Torinto hot media Blog.
Na Jerome Mlaki wa DAR.
Katibu Mtendaji wa BASATA Dkt. Kedmon Mapana akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es salaam.
Mwanzilishi wa tuzo za Road To Uni Awards Joseph Ndalo akielezea maandalizi ya Tuzo hizo na namna ambavyo watashiriki katika tuzo hizo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es salaam.
Katika kuhakikisha vipaji vya vijana katika tasnia ya sanaa vinakua Serikali kupitia Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limesema litashirikiana na Road To Uni Awards kufanikisha utoaji wa tuzo za vijana wenye vipaji vyuo vikuu zinazotarajiwa kufanyika Novemba 14 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa BASATA Dkt. Kedmon Mapana amesema tuzo hizo zilizoanzisha na vijana hao kwa msimu wa nne sasa zinalenga kuibua vipaji na kukuza tasnia ya sanaa nchini.
“Serikali ina nia ya kuendeleza vipaji vya vijana ambavyo ni ajira kwao hivyo tupo hapa kuwaunga mkono vijana wetu wa vyuo vikuu katika kutimiza adhima yao ya kuona kila kijana mwenye kipaji anapata fursa ya kukuza kipaji chake ambacho kitampatia ajira na kipato na pia kuitangaza Tanzania yetu” Amesema Dkt Mapana.
Aidha amesema shindano hilo la msimu wa nne litahusisha washiriki 119 kutoka vyuo mbalimbali nchini ambapo amewataka vijana kujitokeza kushiriki katika nashindano hayo ili wazidi kuwa na wigo mpana wa kufahamika.
Sambamba na hayo amesema kuwa Baraza pia linaweka mfumo wa kuwatambua wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo ya sanaa katika shule za msingi na sekondari kwa kuwapatia vyeti ba zawadi mbalimbali.
Kwa upande wake mwanzilishi wa tuzo za Road To Uni Awards Joseph Ndalo amesema lengo la tuzo hizo ni kuwapata wanasanaa wasomi ambao watalimudu soko la ushindani la sanaa Duniani.
Hatahivyo amesema wameshatembelea vyuo mbalimbali nchini na Oktoba 28 mwaka huu wanatarajia kuendelea na ziara yao Jijini Dar es Salaam ambapo wataanzia katika chuo cha City College ambapo mwaka jana kilifanikiwa kutoa mshindi katika tuzo hizo.
Amesema kuwa vipengele vitavyoshindaniwa ni pamoja na mwimbaji bora wa nyimbo za Injili, Singeli, hipapu, kaswida, mchekeshaji bora, mpigapicha bora pamoja na wabunifu wa mavazi.
0 maoni:
Chapisha Maoni