WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Alhamisi, 21 Septemba 2023

 20:46      No comments

 Na. Jerome Mlaki wa Dar

 

Waziri wa Viwanda na Biashara Dokta Ashatu Kijaji akifafanua jambo katika mkutano na Viongozi, watumishi na waandishi wa habari katika kiwanda cha Dawa za Kuua Viluwiluwi wa Mbu kilichopo Kibaha Mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) Dkt. Nicolas Shombe akizungumza katika mkutano na Viongozi, watumishi na waandishi wa habari katika kiwanda cha Dawa za Kuua Viluwiluwi wa Mbu kilichopo Kibaha Mkoani Pwani.

Kibaha - Pwani
WaziriI wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji ameagiza kiwanda cha kuzalisha dawa za kuua viluwiluwi wa Mbu (TBPL) kuanza kuzalisha bidhaa za Viuatilifu hai kwa ajili ya Kilimo.

Akizungumza katika kikao na viongozi, Watumishi na waandishi wa mara baada ya kumaliza ziara kiwandani hapo kuona namna wanavyofanya uzalishaji amesema  kiwanda kianze kuzalisha bidhaa za Viuatilifu hai hususani kwa ajili ya Kilimo.

“Tayali Bidhaa za viuatilifu ambayo inatumika kwa ajili ya afya ya mimea tayali mamlaka za kupima ubora zilitupatia usajili hivyo ningependa bidhaa hii Mwezi wa 10 Mwaka huu ianze kuzalishwa kwa wingi na iingie sokoni kwani huu ni msimu wa Kilimo,” Alisema Waziri Kijaji.

Amesema serikali itahakikisha dawa hiyo inawafikia wakulima sambamba na kutoa elimu kwa wakilima dawa hiyo ni rafiki kwa Mazingira, afya ya Binadamu na mimea kwani haina kemikali na inawekwa katika mmea wa aina yoyote na haina madhara. 

Alisema dawa ya viluwiluwi vya kuua Mbu inayozalishwa katika kiwanda hicho imekubaliwa barani Afrika ambapo hadi sasa imefikia Nchi saba, ambazo miongoni mwake ni Kenya, Angola, Botwana, Msumbiji Niger na hivi karibuni itaanza kupelekwa nchini Uganda.

Aidha katoka hatua nyingne Dkt. Kijaji ameupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa hatua mbalimbali ambazo uongozi wa kiwanda hicho umezitekeleza kufatia maagizo aliyotoa alipotembelea kiwanda hicho.

"Nitoe rai kwa uongozi wa kiwanda kuendelea kutafuta masoko ya bidhaa ndani na nje, pamoja na jitihada za kuboresha kitengo cha masoko bidhaa zinazopelekwa kwa Nchi ni zaidi ya lita 207, 2000 na kuingiza zaidi ya shilingi milioni 3.

Mapema akizungumza wakati akimkaribisha waziri, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) Dkt. Nicolas Shombe amesema kiwanda hicho kinazalisha bidhaa za kibaolojia za kuulia viluwiluwi vya Mbu.

"Kiwanda hicho ni cha kipekee na cha Kimataifa kwamba pamoja na kuazalisha sawa hiyo ya viluwiluwi wa mbo lakini pia ni maabara kubwa bidhaa za kibaolojia" Alisema Dkt. Shombe

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *