NA Jerome Mlaki wa Dar.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 8, 2023 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Pulses Network (TPN) Zirack Andrew amesema mkutano huo wa mazoa ya chakula inafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika hususan nchini Tanzania.
Amebainisha kwamba zamani Afrika walikuwa wanalima Mazao kwa ajili ya kijikimu, lakini kwa sasa watu wamehama kwenda kilimo cha Biashara, hivyo maonesho haya yatawakutanisha wazalishaji wa Mazao ya chakula wa Afrika na wafanyabiashara wa Kimataifa ambao watayanunua mazoa hayo.
Taso Event Organizer imeandaa maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Mazao ya Kilimo yatakayofanyika Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Maonesho hayo ambayo yataanza Agosti 10 hadi 12 yatahusisha wataalam kutoka nchini India na makundi ya wakulima wa Bara la Afrika.
“Kutakuwa na vyama mbalimbali vya wakulima na lengo ni kuwakutanisha ili kupata uzoefu na masoko ya Mazao yao,” amesema Andrew na kuongeza,
“Zaidi ya Watu 3000 watembelea na kushiriki maonesho haya, dhamira ni kufungua masoko ya Mazao yetu ya chakula ya Afrika Kimataifa,”.
Kwamba kunapokuwepo na siko la uhakika la Mazao kunachochea wakulima kuzalisha zaidi.
Hivyo ametumia fursa hiyo kuwaalika watu wote kuhudhuria maonesho hayo ambapo kutakuwa na mijadala mbalimbali kuhusu Mazao tofauti tofauti, kutakuwa na teknolojia mbalimbali pamoja na kuingia mikataba mbalimbali ya kibiashara.
Kwa upande wake Mbobezi katika Kilimo Biashara kutoka nchini India G. Chandra Shekhar maonesho haya ni muhimu katika kuimarisha na kudumisha mahusiano ya kijamii na kiuchumi baina ya India na Afrika.
Amesema kuwa kupitia maonesho haya, wataweza kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili Kilimo cha Mazao na namna ya kukabiliana nazo ili kuhakikisha Kilimo kinastawi na wakulima wanakua zaidi.
Shekhar amesema kwamba Afrika imekuwa ndiyo mzalishaji Mkuu wa Mazao ya chakula kwa ajili ya Nchi ya India huku India ikiwa ndiyo mzalishaji mkubwa wa Mazao ya Biashara kwa ajili ya Afrika ambapo ametaja baadhi ya Mazao yanayozalisha nchini India na kuletwa Afrika kuwa ni pamoja na Kahawa, Mbegu za mafuta, na mkonge.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taso Event Organizer Suveer Rajpurohit amesema kwamba wanakuja barani Afrika kwa ajili ya kutafita fursa ya soko kwa mazao ya Kilimo ya Afrika na India.
Hivyo amewakaribisha wakulima kutembelea maonesho hayo ili kuona fursa mbalimbali zitokanazo na Kilimo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taso Event Organizer Suveer Rajpurohit akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Pulses Network (TPN) Zirack Andrew akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
0 maoni:
Chapisha Maoni