TORINTO HOT BLOG.
Na. Jerome Mlaki Dar.
Waziri
wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage ameipongeza kampuni ya mafuta
ya TOTAL kwa kuwa mstari wa mbele kwenye kuhakikisha kuwa watanzania
wanapata mafuta bora ya vyombo vya moto.
Mwijage
alizungumza jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa mafuta ya vyombo
vya moto aina ya TOTAL Excellium kutoka kampuni ya mafuta ya TOTAL.
Mafuta hayo yaliyotengenezwa kwa teknolojia ya ubora wa juu ya kimataifa
ya TOTAL EXCELLIUM, kwa bidhaa zinazotumia mafuta ya Petroli na Diesel
katika soko la Tanzania.
“Uzinduzi
wa mafuta haya umekuja wakati muafaka kwani sasa tuko kwenye wiki ya
mazingira na mafuta haya yanapunguza uchafuzi wa hali ya hewa utokanao
na vyombo vya moto, nawapongeza kampuni ya TOTAL kwa kuwaletea
watanzania bidhaa bora, na mimi na utaalamu wangu wa mafuta nafahamu hii
ni hatua kubwa sana kwenye teknolojia ya kuboresha mafuta,” alisema
Mwijage.
Mafuta
haya mapya yana uwezo wa kusafisha injini na kuwezesha injini kufanya
kazi kwa kipindi kirefu, kuwezesha matumizi kidogo ya mafuta na
kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa utokanao na moshi wa vyombo vya moto.
Mafuta
ya TOTAL EXCELLIUM yanapatikana katika vituo vyote vya kuuza mafuta vya
kampuni ya TOTAL kwa gharama ya bei ya kawaida ya mafuta kwenye soko.
Tarik
Moufaddal, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya TOTAL nchini
anasisitiza, “Kuzinduliwa kwa TOTAL EXCELLIUM, katika soko la Tanzania
ni hatua mpya na muhimu kwetu nchini hususani katika kufanikisha dhamira
yetu ya kuingiza bidhaa bora za nishati. Tunayo dhamira ya kuwapatia
wateja wetu bidhaa zenye ubora wa hali ya juu, sambamba na huduma bora
kupitia mtandao wetu ambao umeenea nchini kote, uzinduzi wa TOTAL
EXCELLIUM, unadhihirisha kuwa tumejipanga kuleta mapinduzi yenye kuleta
manufaa katika sekta ya mafuta nchini.”
“TOTAL
EXCELLIUM imetengenezwa kwa teknolojia ya juu ya kisasa ambayo
inawezesha kusafisha injini, kuwezesha injini kufanya kazi kwa kipindi
kirefu bila kuchoka, matumizi kidogo ya mafuta kuendesha injini,
kupunguza uchafuzi wa mazingira utokanao na moshi na ni mazuri kwa
matumzi ya aina zote za magari kuanzia madogo mpaka makubwa,” aliongeza
Tarik.
“Uzinduzi
huu ni moja ya ubunifu mkubwa wa kampuni uliolenga kuhakikisha wateja
wetu wanapata bidhaa bora na kuwawezesha matumizi kidogo ya mafuta
yaliyotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa ya Excellium.
"TOTAL
EXCELLIUM imetengenezwa kwa ubunifu wa teknolojia za kisasa zenye
kuleta ubora. Timu yetu ya wataalamu wa utafiti wamefanikisha
kutengeneza mafuta haya kukidhi mahitaji ya wateja wetu wanaotumia
magari ya kisasa ambayo yanahitaji umakini mkubwa katika matunzo ya
injini kwa matumizi yao ya kila siku” Mkurugenzi wa Mtandao wa TOTAL wa
Nikesh Mehta.
“Zaidi
ya watafiti makini na wataalamu wenye uzoefu mbalimbali wanafanyia kazi
suala la kuleta bidhaa za mafuta na vilainishi vya injini na mitambo
zenye ubora mkubwa zaidi katika kituo chetu cha utafiti cha
Solaize,nchini Ufaransa.Wataalamu hao wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa
zaidi ya miaka miwili kuboresha mafuta ya TOTAL EXCELLIUM.
"Zaidi
ya kanuni za kisayansi 2,300 zimefanyiwa majaribio katika maabara kwa
zaidi ya masaa 6,000 na mafuta haya yamefanyiwa majaribio ya awali
barabarani kwa zaidi ya masaa 8,500 sawa na kilometa 300,000.
"Haya
yote yanathibitisha uhakika na ubora wa mafuta ya TOTAL EXCELLIUM na
yanasafisha injini za magari na kupunguza uharibifu wa mazingira,”
anasema Marsha Msuya, Mkurugenzi wa Masuala ya Ndani ya kampuni ya TOTAL
0 maoni:
Chapisha Maoni