WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumatatu, 11 Juni 2018

 04:30      No comments




NA JEROME MLAKI DAR.

MKUU wa Wilaya ya Ilala SOPHIA MJEMA amewataka watendaji wa Manispaa hiyo na Watumishi wake kufanya kazi kuacha kubweteka. 

Mjema aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati wa kikao maalum kilichoandaliwa na manispaa ya Ilala cha kutoa majibu ya ufafanuzi wa kero zilizowasilishwa wakati wa ziara ya MWENYEKITI WA Chama cha mapinduzi mkoa wa Dar esSalaam  Cathe Kamba. 

"Nawakumbusha kila mtumishi kusimamia majukumu yake msivuke mipaka katika utekelezaji wa kazi zenu. "alisema Mjema. 

Alisema watumishi na Watendaji wa Ilala watakaokiuka misingi ya kazi watachukuliwa hatua Kali. 

Amewataka wafanye kazi kwa weledi pia washirikiane katika kutatua changamoto mbalimbali za wananchi wa Ilala. 

Alisema kikao hicho kilikuwa kinawahusisha watendaji wa idara zote za I LALA wakiwemo chama na serikali,  Idara, AFYA, Mazingira, Maendeleo ya Jamii, Tasaf, elimu msingi na sekondari  ,idara ya usafishaji,   ambapo zote zilitolewa majibu.

Kwa upande wake Katibu wa ELIMU na mazingira jumuiya ya Wazazi WILAYA ILALA Wilson Tobola alipongeza ofisi ya mkuu wa WILAYA ILALA  
Kutolewa majibu ya kero zilizojitokeza katika ziara ya MWENYEKITI wa CCM Mkoa.

Tobola Alisema  tumepokea kwa Furaha majibu hayo wanasubiri utekelezaji wake watendaji wa serikali tunawaomba wawajibike wasikae ofisini washuke chini kusikiliza kero za wananchi. 


"Tunawaomba watumishi wetu wa Ilala washirikiane na mkuu wetu wa WILAYA 
Kutatua changamoto pia waweke utaratibu wa kutembelea wananchi kila mwenye idara yake "alisema Tobola. 

Alisema kwa upande wa chama na jumuiya ya Wazazi wameaidi kupokea maelekezo na kuyafanyia kazi kwa ushirikiano wa ofisi ya wilaya ILALA kwa faida ya wananchi.

Alimpongeza mkuu wa wilaya Ilala SOPHIA MJEMA kwa kuwaunganisha jumuiya zote pamoja na chama cha mapinduzi CCM.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *