Torinto Hot Blog.
Na. Husein Ndumbikile Dar.
Tanzania
inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Majaji na Mahakimu unaotarajiwa
kufanyika mkoani Arusha kuanzia Juni 11 hadi 13 mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha
(AICC).
Akizungumza
na wanahabari leo jijini Dar es Salaam Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya
Tanzania, Dk. Elieza Fereshi amesema mkutano huo utajadili mada na mijadala
mbalimbali ikiwemo ya usawa wa kijinsia katika katika utoaji na upataji haki
pamoja na washiriki kubadilishana uzoefu katika masuala ya utendaji.
“ Wageni
wameshaanza kuwasili tunategemea majaji wakuu wengi kushiriki mkutano utafungua
fursa kwa washiriki kujadili na kuweka mikakati itakakayosaidia kuboresha utendaji
kazi wa mahakama,” amesema.
Amebainisha
kuwa katika mkutano mijadala na changamoto zitajadiliwa ili kupata maazimio
yatakayoingiwa kwa pamoja na washiriki lengo likiwa kuwasaidia katika utendaji
wao.
Amesisitiza
kuwa suala la jinsia litajadiliwa kwa kuangalia jinsi gani haki za kisheria
zinalindwa katika utoaji na upataji haki kwa kuwashirikisha wadau wa madawati
ya jinsia na washiriki wa mkautano huo.
Kwa upande
wake, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Catarina Revocati amesema mkutano
huo utashirikisha nchi 51 za Afrika huku akibainisha kuwa siku ya kwanza
kutakuwa na wajumbe 200 na kwamba siku zitakazofuata watafikia wajumbe 350 hadi
400.
Ameongeza
kuwa katika mkutano huo mpango mkakati ni kuangalia suala la ufikiwaji wa haki
kwa wote bila kujali jinsia.
MWISHO
0 maoni:
Chapisha Maoni