Na Jerome Mlaki
MANISPAA ya Ilala imetakiwa kuanzisha klabu za mazingira katika shule zake za msingi za manispaa hiyo ili wanafunzi wafundishwe umuhimu wa utunzaji mazingira.
Ushauri huo umetolewa Dar es Salaam jana na Ofisa Tawala wa Wilaya ya Ilala Jabiri Makame wakati wa kampeni ya upandaji miti shule msingi Yongwe iliyopo Chanika ILALA.
"Naomba Idara ya Mazingira manispaa ya Ilala muunde vilabu vya mazingira katika shule zenu za msingi ili wanafunzi wafundishwe umuhimu wa utunzaji wa mazingira"alisema Makame.
Makame alisema suala la utunzaji wa mazingira ni letu sote hivyo inatakiwa tuweke mikakati mbalimbali jinsi ya uendelezaji na utunzaji wa mazingara.
Alisema ikiwekwa mikakati endelevu ya kuanzisha vilabu mashuleni wanafunzi wakafahamu jinsi utunzaji mazingira serikali itakuwa imefaidika jamii nzima itapata elimu hiyo.
Amewapongeza Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa juhudi zao kwa kuwekeza shule za msingi hasa upande wa mazingira na kuwataka wadau wengine Kushirikia na serikali.
Alisema utunzaji wa mazingira unafaida nyingi nchi yetu inaepuka jangwa,faida nyingine miti inaleta kivuli na miti mingine ya matunda.
Kwa upande wake Ofisa Elimu Msingi Ilala Elzabeth, thomas alisema Standard Chartered wameanza kampeni ya kusaidia shule za Msingi Ilala toka mwaka 2014 mpaka sasa wameweza kupanda miti 3300.
Thomas alisema kuanzia mwaka 2014 hadi sasa wamekuwa wakishirikiana katika utunzaji wa mazingira katika shule mbalimbali.
Alisema awali kabla kupanda miti SHULE ya Yongwe kampeni hiyo ilianzia shule ya msingi Majani ya Chai, Pugu Kajiungeni, Buyuni, Kigogo Freshi, Viwege na Uhuru Mchanganyiko.
Kwa upande wake Ofisa wa Benki hiyo Isema Bilali alisema benki hiyo ilianza shughuli zake nchini mwaka 1917 na baadae mwaka 1993 mara baada kuundwa kwa azimio la Arusha ambapo kwa sasa inashirikiana pia na serikali katika shughuli za kijamii.
Bilali alisema upandaji miti una faida nyingi ikiwemo kutuwezesha kupata mvua,ujenzi,inatupa chakula inazuia mmomonyoko wa udongo.
0 maoni:
Chapisha Maoni