Na Jerome Mlaki wa Dar
Mamlaka ya huduma za nishati na maji nchini (EWURA) usiku wa kuamkia leo, imetangaza bei mpya za mafuta zitakazoanza kufanya kazi kuanzia Jumatano hii, Oktoba 04, 2023 ambapo katika bei hizo inaonesha mafuta ya Dizeli yamepanda zaidi ukilinganisha na aina nyingine za mafuta
Taarifa kwa umma iliyotolewa na mamlaka hiyo inaonesha kuwa mafuta ya Dizeli sasa yatapatikana kwa Tsh.3520/- kwa lita wakati Petroli na mafuta ya taa yatakuwa yanauzwa kwa Tsh.3353/- na Tsh.3016/-
Imeelezwa sababu ya kupanda kwa bei hizo kuwa ni kupanda kwa gharama za mafuta katika soko la Dunia hadi kufikia asilimia 4.21 na gharama za uagizaji wa mafuta hadi kufikia asilimia 17 kwa Petrol, asilimia 62 kwa Dizeli na asilimia 4 kwa mafuta ya taa, lakini pia sababu nyingine iliyotajwa kupelekea kupaa kwa bei hizo ni uamuzi wa wazalishaji wakubwa wa mafuta Duniani (OPEC+) kupunguza uzalishaji na vikwazo vya kiuchumi ambavyo nchi ya Urusi imewekewa na mataifa ya magharibi
Aidha katika taarifa hiyo ya EWURA iliyosainiwa na Mkurugennzi Mkuu wake Dkt.James Mwainyekule imewakumbusha wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla na rejareja sambamba na jamii yote kuzingatia bei za kikomo zilizowekwa
Katika bei hizo ambazo zonapaswa kuchapishwa kwenye mabango yanayoonekana bayana katika vituo vyote vya mafuta nchini zinaonesha kuwa bei za rejareja za mafuta ya Petrol kwa mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara kuwa ni Tsh.3281/-, Tsh.3287/- na Tsh.3283/-, Dizeni ni Tsh.3448/-, Tsh.3494/- na Tsh.3590/- na mafuta ya taa ni Tsh.2943/-, Tsh.2989/- na Tsh.3016/- kwa lita
0 maoni:
Chapisha Maoni