Date: October 27, 2022Author: torinto hot media
Na Jerome Mlaki wa DAR.
Waziri wa Mali Asili na Utalii Balozi Dkt.Pindi Chana amesema kwa sasa sekta ya utalii ni soko kubwa la kuzalisha ajira na kuongeza pato la taifa hivyo jitihada mbalimbali zinaendelea kufanyika kuboresha Sekta hiyo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa wataalamu wa mafunzo ya utalii kutoka vyuo vya utalii Balozi Chana amesema serikali kwa kushirikiana na wadau wa utalii wameendelea kutangaza vivutio mbalimbali vya utaliu vilivyopo nchi hususani kusini mwa Tanzania ili kuwavutia wawekezaji.
Aidha amewataka waeekazaji wa hoteli kuwekeza katika hifadhi za taifa zilizopo katika mikoa ya kusini nwa Tanzania katika Masuala ya hoteli nasehemu za kulala wageni ili kuweza kuboresha Sekta hiyo.
” Maeneo ya Uwekezaji wa Hoteli na sehemu zakulalawageni bado ni hitaji kubwa katika utalii wa kusini mwa Tanzania hivyo wawekezaji wachangamkie fursa hiyo” Amesema Balozi Chana.
Hata hivyo amesema kumekuwa na mwitikio mkubwa kwa watalii kutokana na filamu Royal Tour idadi kubwa ya watalii wamekuwa wakija nchini Tanzania hivyo nifursa kwa wafanyabishara wa sekta ya utalii kukuza Biashara zao kupitia Sekta hiyo.
Kwa upande wake Kaim Afisa Mkuu wa Chuo cha Utalii Dkt. Florian Mtei amesema katika mkutano huo watapitia tafiti zilizofanywa na wataalamu kutokana nchi mbalimbali ikiwemo Afrika Kusini kuangalia changamoto zilizosababishwa na janga la Covid 19 na jinsi ya kukabiliana nazo ili kukuza sekta ya utalii.
Sambamba na hayo amesema kuwa kupitia mkutano huo wataweza kuweka mikakati kama nchi kuangalia njia gani wanazoweza kufanya kuepukana na majanga kama Covid 19 yanayoisumbua Duniani.
0 maoni:
Chapisha Maoni