Na Jerome Mlaki wa Dar.
Hatua hiyo imekuja ikiwa na siku chache zimepita tangu kufungiwa kwa vituo vingine viwili septemba 4 mwaka huu.
Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA)imevifungia vituo vitatu vya kuuza mafuta kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kutokuuza mafuta kwa maslahi binafsi,
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam,Mkurugenzi mkuu wa Ewura Dkt James Andilile amesema kuwa mamlaka hiyo ilikuwa ikivichunguza vituo hivyo ambavyo vimekuwa vikijihusisha na tabia ya kuficha mafuta na hatimaye kuvikuta na hatia na vimefungiwa kwa muda wa miezi 6.
"ndugu wanahabari mamlaka ilibaini kuwa pamoja na kuwepo na mafuta baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakichukua mafuta na kuchelewesha kufikisha vituoni huku wengine wakiwa na mafuta kwenye visima lakini hawauzi hivyo kusababisha kuwa na usumbufu mkubwa kwa wananchi,na nataka wafanyabiashara hao wajue kuwa ewura tuna vijana kila mahali wakifuatilia tabia hizo na watachukuliwa hatua wakibainika kuficha mafuta"amesema Dkt Andilile.
Mkurugenzi mkuu wa Ewura Dkt James Andilile akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo septemba 18,2023 |
Akivitaja vituo hivyo amesema ni pamoja na kituo cha mafuta cha Camel Oil-Gairo chenye leseni namba PRL-2019-164,pamoja na kituo cha mafuta cha Petcom-Mbalizi chenye leseni namba PRL-2023-025.
Kingine ni kituo cha mafuta cha Rashal Petroleum Ltd-Mkalama chenye leseni namba PRL-2019-034 ambavyo vimefungiwa kwa muda wa miezi sita ambapo kufungwa kwa vituo hivyo kunafanya vituo vilivyofungiwa kuwa vitano kwani septemba 4 mwaka huu Ewura ilitangaza kuvifungia vituo vya Camel Oil,Msamvu Morogoro na Matemba cha Turiani ambapo vingine vitatu bado vinachunguzwa kwa ajili ya hatua zaidi.
Hata hivyo Dkt Andilile amewatoa hofu wananchi wa maeneo vilivyofungiwa vituo hivyo kutokuwa na hofu ya kukosa huduma za mafuta kwani maeneo yote yana vituo vingine vya kutosha vya mafuta huku akiwataka wafanyabiasshara wa vituo vya mafuta kuachana na janjajanja ya kuficha mafuta ili wayauze bei mpya za mafuta zinapotangwazwa
0 maoni:
Chapisha Maoni