WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Alhamisi, 25 Mei 2023

 14:36      No comments

 


Na mwandishi wetu.

Kampuni ya Swissport Tanzania Plc imefanya mkutano mkuu  kwa kukutana na wanahisa waliowekeza katika kampuni hiyo na kujadili ajenda ikiwemo kupitia mahesabu ya kampuni kwa mwaka 2023 pamoja na kupitisha gawio kwa wanahisa.


Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam Afisa Mtendaji Mkuu wa Swissport Tanzania Plc Mrisho Yassin amesema kuwa, katika mkutano huo wamekutana na wanahisa na kupitia ajenda mbalimbali ikiwemo ya kuweka mikakati katika kipaumbele cha mwaka huu wa 2023 kwa kuendelea mbele na kuhakikisha uthabiti katika utoaji wa huduma bora na salama kwa wateja wao pamoja na kufuatilia mwenendo wa biashara ili kuyafikia malengo ya biashara kwa mwaka.


''Katika mkutano huu ajenda kuu ilikuwa ni kupitisha mahesabu ya kampuni kwa mwaka 2023 ambayo wanahisa wameyapitisha, pia kulikuwa na ajenda ya ya kutoa gawio kwa wanahisa na kwa pamoja wanahisa wamepitisha gawio la jumla kwa share anayomiliki.


Mrisho amesema, kwa mwaka 2020 kampuni hiyo haikutoa gawio kutokana na hasara ya shilingi bilioni moja na laki tano waliyoipata kutokana na athari la janga la UVIKO-19 na kwa mwaka 2021 walipata faida ya shilingi bilioni mbili la laki moja na gawio hilo liliingia katika mifuko ya wanahisa Julai, 5 mwaka 2022.



Aidha amesema kuwa, wataendelea kuweka mikakati itakayoiwezesha kampuni kupata faida na wanamatarajio makubwa katika kukuza uchumi wa kampuni hiyo.


Pia Mrisho amesema kuwa wamekuwa wakishiriki shughuli za kijamii kwa kulipa kodi pamoja na kutoa ajira kwa watanzania ambapo hadi sasa wametoa ajira takribani 700 na baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuzindua Royal Tour tayari wameanza kupokea watalii wengi na kuwahudumia kupitia anga na wanategemea matokeo chanya zaidi katika kukuza uchumi wa kampuni na Taifa kwa ujumla.


Amesema Uongozi wa Swissport Tanzania ukiongozwa na Mrisho Yassin umejitahidi katika kutekeleza majukumu licha ya kuwepo kwa ushindani mkubwa na makampuni mengine na wameendelea kushikilia soko la huduma za ndege kwa asilimia 90 kwa ndege zinazoingia Tanzania

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *