WELCOME TORINTO HOT MEDIA BLOG | FOR MORE INFORMATION ABOUT OUR NEWS CONTACT US CELL: +255 756 188 180 | Email: josephlieme@gmail.com| KARIBU TORINTO HOT MEDIA BLOG | KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU HABARI ZETU WASILIANA NASI SIMU: +255 756 188 180 | Barua Pepe: josephlieme@gmail.com | DO YOU NEED TO DEVELOP YOUR BLOG CONTACT US CLICK HERE | JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Jumatano, 30 Mei 2018

 04:44      No comments


Na Jerome Mlaki.
Mwakilishi wa Jimbo la Jang’ombe visiwani Zanzibar, Abdallah Maulid Diwani amevuliwa uanachama wa CCM na Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), kwa kosa la kukiuka maadili ya chama cha Mapinduzi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole, Mwakilishi huo wa Jimbo la Jang’ombe, amefukuzwa uanachama kwa kwenda kinyume na maadili na miiko ya viongozi wa CCM.

“Kikao pia kimetoa karipio kwa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki, Fancy Nkuhi na Mariam Ussi Yahya kwa mwenendo usioridhisha, usiolinda maslahi ya nchi na unaokinzana na misingi na miiko ya uongozi na wamewekwa chini ya uangalizi wa kimaadili kwa miezi 18,” imesema taarifa hiyo ya Polepole.

Katika kikao hicho Rais John Magufuli pia imeazimia mapendekezo yote ya Tume ya Rais ya uhakiki wa mali za chama yafanyiwe kazi mara moja na chama chenyewe chini ya Baraza la Wadhamini na Uongozi wa Katibu Mkuu, wenyeviti na makatibu wakuu wa jumuia zake

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kurasa

Translate

Popular Posts

Blog Archive

Tangazo!

JE UNAHITAJI KUBORESHA BLOG YAKO?

WEIGHT MANAGEMENT

WEIGHT MANAGEMENT

SIKILIZA NYIMBO MPYA

Watembeleaji

On Facebook

Tangazo Victoria!!

Date & Time

Weight Management



CLICK THIS IMAGE

Sikiliza Clouds Radio



Sikiliza Kwanza Jamii Radio

Total Pageviews

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *