Torinto hot blog.
Na Jerome Mlaki Dar.
Waziri
wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa
Idara ya Sheria na Usajili wa Jumuiya za Kidini na Vyama vya Kijamii ili
kupisha uchunguzi wa barua iliyoandikwa ukililenga Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri Tanzania (KKKT).
Waziri Nchemba amesema hayo leo Ijumaa Juni 8, katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
“Huo
waraka una maudhui kama matatu, ni waraka batili na tunaendelea
kuchunguza kama umeyengenezwa basi umetengenezwaje, kwani haujapita
kwetu.
“Hivyo
basi, namsimamisha Msajili wa hizo taasisi kupisha uchunguzi na
ikithibitika ni za Wizara tuweze kujua maana jambo hilo halijapita kwa
Waziri, Katibu Mkuu na wala si maelekezo ya serikali,” amesema.
Hata hivyo, Waziri Mwigulu aliuita waraka huo ni batili kwa kuwa haukukidhi viwango vya uandishi wa nyaraka za serikali.
0 maoni:
Chapisha Maoni