Na. Jerome Mlaki wa Dar.
WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELA) wamesema kwamba wameshiriki kwenye maonyesho ya biashara na utalii ya 10 ili kuweza kutoa elimu juu ya matumizi ya mifumo wanayosimamia kwa sasa ambao ni ORS na Tanzania Nationali Business Portal.
Hayo yalibainishwa na Afisa Usajili wa Wakala huo Julieth Kihwelu wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda lao lililopo eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho hayo ambapo wameamua kushiriki ili kusogeza karibu huduma kwa wakazi wa mkoa wa Tanga na mikoa ya kanda ya kaskazini.
Alisema kwamba mifumo hiyo ni mikuu pendwa ambayo mwombaji anatakiwa kutumia kuwasilisha ombi lake huku akieleza wanatoa huduma ya kuwafundisha namna ya kutumia mfumo huo kuweza kujisajili.
“Katika mifumo hii mwombaji anatakiwa awe na kitambulisho na Taifa,barua pepe aweze kujisaijili na nitoe wito kwa wajasiriamali nchini kuendelea kusajili alama za biashara zao kwa kuwa alama moja inamtumbisla mtu mmoja”Alisema
Afisa usajili huyo alisema kwamba wasiposajili alama zao wanaweza kutegeneza bidhaa ambayo kuna mtu mwengine anayo na amesajili kwa mujibu wa sheria kwa alama za biashara na huduma.
Hata hivyo aliwashauri wakazi wa Tanga na mikoa ya jirani waenda kupata huduma ya papo kwa papo ambapo kwa sasa wanaendelea kutoa huduma hiyo katika maeneo hayo.
“Tokea 28 mei mpaka Mei 31 tumekwisha kuwahudumia wananchi 35 na tukilinganisha mwaka jana na mwaka huu kuna utofauti na tunategemea kufikia watu wengi kwa kuwatembele kwenye mabanda hususani wajasiriamali kuweza kuwapa ushauri namna ya kuweza kusajili alama za biashara “Alisema Afisa huyo.
Hata hivyo aliwataka wajasiriamali na wafanyabiashara kufika kwenda banda lao kupata elimu na kufanyiwa usajili alama zao za bidhaa zao
0 maoni:
Chapisha Maoni