Na. Jerome Mlaki wa Dar.
Mkurugenzi mkuu wa NSSF. Masha Mshomba ameonana na wahariri wa vyombo vya habari hii Leo na ameelezea Fursa mbalimbali za uwekezaji na kuwaomba wanahabari washirikiane katika kutoa elimu kwa wananchi katika suala zima la uwekezaji.
Ikumbukwe kwamba Trilioni 6.08 na kuwa mpaka kufikia mwezi Juni 2023 thamani ya Mfuko imefikia trilioni 7.6 kwa hesabu ambazo zinaendelea kukaguliwa.
“
Huo ni ukuaji mkubwa mno hasa ukizingatia kabla ya hapo na baada ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingia madarakani thamani ya Mfuko ilikuwa ni trilioni 4.8 hivyo mafanikio hayo ni kazi kubwa anayofanya Mheshimiwa Rais ya kuvutia wawekezaji,” amesema Mshomba.
Amesisitiza kuwa, endapo elimu ya uwekezaji itatolewa kiufasaha kwa wananchi italeta chachu ya ongezeko la wanachama na michango, ambapo ameushukuru uongozi wa wahariri kwa ushirikiano mkubwa wanaowapatia.
Kuhusu matumizi ya TEHAMA, Mshomba amesema NSSF imeweka kipaumbele kikubwa katika matumizi ya TEHAMA ili kurahisisha huduma za wanachama wao jambo ambalo linaendana na kasi ya Rais Dk. Samia Suluhu Hasani.
Mshomba amesema NSSF inaendelea kusajili wanachama wapya kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi Kote inchini ambalo ndio lengo la Mfuko kushiriki katika maendeleo ya wanachama na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi inchini.
0 maoni:
Chapisha Maoni