Na Jerome Mlaki, Dar es Salaam
Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam katika Kongamano la tano la kimataifa la maonyesho ya Nishati na Naibu Mkurugenzi wa Uwezeshaji wa shirika hilo Declan Mhaike wakati akizungumza na waandishi wa habari na kubainishakuwa miradi ya umeme wajua na Upepo ya Megawati170 hadi 100 inatarajiwa kutekelezwa.
Shirika la Ugavi wa Umeme Nchini (TANESCO) lipo katikaa hutua mbali mbali ya kuondokana na changamoto ya nishati ya umeme kwa kutekeleza miradi ya kimkakati ya uzalishaji wa umeme kwa njia ya upepo, jua na gesi.
Aidha Mkurugenzi huyo amesema miradi hiyo itaongeza mchango wake katika gridi ya Taifa kutoka asilimia 0.5 ya sasa hadi asilimia 20 ifikapo mwaka 2025.
Ameendelea kusema kuwa miradi inayoendelea kutekelezwa ni pamoja na wa megawati 100 wa upepo iliyopo Makambako Mkoani Njombe,
Mradi wa megawati 100 wa Upepo uliyopo Ismani Mkoani Iringa,pia Megawati 60 za Umeme jua uliyopo Dodoma,na Megawati 100 za umeme jua uliyopo Manyoni.
Ameongeza kuwa Mradi mwingine unaotarajiwa kutekelezwa ni ule wa Kituo Cha Kishapu ambao utazalisha megawati 50 hadi 150 ,huku kuna mradi mwingine utakaotekelezwa Wilayani Same .
Halikadhalika katika kongamano hilo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kwamba Serikali imejidhatiti kutekeleza vyanzo vingine vya umeme na sio kutegemea umeme wa Maji pekee na kwamba Tanzania
Lina mpango wa kua mzalishaji Mkubwa wa Nishati ya Umeme Duniani.
“Tunaendelea na utafutaji wa gesi, tunataka tuwe wazalishaji wakubwa wa nishati, tuwe na umeme wa kutosha utakaopatikana kwa urahisi na nafuu na ziada tutauza nje ya nchi."
Amesema kuwa Tanzania haitegemei kuzalisha umeme kwa kutumia maji pekee bali inaendelea kuweka mkazo katika uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati nyingine kama gesi na jua.
Waziri Mkuu amesema katika kongamano hilo la kimataifa la nishati ambalo limehusisha viongozi na wadau kutoka katika mataifa mbalimbali Duniani litajadili namna bora ya kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa nishati.
Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa kuzisisitiza nchi zote wanachama kuhakikisha taasisi za mafunzo zinatoa programu maalum za mafunzo katika sekta za nishati ili kuongeza idadi ya watu walio na ujuzi na maarifa kwenye sekta hiyo.
Amesema kuwa nishati ni sekta muhimu katika kufikia lengo la uanzishwaji wa viwanda na katika kuimarisha na kuwezesha uzalishaji na shughuli nyingine za kiuchumi. “Lazima tufanye kazi kwa ushirikiano na wadau wote ili kufungua fursa kwa Watanzania wote.”
Amesema ili kuwaendeleza wafanyabiaahara wa ndani na Watanzania kushiriki katika sekta ya nishati, Serikali itaendelea kuhakikisha kanuni na taratibu zinazofaa zinawekwa ili kuwezesha ushirikishwaji katika mnyororo wa thamani wa maendeleo kwenye sekta ya nishati.
Dkt. Biteko amesema zaidi ya kampuni 100 za nishati kutoka katika maeneo mbalimbali duniani zinashiriki katika kongamano hilo ambalo lilitanguliwa na mkutano wa viongozi wa nishati.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema wameendelea kutekeleza mipango mbalimbali waliojiwekea katika kuhakikisha umeme unapatikana wakati wote nchini.
0 maoni:
Chapisha Maoni