Torintohot media Blog.
Na Jerome Mlaki wa Dar.
Wafanya biashara wa samaki Katika soko la feli Dar es Salaam wanapitia Hali ngumu kwa sasa kutokana na uhaba wa samaki Katika soko la samaki Feli
Mwandishi wetu ametembelea soko la feli na kujionea Hali ilivyombaya Sana ya ukosefu wa samaki pamoja na mrundikano wa wafanyabiashara wa samaki wakihangaika kutokana na ukosefu wa bidhaa hiyo muhimu Katika Moja kati ya hitaji muhimu Sana jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wetu amefanya mahojiano na Mkurugenzi wa soko Mh. Mfinanga amesema kuwaMvua kubwa na upepo mkali baharini jambo linalosababisha samaki kwenda mbali na Katika kina kirefu na kusabisha samaki kutopatikana kwa urahisi.
Hata hivyo ameeleza kuwa Hali ya Mvua nyingi na upepo mkali baharini husababisha wavuvi wengi wasiingie baharini kwa kuhofia vyombo vyao kuzama na hata wao kupoteza maisha.
Nae Abeid Muhammed Shamte Mmoja kati ya viongozi wa soko la feli amesema kuwa Hali ya samaki kuadimika imesababisha hata bei ya samaki kupanda Sana tofauti na awali kabla ya Hali hii kujitokeza.
Hata hivyo Shamte ameongeza kuwa wameendelea kutoa elimu kwa watumishi wote wa soko na wateja kwa ujumla waendelee kutumisha Hali safi ya mazingira Ili kujiepusha na athari za kiafya zinazoweza kujitokeza kwa kusabishwa na mazingira machafu kama magonjwa ya mlipuko na n.k
Nae Mmoja kati ya wafanyabiashara wa samaki Katika soko la feli Dar es Salaam Ahmed Juma amesema ukosefu wa samaki ni jambo linaloendelea kufifisha mitaji ya wafanyabiashara na kuendelea kukosekana hitaji Hilo kwa walaji.
0 maoni:
Chapisha Maoni