Na Jerome Mlaki wa DAR.
Tuzo za Vijana jumuaya ya Africa Mashariki zimezinduliwa rasmi hii Leo jijini Dar Es Salaam.
Tuzo hizo zimezinduliwa na Balozi wa Uganda mapema asubuhi katika hoteli ya Rotana iliopo katikati ya Jiji Dar
Tuzo hizo zinalenga kutambulisha kazi Bora zinanofanywa na Vijana wa jumuiya ya Africa Mashariki wabunifu wanaoendeleza VIPAJI VYAO katika kutatua changamoto kadhaa za ajira.
Ukubwa wa tuzo hizo umeelezwa vizuri na Haji Manara almaarufu Bukati. Yakwamba tuzo hizo zinatoa hamasa kwa Vijana wa East Africa Mashariki kuchochea VIPAJI VYAO katika Kubuni vitu vyenye uwezo wa kutatua changamoto za ajira.
Nae mwenyekiti wa tuzo hizo Mh Richard Kasesela amewataka Vijana kuendeleza ubunifu ili kujenga uwezo wa kupokea tuzo hizi zitakazo watambulisha wao na kazi zao
Spika mstaafu Bunge la Vijana Jumuiya ya Africa Mashariki Mh. Helen Mollel ambaye ndie mwanzilishi wa Tuzo hizo amesema kuwa Ipo haja ya kuthamini kazi za Vijana wabunifu wa jumuaya ya Africa Mashariki ili kuwapa hamasa kuendeleza ubunifu na kutatua tatizo la Ajira nchini.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Africa Mashariki EAST AFRICA YOUTH AWARD MH. Richard Kasesela Akiwa na Balozi wa Uganda wakiteta jambo ktk hafla ya uzinduzi huo.
0 maoni:
Chapisha Maoni