Torintohot Blog.
Na Jerome Mlaki wa Dar
Dar es salaam,
Akizungumza katika uzinduzi wa maonesho hayo naibu waziri Kasekenya amesema maonesho hayo ni muhimu kwani yamewakutanusha wadau mbalimbali wa ujenzi kutoka ndani na nje ya nchi
Maonesho ya dar construction expo 2023 yamefunguliwa rasmi hii leo jijini Dar es salaam na naibu waziri wa ujenzi Godfray Kasekenya.
Kasekenya amesema kuwa sekta ya ujenzi hapa nchini imezidi kukua siku baada ya siku hivyo kupitia maonesho hayo watanzania wataweza kukutana na makampuni mbalimbali bora ya vifaa vya ujenzi kutoka hapa nchini na yale ya nje ya Tanzania.
"maonesho haya ni muhimu sana kwenye sekta ya ujenzi hivyo niwapongeze kampuni ya Dar expo kwa kuyaandaa"amesema Kasekenya
Awali akizungumza katika uzinduzi huo,muandaaji wa maonesho hayo Deogratius Kilawe amesema Maonesho hayo yanatarajiwa kuwa ni ya siku Tatu kuanzia leo Tarehe 11- 13 Oktoba 2023 ambapo yanafanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dae es salaam.
Amesema maonesho hayo ni jukwaa muhimu katika kuwakutanisha wadau wa sekta ya ujenzi.
Aidha katika hatua nyingine ameipongeza bodi ya wakandarasi hapa nchini kwa kusimamia ujenzi wa miundombinu mbalimbali yakiwemo madaraja na barabara zenye ubora hali iliyopelekea Taifa kuwa na Miundombinu bora.
0 maoni:
Chapisha Maoni