WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Alhamisi, 21 Septemba 2023

 21:22      No comments


Na Jerome Mlaki wa Dar.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Mhandisi Charles Sangweni, kuhusu kuharakisha mchakato wa kunadi vitalu vya utafutaji mafuta na gesi asilia nchini. Ametoa maelekezo hayo Septemba 20, 2023 kwenye kongamano la nishati linaloendelea katika Ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mkuu wa PURA Mhandisi Charles Sangweni (kulia) akimweleza jambo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa (kushoto) Septemba 20, 2023 wakati wa kongamano la nishati linaloendelea katika Ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

 


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) kuharakisha mchakato wa kunadi vitalu vya mafuta na gesi asilia nchini.


Majaliwa ameyasema hayo Septemba 20, 2023 pindi alipotembelea banda la PURA kwenye kongamano la nishati linaloendelea kwa siku mbili katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.


“Hakikisheni mnaongeza kasi katika mchakato wa kunadi vitalu vyetu ili wawekezaji waje kuwekeza katika utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini ili nchi inufaike,” aliongeza.


Akitoa taarifa fupi mbele ya Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mkuu wa PURA Mhandisi Charles Sangweni alieleza kuwa mamlaka inaendelea na shughuli za awali za utekelezaji wa duru ya tano ya kunadi vitalu vya mafuta na gesi kwa maeneo ya nchi kavu na baharini kwa lengo la kuongeza wawekezaji.


Aliongeza kuwa sambamba na maandalizi hayo PURA inaendelea kuweka mipaka ya vitalu vitakavyonadiwa na kuandaa vifurushi vya data (Data Packages) kwa kila kitalu. 


“Hadi sasa vitalu 26 vinafanyiwa uchambuzi ili kupendelezwa kwa ajili ya kuingizwa katika mnada. Kati ya hivyo, vitalu 15 vipo nchi kavu na 11 vinapatikana baharini,” alifafanua Mhandisi Sangweni alibainisha kuwa Serikali inatarajia kuzindua zoezi la kunadi vitalu kati ya mwezi Desemba, 2023 hadi Machi, 2024 baada ya kukamilika kwa shughuli za maandalizi zinazoendelea.


Inaelezwa kuwa zoezi la kunadi vitalu linakadiriwa kugharimu jumla ya shilingi bilioni 3.5. Aidha, kwa mwaka 2023/24 Serikali kupitia PURA imetenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya kazi za awali za maandalizi ya zoezi hilo.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *