Na Jerome Mlaki wa Dar
"Ndege ya abiria ya masafa ya kati aina ya B737-9MAX ambayo uundaji wake umekamilika inatarajia kuwasili nchini tarehe 03 Oktoba, 2023. Ndege hiyo inauwezo wa kubeba abiria 181 katika madaraja mawili ambapo daraja la kawaida “economy class” ni abiria 165 na daraja la biashara (business class) abiria 16, pia uwezo wa kubeba mzigo wa tani 6 na kuruka wastani wa masaa 8 bila kutua," Alisema Prof. Mbarawa.
Aidha Prof. Mbarawa aliongeza kuwa Kuwasili kwa ndege hiyo kutaifanya ATCL kuwa na ndege 13 mpya zilizonunuliwa kutokana na utekelezaji wa mpango mkakati wa Serikali ulioanza kutekelezwa kuanzia mwaka 2016 na hivyo kuwa na ndege 14 zinazosimamiwa na ATCL katika uimarishaji wa wigo wa mtandao wa safari zake ndege kwa soko la ndani, kikanda na kimataifa.
Alisema hatua hizo ni pamoja na kukijengea uwezo Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa kukijengea majengo, ununuzi wa mitambo na vifaa vya kufundishia, ununuzi wa ndege za mafunzo, na kuweka miundombinu wezeshi kwa ajili kutoa Kozi za muda mrefu za Uhandisi wa Matengenezo ya Ndege (Degree and Diploma); Kozi za kutoa mafunzo ya Wahudumu wa Ndani ya Ndege (Cabin Crew) na Uendeshaji wa Safari za Ndege; Pamoja na Ndaki ya Chuo cha Urubani (Flight Crew).
"Hadi sasa Chuo kinatoa mafunzo ya Uhandisi wa Matengenezo ya Ndege, Uendeshaji wa Safari za Ndege pamoja na Uhudumu wa Ndani ya Ndege kwa Ithibati za TCAA. Vilevile, Chuo kinatoa mafunzo ya Air Fares and Ticketing, Airport Operations Fundamentals, Airline Marketing pamoja na Airline Customer Service kwa Ithibati ya IATA," Alisema Prof. Mbarawa.
Alisema Katika kuongeza ufanisi wa mafunzo ya urubani Juni, 2023 Serikali ya Awamu ya Sita imewezesha NIT kuingia mkataba na ununuzi wa ndege moja ya mafunzo ya injini mbili aina ya Beechcraft Baron G58 toka Kampuni ya Textron Aviation Inc. ya Marekani na Ndege hiyo inatarajia kuwasili katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2024/2025. Kuwasili kwa ndege hii kutawezesha wahitimu wa kozi ya CPL kufanya mafunzo ya Multi-Engine Class Rating na Multi-Engine Instrument Rating hivyo kukidhi vigezo vya kuingia kwenye ajira.
0 maoni:
Chapisha Maoni