezaji wa miradi mbalimbali itakayochochea maendeleo Katika taifa.
0 maoni:
Chapisha Maoni