Na. Jerome Mlaki wa Dar.
• Mbio za NBC Dodoma Marathon kufanyika tarehe 23.07.2023 Dodoma
• Zaidi ya wakimbiaji 6,000 kutoka nchi mbalimbali kushiriki
nchini.
Dar es Salaam, 23 Mei 2023. Benki ya NBC imetangaza kufanyika kwa mbio kubwa za NBC Dodoma Marathon mwaka 2023 siku ya Jumapili tarehe 23 Julai 2023 Jijini Dodoma.
Lengo kuu la mbio za NBC Dodoma Marathon ni kukusanya fedha ili kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi na kuchangia kutoa ufadhili wa elimu kwa wanafunzi wanaosomea taaluma ya ukunga ili kuboresha afya ya mama wa mtoto.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenziwa Fedha wa Benki hiyo Waziri Barnabas alisema; “Kupitia mbio hizi za NBC Dodoma Marathon,tunalenga kuchangia katika kuboresha afya ya uzazi kupitia sapoti kwenye mapambano dhidi ya kansa ya shingo ya kizazi kwa wanawake na pia kutoa ufadhili kwa wanafunzi wa taaluma ya ukunga nchini. Tunaamini kuwa kupitia shindano hili tuweza kuisaidia jamii yetu kupambana na changamoto hizi. Kupitia ufadhili wa wanafunzi wa elimu ya ukunga itasaidia kukabiliana na upungufu wa wataalamu hao na hivyo kupunguza vifo vya kina mama wakati wa uzazi. Vilevile tunaendelea na msaada wetu katikamapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi ambapo mpaka sasa tumeshakusanya zaidi yashilingi milioni 500 zilizosaidia kufikia upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake zaidi ya 23,500 na matibabu kwa zaidi ya wanawake 1,300. Tunajivunia mafanikio haya” alisema.
Akizungumza kuhusu mchango wa Benki ya NBC kwenye sekta ya michezo nchini, Ndugu Barnabas alisema; ”Benki ya NBC inatambua na kuthamini sana umuhimu wa michezo katika ujenzi wa taifa hususan katika kutoa ajira na kuongeza pato la taifa. Hivyo basi, tumeendelea kuwekeza katika michezo ikiwemo udhamini wetu mkubwa wa ligi kuu ya soka Tanzania yaani NBC Premier League ambayo imekuwa na matokeo chanya sana kwa taifa letu. Tunajivunia kuwa wadau wakubwa wa michezo nchini”.
Waziri pia alitumia fursa hii kuwapongeza na kuwashukuru taasisi ya ORCI ( Ocean Road Cancer Institute) na Benjamin William Mkapa kuwa wabunifu na kwa huduma wanazotoa ili kusaidia jamii kuimarisha afya ya mama na mtoto.
Vile vile aliwashukuru wadau wa mashirika na makampuni mbali mbali kama Sanlam, JubileeGeneral Insurance, Garda World, Cheknocrafts, Icea Lions Insurance, Metropolitan Life Insurance,Strategies Insurance, Hans Paul, SBC- Pepsi, na Aramex kwa udhamini wao ili kufanikisha mbio hizi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Julius Mwaiselage alisema kuwa taasisi hiyo inafurahia kujumuika tena katika mbio hizi jijini Dodoma baada ya mafanikio awali. “Dhamira yetu ni kuendelea kutoa elimu zaidiya saratani ya shingo ya kizazi ili kuimarisha afya ya mama na mtoto nchini. Saratani ya Shingo ya Kizazi, ndiyo inayoongoza kwa kusababisha vifo vingi zaidi vinavyohusiana na saratani kwa wanawake nchini Tanzania. Jambo la kutia moyo ni kwamba saratani hii inaweza kuzuilika na kutibiwa iwapo itagundulika mapema. Na kwa kuimarisha afya ya mama na mtoto tunajenga taifa lenye uwezo zaidi. Ni jukumu letu kwa pamoja kuunga mkono serikali yetu katika kuongeza uelewa na kuchangia uimarishaji wa afya za mama na watoto kulinda kizazi kijacho.” Alisema.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa programu kutoka Benjamin Mkapa Foundation alisema. "Nina furaha kujumuika na NBC katika mbio hizi kwani fedha zitakazo patikana katika mbio hizi zitasaidia kusomesha wakunga zaidi na kuboresha huduma ya afya kwa mama na mtoto na hivyo kujenga taifa lenye afya bora, Tatizo hili ni kubwa na uhaba wa wataalamu hawa ni mkubwa hivyo tunawasihi watanzania kujumuika katika mbio hizi kuchangia upatikanaji wa fedha ili tuweze kukabiliana na uhaba huu kwa pamoja” alisema.
Usajili wa mbio za NBC Dodoma Marathonumefunguliwa rasmi hivyo washiriki wanaweza kujisajili kupitia tovuti ya www.nbc.co.tz na kuchangia kiasi cha TZS 30,000 kwa usajili au25,000 kwa kundi la watu ishirini na zaidi. Kwa maelezo zaidi tembelea matawi na vituo vya usajili vitakavyowekwa na NBC.
KUHUSU BENKI YA NBC
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ni Benki kubwa nchini yenye kutoa huduma kwa makundi yote ya wateja kupitia mtandao mpana wa matawi, wakala ATM, na Mashine za malipo(POS). Benki ya NBC pia inatoa huduma kupitia simu za mikononi na mtandao wa intaneti.
0 maoni:
Chapisha Maoni