WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumatano, 31 Mei 2023

 13:26      No comments

 


Na. WAF,Dsm
Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuwapeleka watoto kupata chanjo mbalimbali zinazotolewa na Serikali kupitia Wizara ya afya.

Rai hiyo imetolewa leo na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid Mfaume wakati wa semina kwa waandishi wa habari wa Mikoa ya Mtwara, Lindi Pwani na Morogoro iliyofanyika kwenye ukumbi wa Anatoglo jijini Dar es Salaama.

Dkt. Mfaume amesema waandishi wa habari ni muhimu katika kuhamasisha masuala yote ya afya hususani  chanjo ili kuweza kuwakinga watoto magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.

Ameongeza kuwa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuhakikisha huduma za chanjo zinapatikana kila mahali ikiwemo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

"Tunamshukuru Rais wetu kwa uwekezaji mkubwa kwa sekta hii kwa upande wa chanjo tumepata majokofu yanayotumia nishati ya jua hakuna sababu tena ya kituo kukosa chanjo kwa sababu hii".

Aidha, amesema Mkoa wa Dar es Salaam wamepatiwa magari ya chanjo na hivyo kurahisisha utoaji wa chanjo na  kuwafikia watoto wote wanaolengwa kupata chanjo hizo.

Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Chanjo umetoa mafunzo kwa waandishi wa habari lengo ni kuwafikia waandishi wa mikoa yote Tanzania

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *