WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumanne, 23 Mei 2023

 14:08      No comments

Na. Jerome Mlaki wa DAR.

Kiza Mayeye akiwa bungeni.

ALIYEWAHI kuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kigoma kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF Kiza Mayeye amejiunga na Chama cha ACT Wazalendo.

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam wakatia akipokelewa Mayeye ametoa tamko la kuachana na CUF na kujiunga na ACT.

Mayeye ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake CUF (JUKE) amekishukuru chama cha CUF kwa kumlea, kwamba amekitumikia kwa nafasi mbalimbali tangu mwaka 2011 nilipojiunga nacho.

“Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipokishukuru Chama cha CUF kwa kunilea kiuongozi na kunipa fursa mbalimbali kukitumikia,” amesema Mayeye na kuongeza,

“Leo, nimelazimika kuchukua maamuzi haya magumu kwa sababu ambazo haziwezi kuzuilika,”.

Ametaja sababu hizo akieleza kwamba, Mosi true ni mwanasiasa wa vitendo.

Hivyo anaamini siasa halisi ipo chini (field), kwa wananchi kwamba  Mwaka 2020 aligombea Ubunge katika Jimbo la Kigoma Kaskazini na kwa matokeo halisi nilishinda.

“Lakini, kilichotokea mwaka 2020 sote tunakifahamu; walioshinda walishindwishwa na walioshindwa walishindishwa!,” ameeleza Mayeye.

Kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipotangaza kuwa amekuwa mshindi wa pili kwa kupata kura 16252 kila mmoja alishangaa.

“Bila shaka hata CCM wenyewe walishangaa, kwa sababu walijua nilishinda!,” amesema Mayeye.

Mayeye ameeleza kuwa anajiunga na ACT Wazalendo ili kuendeleza mapambano.

Amesema amefanya uchambuzi wa kina na kujiridhisha kuwa ACT Wazalendo ndio jahazi sahihi la kuendeleza harakati zangu kwa ajili ya kuwakomboa wanachi wa Kigoma Kaskazini, Mkoa mzima wa Kigoma na Tanzania kwa ujumla.

Kwamba amevutiwa sana na sera za ACT Wazalendo za kujenga Tanzania ya wote kwa maslahi ya wote.

Mayeye ameendelea kueleza kuwa ameshawishika pia na jitihada za Chama kuimarisha mtandao wake nchi nzima.

Vile vile amevutiwa pia na jitihada za Chama kukuza vipaji vya vijana na wanawake.

Ameeleza kabla hajafanya uamuzi huu amezungumza na vyama vingi ili kufanya utafiti kabla ya kujiunga na Chama husika.

“Mwishowe nikafanya hitimisho kuwa ACT Wazalendo ndio jukwaa sahihi. Wale ambao walitarajia nitajiunga nao, waniwie radhi, vigezo vya kisayansi vimenipeleka ACT Wazalendo,” ameongeza Mayeye na kubainisha,

“Nimekuja kuongeza nguvu kwenye ujenzi wa Chama katika kujihakikishia ushindi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025,”.

Amebainisha kwamba hivi karibuni anatarajia kwenda jimboni Kigoma Kaskazini ambapo atakwenda kueleza kwa kina zaidi kwa nini Chama hiki kinapaswa kuwa tumaini lao kutokana na utafiti na  uchambuzi wa kina alioufanya.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Tanzania Bara Dorothy Semu amemkaribisha mwanachama huyo mpya ndani ya chama

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *