Torinto Hot Blog.
Na. Benny Mwaipaja, Kondoa.
SPIKA
wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amewataka watanzania kuwa na
uvumilivu wa masuala ya kidini ili nchi iendelee kuwa na amani, utulivu
na maendeleo.
Ndugai
ametoa wito huo katika Kata ya Pahi wilayani Kondoa mkoani Dodoma,
alipokuwa akizungumza wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur'an
yaliyowashirikisha zaidi ya watoto na vijana 40 kutoka maeneo mbalimbali
ya nchi.
Spika
Ndugai ameeleza kuwa umoja na mshikamano uliopo hapa nchini ni matokeo
ya viongozi wa dini mbalimbali hapa nchini kuendelea kuhubiri amani na
utulivu na kuitaka jamii na viongozi hao kuiendeleza kazi hiyo
Kwa
upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba,
ameitaka jamii kuendelea kupiga vita uhalifu na kuwafichua wahalifu
popote walipo ili nchi iendelee kuwa na amani.
Mratibu
na Mwandaaji wa mashindano hayo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema
kuwa lengo la mashindano hayo ya kuhifadhi Qur'an Tukufu ni kuwajengea
vijana maadili mema ili waweze kushiriki kikamilifu kuleta maendeleo ya
taifa.
Mgeni
Rasmi katika Mashindano hayo, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustapher
Shabaan amewapongeza vijana walioshiriki mashindano hayo na kuonesha
umahili mkubwa wa kuhifadhi qoran na kuwataka waumini wa kiislamu kusoma
na kukielewa kitabu hicho kitukufu kwa kuwa kimejaa elimu na maarifa
mengi yatakayo wasaidia kuenenda vyema katika jamii na kupata thawabu
kutoka kwa Mungu.
0 maoni:
Chapisha Maoni