Na mwandishi wetu 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amewataka Watumishi wa Serikali  wawe na umoja na uawanifu  katika utendaji kazi wao   utakao leta chachu ya maendeleo ndani ya Mkoa huo. 


Wito huo umetolewa Leo Mkoani humo katika kikao kilicho wakutanisha Watumishi  hao wakiwemo Watendaji wa Kata na

 Mitaa waliopo kwenye Wilaya ya Kinondoni kwa lengo la kufahamiana na Mkuu Mpya wa Mkoa huo.


Akizungumza katika kikao Hicho Chalamila amesema Watumishi hao wanatakiwa kufanya kazi kwa weledi, kutatua changamoto zinazowakabili Wananchi na  kusimama vizuri miradi inayotekelezwa na Serikali lakini pia  waache vitendo vinavyovunja  Sheria za nchi  ikiwemo rushwa , uchoyo  


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule amesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ajali barabarani, ajali za moto, mafuriko, na Kipindupindu hususani maeneo ya Mwananyala, Makumbusho, kigogo, ambapo hali  hiyo ni kutokana na baadhi ya Wananchi kutiririsha ovyo maji machafu.


Aidha Mtambule ameongeza kuwa Rais Dr Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya bilioni 160 kwa lengo la kutatua hangamoto mbali zinazoikabili Wilaya hiyo ambapo wamefanikiwa katika Masuala mbalimbali ikiwemo Sekta ya Elimu.