\
Na Jerome Mlaki wa Dar
Leo hii Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mh.Albert Chalamila amewataka Wadau wa Bima nchini kuangalia namna mpya yakuwa na maboresho katika bidhaa za kibima ili kuwavutia wateja wengi waweze kujiunga.
Mkuu wa mkoa ameongeza kuwa hayo alipokuwa akifungua Semina kwa mawakala wa Bima katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema kuwa kama mawakala wa Bima watakuwa wabunifu katika kutoa huduma zao hali hiyo itawavutia watu wengi.
Ameeleza kuwa Watanzania wengi wamekuwa wakikata bima hasa za magari ili kuepukana na changamoto za kukamatwa na askari wa usalama barabarani jambo ambalo sio makusudi ya kukata bima .
"Kwenye bima hasa kwenye third part watu wanakata bima sio kwasababu wameelekezwa faida za bima bali wanakata kwasababu watakutana na Traffic barabarani na huo ndio ukweli na si kwasababu wanajua Umuhimu wa bima" Amesema Chalamila.
Hata hivyo amelipongeza Shirika la Bima Nchini (NIC) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Huduma za Bima Nchini (TIRA) kwa kutoa mafunzo hayo kwa mawakala ambapo ameongeza kuwa kuna haja kuhuhisha maarifa kwa mawakala, Askari wa kikosi cha Usalama Barabarani na Wadau wengine wa bima ili watanzania waone faida ya kuwa na bima.
Ameendelea kwa kubainisha kuwa Serikali inampango wa kutoa elimu ya bima kupitia wadau mbalimbali ikiwemo NIC ili mpaka kufikia 2030 angalau asilimia 50 ya Watanzania wawewanatumia bima hasa za Afya huku akiitaka sekta ya bima kujitafakari ilipo,inapokwenda na wapi inaweza kuwafikia watu wengi zaidi.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Huduma za Bima Nchini ambaye ni Meneja wa ukaguzi wa TIRA Frank Shangali Amesema TIRA itapendelea kusimamia sekta hiyo, makampuni ya bima na watoa huduma za bima kote nchini ambapo kwa Sasa kuna zaidi ya mawakala 1300 ambapo TIRA itahakikisha mawakala hao wanaongezeka.
Amebainisha kwamba TIRA kwa kushirikiana na NIC wamekuwa na mpango wa kutoa elimu ya bima ambapo wameanza na watoa huduma (mawakala) kwa kuwapatia mafunzo yenye lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za bima kupitia wao.
Nae Meneja wa Biashara na Huduma kwa Mawakala wa Shirika la Bima la Taifa NIC Kafiti Kafiti NIC imekuwa mdau mkubwa wa bima hapa Nchini na kupitia mawakala hao wanaowapa mafunzo hayo wamechangia kuwafikia wanachi wengi zaidi hali iliyosababisha kuwapa mafunzo ili kuwajengea uwezo zaidi .
Ameongeza kuwa NIC ndio Shirika la Bima pekee lenye mawakala wengi zaidi hapa Nchini ambapo kwenye mawakala 1300 hapa nchini NIC lina zaidi ya mawakala 700
Hata hivyo ametoa rai kwa watanzania kutumia huduma za bima za NIC ili kuhakikisha wanatimiza dira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa ifikapo 2030 Asilimia 50 ya Watanzania wawe wanatumia huduma za bima na wao kama NIC wanatimiza hilo.
0 maoni:
Chapisha Maoni