Na Jerome Mlaki wa Dar.
- CDF amewataka viongozi wa Shirika la Suma JKT kukaa na wataalamu wa uchumi kushauriana na kuja na mfumo mzuri utakaoleta tija na faida katika uendeshaji wa kiwanda cha maji ya kunywa kinachomilikiwa na shirika hilo.
Aidha amesema kuwa endapo wataalam watakaa na kuchakata mawazo tofauti ya kukabiliana na changamoto katika biashara anaamini lazima watapata mawazo chanya yatakayo tatua changamoto mbalimbali za kibiashara na hivyo itasaidia kuongeza uzalishaji Hali itakayosaidia wafanyakazi kuongezewa mishahara na hata kuzaa ajira Mpya kwa watanzania.
Ikumbukwe kwamba Kiwanda hiki kinaozalisha maji ya kunywa yanayoitwa “Uhuru Peak Pure Drinking Water”, kilianzishwa rasmi tarehe 17 Aprili 2018 kwa jina la SUMAJKT Bottling Plant. Kilisajiliwa kuwa Kampuni kwa jina la SUMAJKT Bottling Co. Ltd mwaka 2020. Kiwanda kipo katika eneo la Mgulani JKT jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya kiwanda ni “The Peak of Natural Purity”.
Wazo la uanzishwaji kiwanda cha maji lilikuja baada ya SUMAJKT kutaka kufufua kiwanda kilichokuwa cha dawa za binadamu cha TANZANSINO kwa kushirikiana na Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (TSSA). Tathimini ya kitaalamu ilifanywa kwa ushirikiano wa watendaji kutoka SUMAJKT, NHIF na MSD katika eneo la TANZANSINO na kushauri kuwa eneo halikidhi vigezo vya uanzishaji wa kiwanda cha kisasa cha dawa za binadamu. Kwa kuzingatia ushauri huo Shirika liliamua kuanzisha kiwanda cha maji ya kunywa katika eneo hilo.
Maji yanayozalishwa na kiwanda hiki ni sehemu muhimu ya huduma ya maji ya kunywa safi na salama inayotolewa kwa jamii vikiwemo Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Taasisi za Serikali na watu binafsi katika maeneo mbalimbali ya nchi
CDF ametaka viongozi wa Shirika la Suma JKT kukaa na wataalamu wa uchumi kushauriana na kuja na mfumo mzuri utakaoleta tija na faida katika uendeshaji wa kiwanda cha maji ya kunywa kinachomilikiwa na shirika hilo.
Kiwanda hichi ni cha kisasa kinazalisha maji kwa yenye kiwango Cha juu Cha ubora na kimefanikiwa kutengeneza maji yenye ujazo tofauti tofauti kilingana na mahitaji ya wateja
0 maoni:
Chapisha Maoni